LEMA mikononi mwa LISSU...

Kusikilizwa ni tarehe 20 Sept 2012 na hukumu huenda ikawa tarehe 22 Sept 2012
 
Maundumula humjui Lissu Tundu A.Mughai, wee kaa kimya uone kitakachoendelea.. Yule ambaye Lissu hana imani naye (Judge Mbarouk) keshaondolewa na saa hii yuko uingereza eti anajiendeleza na badala yake Judge Mkuu atakuwepo....Naye atakabiliwa na hoja ambazo hana ubavu wa kuzikwepa.
 
Chande ameshtuka na kumuondoa yule jaji mwenye sifa za kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo, kukosa kufanya hivyo, tasnia ya sheria ilikuwa inaandika kitabu kipya.

Hizo sifa ni za karani mkuu siku hizi hakimu mahakam ya mwanzo lazima awe na degree waliojariwa mwaka huu wote wana degree na wamepita law school ukiwa na diploma ya sheria unaajiriwa kama karani
 
Alishashirikiana na Kimomogoro wakaandika rufaa hiyo kurasa 930 kama sikosei. Hatma yake ni tarehe 20/9/2012
 
HILI LA JWTZ KUDAIWA KUONEKANA KURANDARANDA OVYO KWA MAKUNDI KATIKA MITAA MBALIMBALI NCHINI NA 'UGENI WA GHAFLA' WA RAIS KIKWETE KENYA ...???

Tangu WaTanzania kushuhudia kero na ukatili wa kihistoria uliovuka mipaka ya Jeshi la Polisi kumfumua utumbo nje mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, watu wengi sana huku uswahilini wala hatujajua kitu tabasamu kwa hili li-serikali li-ovu linaloongozwa na Rais Kikwete.

Hakika tangu damu imwagike machoni mwetu mchana kweupe mkoani Iringa kwa namna ambayo imepata kuitisha ulimwengu mzima, ni wazi kwamba WaTanzani tulio wengi kiwango chetu cha HASIRA DHIDI YA SERIKALI YA CCM hivi sasa imepanda maradufu zaidi ya kule nyuma tulipochakachuliwa kura zetu hivyo kwa sura halisi ilivyo, kamba laweza kukatika wakati wowote penye hata jambo dogo tu ilmradi watu wapate pa kumalizia hasira zao.

Na kama kumbukumbu zetu ni sahihi, kesi ya maonevu makubwa kwa yule Mbunge lulu kwa vijana kote nchini Tanzania ndio kama hivyo inatazamiwa kusikilizwa hivi karibuni. Hii inamaana kwamba karibia wote watakua wakiangalia kama kuna chao kwa mbunge huyu pale Arusha au ndio kusema ubabe wa Magogoni sharti lipewe njia.

Hadi hapo hofu yetu ni kwamba, kwa matumizi zaidi ya dola mitaani tuwatisha wananchi, endapo uonevu utaendelea kupewa nafasi zaidi, chozi la Daudi Mwangosi huenda likadondoka upya mitaani kote nchini.

Pindi unapoona wanajeshi wakitolewa kwa mara ya kwanza kambini na kuanza kurandaranda ovyo mitaani katika makundi kote nchini, kwa watu makini ni ashirio kwamba kuna baya liko njiani.

Siku zote si kawaida kwa mnyama kakakuona kujitokeza hadharani mitaani hivyo hadi hapo juu ya madai haya ya JWTZ kutengeneza vijiwe mitaani basi mtu usisubiri kuambiwa kwamba tayari HUKUMU KINYUME NA HAKI tayari imeshatoka Magogoni juu ya Ubunge wa Mhe Lema, wiki kadhaa hata kabla ya kesi rufaa yenyewe kuanza kusikilizwa, hivyo wao ni kusubiri tu kuja kutusomea alivyotaka mkuu huyu kama kawaida yake.

Vijana wote nchini macho yetu ni kwenye kesi ya Kamanda Lema Arusha; tumechoka kabisa na maonevu ya Rais Kikwete kutoa maamuzi ya kesi mbaalimbali nchini akiwa Magogoni ... na kama vipi ... !!!
 
Mbona ambao aliwataja wameondolewa na wambaki wale wenye sifa. Kama wewe ni mfatiliaji mzuri, utakuwa unafahamu kuwa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni mmojawapo aliyetajwa na Lissu ambaye hakuwa hata na degree moja ameondolewa kusikiliza rufaa ya Lema kama ilivyopangwa awali. Badalayake ameingia Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman ambaye ataungana Majaji wa Mahakama ya rufaa, Natalia Kimaro na Salum Massati ambao wote ni wa ukweli. Lissu hakusema majaji wote ni feki, ukisoma taarifa yake aliyoipeleka bungeni aliwataja wote kwa majina na mapungufu yao. Nashauri wakati mwingine tuache ushabiki wa kitoto.

Ahsante mkuu kwa kunisaidia kuyaelimisha mambugila kama hilo.
 
Sina imani sna na hyo panel kwa kuwepo j/mkuu mweneywe nadhani ushindi kwa lema utakuwa mgumu. Mtakuja kuniambia!hyu chande alibadilisha majaji kwy kesi ya serukamba ili ccm isipoteze jimbo
 
jamani nijuzeni hiyo rufaa itasikilizwa na kutolewa hukumu lini ili nije A-town kuiona na kiusikia live! maana mie nakaa Nanjilinji.
 
Lissu anaenda mbele ya jopo la majaji ambalo hana imani nalo!

so anataka wakihukumu kinyume na matarajio yake apate kigezo cha lawama?
Hiyo ndio Taaluma yake, Siasa ni mpito kwake. Kama unafuatilia sheria, Hukumu ile imekosa nguvu kisheria
 
jamani nijuzeni hiyo rufaa itasikilizwa na kutolewa hukumu lini ili nije A-town kuiona na kiusikia live! maana mie nakaa Nanjilinji.

Daaaah ! Sikuwezi kama ni mapenzi hayo yako yamekuwa " Mahaba " Usisahau kubeba vitambulisho na namba za simu za dharula maana yanaweza kuibuka makubwa huko. Nakushauri !
 
kila la heri kwa kamanda Lema.
Lissu ataichana chana hukumu ya jaji Rwakibarila.
 
Back
Top Bottom