Lema: Ikulu imenivua ubunge ; Ikulu yamjibu vikali

Clouds fm ndo ya kwanza eti kuiweka taarifa ya hiyo kurugenzi hewani! kuwa kuwa ni ya huyo boss wenu eeh! tunajua wanyonyaji wakubwa nyinyi.
 
Hana adabu kwa Rais wala Ikulu, kuwahusisha na maamuzi ya mahakama, Ni kipi hujakielewa hapo?

Tena inafaa afunguliwe kesi mpya na akishindwa kuonesha jinsi Kikwete alivyoingilia hukumu ya mahakama aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Lusinde huyu!
 
Hana adabu kwa Rais wala Ikulu, kuwahusisha na maamuzi ya mahakama, Ni kipi hujakielewa hapo?

Tena inafaa afunguliwe kesi mpya na akishindwa kuonesha jinsi Kikwete alivyoingilia hukumu ya mahakama aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Ovyo! wewe mtu aliyekuwa nagombea ubunge na Lema raisi kamfanya balozi wetu kenya! Unataka ushahidi gani Mnyonyaji wewe!
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
clip_image002.png
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yake ya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumu ya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.
Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikulu imeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu ama kuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.
Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumu ama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.
Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakama ambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katika maamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazima atambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.
Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba Bwana Lema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni la kisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.
Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wa kumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hana mtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012

Jamani hapo kwenye nyekundu mpaka lini?Yani Serikali ya Jamhuri ya Muungano inamiliki yahoo.email address Jamani mbona hii aibu miaka nenda ludi nanyi mnaona sawa this is too much.

Tunajua hamkuhusika lakini mahasimu wenu wametumia nafasi hiyo kukuza hizo tuhuma kuwa mmehusika.Hivyo hata CDM waambieni nani kaengineer issue nzima hiyo!!!!!!!!!! vinginevyo patakuwa hapatoshi.!!!!
 
Duh, unaona maelekezo ya ccm, eti akate rufaa!!! Hakuna rufaa. Kikwete na lowassa wana mkono wao bila shaka
 
Hana adabu kwa Rais wala Ikulu, kuwahusisha na maamuzi ya mahakama, Ni kipi hujakielewa hapo?

Tena inafaa afunguliwe kesi mpya na akishindwa kuonesha jinsi Kikwete alivyoingilia hukumu ya mahakama aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.


Mtu aliyekataliwa na wananchi kuwa kiongozi wao wewe unamfanya mwakilishi wetu tena kwenye nchi nyingine! huyo anatuwakilisha sisi au huyo aliyemteua! hii ni wazi aliposhindwa raisi alikasirika sana. Aibu kubwa sana hii.
Kuwa na uongozi kama huu ni bora kukaa bila kiongozi miaka 100
 
Moto utawawakia tu,Ikulu yenyewe haina heshima tena imejaa kubebana bebana tu na kuongopa. Mbona mambo mengi tu ya maana na mazito huwa hawayatolei majibu fasta kama hii ishu ya kamanda wetu Lema? Naamini kwa hili limewagusa na mostly its true.
 
Wala usimlaumu Rweyemamu pengine si hata yeye anayefanya madudu haya mie nahisi ni mkuu mwenyewe! blander prsnt ever seen in dis world
 
mmh YAWEZEKANA RAIS KIKWETE AMEHUSIKA KWA HILI, COZ KWA NINI WATOE RESPONSE YA HARAKA HIVI????, NA RESPONSE WALOTOA NI YA KIMIPASHO HAWAJAJIPANGA KWELI HIYO KABINETI YA TAARIFA ZA IKULU NNA WASI WASI NA TAALUMA ZAO!!!!!!!!!!:A S 39:. KWA WANANCHI KUPUUZIA ILO WASAAU COZ MACHO YOTE NI ARUSHA MJINI. BUT WHATEVER THE CASE PIPO ARE GOIN TO DECIDE.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.

Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.

Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumuama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.

Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.

Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.

Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012

Hv kuna mwana JF anayekumbuka kauli ya jaji Augustino Ramadhani juu ya mhimili wa mahakama kuingiliwa na serikali?kama kuna anaekumbuka basi hakuna haja ya kujadili ***** huu wa kurugenzi ya maelezo Ikulu!
 
kwani hatakama ni kweli wangesema ndivyo? Na hatakama ikulu iliwahikuingilia wangesema ndiyo? Udhani ikulu wanamapenzi na lema?
 
Hivi inakuwaje taarifa inajaa mipasho? Hii idara ya mawasiliano haina weledi wa proper communication skills? Imekaa kama taarabu!
 
upuuuuuuuuuzi mtupu, kwana lema hayupo juu ya sheria na cdm inawanasheria bora, vp rais aingilie upuuzi km huu,lema mwenyewe angalie wapi alikosea na vp imemuharibia
 
Hiyo report yenyewe imeandikwa kwa Kiswahili huku maneno mengine yakiwa yameungana. Hivi kweli wanakaa chini na kupitia walichoandika au wanakurupuka tu!
 
Naona maneno ya Lema yamewagonga kwenye kidonda na kujikuta wanakurupuka kujibu bila kujipanga. Kama wangeona ni ya kipuuzi kwanini wasinyamaze. Hawaoni kwamba kwa kutoa hii press release ndiyo wameamsha mjadala wa kwanini hili na si mengine mengi ambayo yameshatokea nchini yakimhusisha rais na Ikulu?
 
Back
Top Bottom