Lema kuunguruma NMC Jtano

Cha msingi mpeni pole na aendelee kufarijiwa na mumjengee mazingira mazuri ya kupokea rufaa yake . Mhe Othman Chande anasema he is fit and ready kuihalalisha judgement ya Mahakama Kuu.
 
mbona hakuna maamdalizi yoyote pale kinacho jengwa ni ule mtaro wa maji machafu unaoanzia soko kuu mpaka bwawa la mavi..

Arusha kujenga soko la wafanyabiashara wadogo

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha inakamilisha mchakato wa ujenzi wa soko la wafanyabiashara wadogo katika eneo la Uwanja wa NMC, ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 600.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'a, alisema halmashauri hiyo imeshaingia mkataba na Benki ya Uwekezaji (TIB) kupata mkopo wa fedha za ujenzi wa soko hilo ambalo ujenzi wake utaanza hivi karibuni na kukamilika Desemba mwaka huu.

Alisema lengo la kujenga soko hilo ni kuwezesha wafanyabiashara hao kupata eneo lao ili kuepuka kubughudhiwa na kufukuzwa mara kwa mara na askari wa Jiji kutokana na kufanya biashara katika maeneo ambayo hayakuruhusiwa.

Alisema hatua hiyo imefikiwa na kamati ya ujenzi ya madiwani wa halmashauri hiyo na uongozi wa wafanyabiashara hao ambao kwa pamoja walitembelea baadhi ya maeneo yakiwemo ya NMC, Soko la Kilombero na kulipokuwa kituo kidogo cha magari ya kwenda Samunge wilayani Ngorongoro, kwa ajili ya wasafiri waliokuwa wakienda kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile.

Alisema kamati hiyo na uongozi wa wafanyabiashara hao waliainisha maeneo yote hayo lakini wakakubaliana soko lijengwe kwenye Uwanja wa NMC ambalo ni eneo kubwa linaloweza kuchukua wafanyabiashara wengi zaidi kuliko maeneo mengine.
 
Polisi watatoa kisingizio kuwa kesho Jumatano ni Alhamisi ni siku za mtihani wa Darasa la Saba.
 
Back
Top Bottom