FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,870
- 109,164
Hapo kwenye red; you're right. Lakini unadhani ni sahihi? Well, utasema sheria zetu na Katiba vinamruhusu lakini bado ni sahihi kwa mtu mmoja kurundikiwa mamlaka na uwezo kama huo?
Mh. J. M. Kikwete ni rais lakini rais si Kikwete! Siku akiibuka mwendawazimu Ikulu hizo sheria tunazoshabikia leo kwa kuwa tu tuko madarakani au chama chetu ndicho chenye dola kuna siku zitatugeuka. Tume ya Jaji Mkuu Mtaafu Mh. Nyalali ilipendekeza sheria za aina hiyo zifutwe lakini kutokana viburi vya watawala wetu hadi leo hakuna kilichofanyika.
Taifa litadumu lakini sisi na vyama vyetu ni wa kupita - Tujenge mazingira bora kwa ajili ya Taifa letu na siyo kwa ajili ya makundi yetu.
Tulikuwa nae mmoja zamani akiitwa Nyerere alizitumia sana hizo sheria kwa ukamilifu wake. Tunashkuru toka alipoondoka yeye hakuna Rais aliyezitumia kama ilivyokuwa kwake.