Lema mwanasiasa Bora wa Mwaka 2011

Bado tunasubiri akimaliza harakati labda atakumbuka.

Mkuu Ngongo..
Habari za sikukuu? Vipi mradi wa Machinga Compelex na Barabara za juu alizosema Lema wakati wa Kampeni zimefikia wapi?
 
JF imekuwa kisiwa cha wapambe wa Lema. Kila siku watu wanaanzisha thread zinazomhusu wakati kiuhalisia hamna alichikifanya zaidi ya kuifanya Arusha kuwa uwanja wa vita.

Ole wao wenye macho lakini hawataki kuona!
Wenye masikio lakini hawataki kusikia!
KAMA WEWE!
 
Feedback.

Arusha hakuna barabara ya lami sana sana tunatarajia mradi wa kuboresha miundombinu ya Jiji itaanza mwakani pita pale Arusha Sec uwanja wa mpira kuna kampuni ya kichina imeshaanza kuleta vifaa.Ikumbukwe mradi huu unafadhiliwa na WB chini ya mpango wa maboresho ya Jiji la Arusha bila kusahau madiwani wa CDM hawashiriki vikao vya baraza la madiwani hivyo sifa zinaweza kuchukuliwa na kile chama cha magamba ahaaa aa.
Kwa hali hii tutanunuliwa suti hadi nguo za ndani unashangilia kufadhiliwa na kujengewa na wachina.
 
Feedback.

Sasa wewe unatarajia nini kama mbunge anakesha mochuary akiomba maiti ifufuke ?.Kama haitoshi tunaambiwa eti ndiyo mwanasiasa bora wa mwaka 2011 bora wangesema mwanasiasa mtata wa mwaka 2011 ningeelewa.



Kwa hali hii tutanunuliwa suti hadi nguo za ndani unashangilia kufadhiliwa na kujengewa na wachina.
 
Ndiyo maana nikasema hivi kwa ajili ya kufupisha mjadala, tufanye Manispaa ya Arusha haina Lami hata Moja kama unavyodai. Sasa na wewe utueleze hukumu yako dhidi ya Lema kutokana na Manispaa ya Arusha kutokuwa na Lami.

Tumbiri.

Kumbuka kuwa sote tunaijua arusha vilivyo sana. Sasa tuwekee basi au tutajie basi barabara ya Lami inayomilikiwa na manispaa ya Arusha mjini? na sio kufanya assumption.

Kumbuka kuwa tunachoandika tuna uhakika nacho kwa 100%. sasa kama wewe una mushkeri na maneno yetu. Tunainishie basi ukweli upo wapi na sio kuleta lugha za assumption.

Tunasubiri list ya barabara za manispaa ya Arusha town zenye lami kama hu msema kweli?

 
aah kweli kama ndo pinda aliyoongea mhe. alisema uongo na kulidnganya bunge, alipaswa kuiga nyayo za EL
 
Ahsante Ngongo,

Ni vizuri uwajulishe kuwa manispaa hiyo haina hata barabara moja ya Lami. Zote wanazoziona zinamilikiwa na Tanroad. Na wajuze wajue kuwa kuna barabara za manispaa/ halmashauri na barabara za Tanroad.


Mkuu Barubaru, ni manispaa chache sana hapa TZ zina ubavu wa kujenga barabara za lami. Hata Dar yenyewe zipo chache sana na ziko sub-standard. Labda utujuze huko kwenu mmefanyaje kuweza kutandika mkeka wa lami kila mahali:)
 
feedback.

Sasa wewe unatarajia nini kama mbunge anakesha mochuary akiomba maiti ifufuke ?.kama haitoshi tunaambiwa eti ndiyo mwanasiasa bora wa mwaka 2011 bora wangesema mwanasiasa mtata wa mwaka 2011 ningeelewa.

acha kumdhihaki, mbona ww unaenda kusali katika dini yako lkn umejaa uovu mwingi, lazima tuyainue yaliyo mazuri aliyofanya

kwa mfano hiyo maiti ingefufuka, ungesemaje, acha kubeza imani ya mweznio, tujadili mambo ya msingi aliyofanya kwa lengo la kulikomboa taifa kimaendeleo
 
Mkuu Barubaru, ni manispaa chache sana hapa TZ zina ubavu wa kujenga barabara za lami. Hata Dar yenyewe zipo chache sana na ziko sub-standard. Labda utujuze huko kwenu mmefanyaje kuweza kutandika mkeka wa lami kila mahali:)


Naomba nitajie ni manispaa gani huko Tanzania isiyo na barabara hata moja ya Lami zaidi hiyo ya Arusha mjini? Mimi naomba hata ikiwa substandard lakini iwe ya Lami.

Kumbuka kuwa kuna Halmashauri na Manispaa. Hivyo ni vitu viwili tofauti. Sasa nitajie Manispaa gani zaidi ya Arusha town isiyo na barabara ya Lami?
 



hapo kwenye Red Lema ameyafanya hayo!..? Je kuwaambia watu waandamane na kijipeleka jela ... kuingilia siasa za NCCR ... ndiyo defn. yako ya mobilization ..?!

bado me bado am sticking on my point mwakilishi mzuri ni yule ambaye maendeleo jimboni mwake angalau yanaoneka .. hata kama hatumuoni kwenye TV & Magazeti, Maandamo & vurugu na mapolisi kila siku . lakini anaonekana jimboni kwake..


toa mfano basi... Alitakiwa afanye kama yupi na yupi...
 
Luteni,

Je unajuwa ni kuwa jimbo lake la Arusha mjini halina hata Kilometer moja ya Lami.

Je Lema ameshaweka lami japo hata Km Moja tokea aingie madarakani? Je maendeleo gani aliyowaletea wapiga kura wake? mpaka awe mwanasiasa bora?

kilometa 1 ya lami unajua gharama zake.. Na mambo ya barabara,kwani kodi ya wana Arusha inaenda wapi..
 
Mpaka akumbuke tena? Vipi na kuhusu kufufua wafu kafanikiwa?
Hahahaha ritz..umenikumbusha ukilaza wa huyu mheshimiwa. Hivi kwanini huwa anapenda sana kuongoza mazishi? Nimeshamuna kwenye kamati nyingi sana za mazishi. Halafu lazima kwenye kila msiba atoe waraka!!!
 
Tumbiri.

Naomba ujue siku zote wananchi hawataki malumbano bali wanataka maendeleo. Na Mbunge ndio mwenye dhima kubwa sana katika kuchochea maendeleo ya jimbo lake akishirikiana na wananchi wake. Kwani ni yeye anawawakilisha wapiga kura wake ndani ya chombo kikuu cha kutunga sheria na kupatisha bajeti ya nchi.

sasa tuweke wazi je amewasaidia nini wananchi wake?

kwani haingii bungeni?? Au akiingia hawashi mic na kutoa michango yake kwa spika? Je kazi za madiwani nazo unazijua? Una uelewa wa mambo ila unaongozwa na chuki kwa vyama vya upinzani!
 
Hivi mbona Lema ana washabiki wengi hivyo humu lakini simwoni?

Ama anatumia id gani?

Kuna yule ndugu alikuwa na avatar ya mtoto wa kichina china, nimesahau jina...

Labda angekuwa anajuwa somting about nothing
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom