Lema kuwatoa wafungwa gerezani

Tulikuwa nae mmoja zamani akiitwa Nyerere alizitumia sana hizo sheria kwa ukamilifu wake. Tunashkuru toka alipoondoka yeye hakuna Rais aliyezitumia kama ilivyokuwa kwake.

Islamic propagation at work! Well done.
 
Ukisikia polisi wanasema wanafanya uchunguzi ujue wanatafuta mtu wa kumwachia kesi. Kuna jamaa pale Yombo alimfunga dereva wake eti ameacha kazi. Jamaa alimtafutia vikesi vya kuku na alifungwa miezi sita. Ndugu za yule dereva walishindwa kumtoa lakini hakimu alijua jamaa anamwonea dereva akaipiga chenga lakini mwisho hukumu iliangukia miezi sita wakati jamaa alikuwa anatangaza lazima amlime miaka miwili jela. Na alihukumiwa miezi sita kwa sababu polisi walikuwa wameshachua kidogo dogo. Polisi ndio wanaowafunga watanzania gerezani kwa ubabe wao wa kuweka pesa mbele zaidi kuliko ubinadamu. Mkitaka kujua hujuma zinazotendeka mahakama waweke kipindi, moja kwa moja asubuhi kwenye TV yeyote kama nchi nyingine wanavyofanya, wananchi waone moja kwa moja mambo yanayofanywa na mahakimu wa Tanzania na polisi wanaojifanya watanzania wanavunja sheria.

Hongera Mh Lema sisi tupo nyuma yako.
 
Back
Top Bottom