Lema: Ikulu imenivua ubunge ; Ikulu yamjibu vikali

IKULU YAMJIBU
MBUNGE WA
ARUSHA MJINI
ALIYEENGULIWA
GODBLESS LEMA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Katika mahojiano yake
leo, Alhamisi, Aprili 5,
2012, na Redio One,
ikiwa ni kauli yake ya
kwanza baada ya
Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza
kumvua ubunge,
aliyekuwa Mbunge wa
Arusha Mjini, Bwana
Godbless Lema, amedai
kwa jazba sana kuwa hukumu ya Mheshimiwa
Jaji Gabriel Rwakibalira
imetokana na
maelekezo ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete na Ikulu. Kauli hii ya Bwana Lema
ni upuuzi. Siyo
Mheshimiwa Rais
Kikwete wala Ikulu
imeingilia kati kesi yake
kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu
ama kuzungumza na
Mheshimiwa Jaji
Rwakibalira.Kwa hakika,
haijapata kutokea
Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia
madarakani, Desemba
21, 2005, akaingilia, kwa
namna yoyote ile,
mwenendo wa kesi
yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya
ngazi yoyote katika
Tanzania. Na wala
hakusudii kufanya hivyo
wakati wote wa muda
wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa
hukumu ama kuelekeza
namna ya kutoa
hukumu katika kesi
zilizoko Mahakamani.
Rais hana madaraka wala mamlaka
hayo.Aidha, kauli ya
Bwana Lema ni ukosefu
mkubwa wa adabu na
heshima kwa Mahakama
ambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali
ama na Muhimili
mwingine katika
maamuzi yake. Bwana
Lema amekuwa
kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazima
atambue jambo hili
kubwa na muhimu
katika mfumo mzima
wa utawala wa nchi
yetu.Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na
kwa kweli ni bahati
mbaya, kwamba Bwana
Lema anajaribu kuingiza
mambo yasiyohusika
katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni la
kisheria ambalo msingi
ni hoja na maelezo
mahakamani.Bwana
Lema asitafute visingizio
kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu
mwingine wa kumbebea
msalaba huu. Badala ya
kutafuta mchawi
asiyekuwepo, ni vyema
Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni
sababu zipi za kisheria
zilizomfanya ashindwe
na kama ameridhika
kuwa hakutendewa haki
akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Tunaomba wananchi
wampuuze.
Ameshindwa kesi kwa
makosa yake aliyofanya
hana mtu wa kumlaumu bali ajilaumu
mwenyewe.
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imekanusha kauli ya Mh. Lema kuwa inahusika maamuzi ya kumvua Ubunge. Imemshauri akate rufaa Kama ajaridhika na hukumu. Source clouds fm

Kwa vyovyote vile asingeweza kukubali. ninaamini kwa 99.99% kahusika.
 
Hizo ndo mahakama za tanzania mtu alie pigiwa kura huvuliwa madaraka yake kwa kura yakutokuwa na imani nae kama mahakama ilimpigia kura lema basi wanahaki yakumvua mwalimu jk nyerere alisema kuwa viongozi wa nchi wasipoheshimu utawala wa sheria wakawa wanatoa maamuzi kwa matakwa yao na sio kwa kuzingatia mwongozo ambao ni sheria itafika wakati ambao mwananchi atapoteza imani na serikali yake kwakuwa hajui kesho wakuu wa nchi wataropoka nini baada ya kushauriwa na wake zao au vimada vyao mwogopeni mungu wananchi tunateseka
 
Between those line lies the unspoken truth, ikulu in more than oneway ilihusika. Nashangazwa kila mara na "taarifa" za "kurugenziya ikulu"......kimekuwa ni kitengo cha propaganda na upotoshaji!

CHADEMA wajipange na kujiandaa kwa uchaguzi. Ni mechi nyingine dhidi ya timu yarefa katika uwanja na kwa sheria zao

Litatutokea puani kivipi? Hiyo ni nidhamu ya uoga na dalili ya kutojiamini. Tujenge hoja za msingi na siyo kutishana. Kama una nidhamu ya uoga nenda huko huko thithiem na si Jf.
Jamani vijana tuwe na subira hili la kumvua Lema ubunge litawatokea puani
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imekanusha kauli ya Mh. Lema kuwa inahusika maamuzi ya kumvua Ubunge. Imemshauri akate rufaa Kama ajaridhika na hukumu. Source clouds fm

Hivi clous FM ndo sehemu ya kusemea waarifu au kuna waandishi vibonde wasiojua kuuliza au waliolishwa utamu wa CCM?! I hate this tv an radio.
 
Ni jambo la ajabu sana kukanusha haraka namna hiyo ni kama walijiandaa kujibu lolote litakalotokea baada ya hukumu
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.

Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.

Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumuama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.

Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.

Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.

Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012

Wewe unayeitwa kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu tambua kuwa Lema hakujiweka mbunge yeye mwenyewe!! sawa ! tumemchagua kwa zaidi ya kura 56,000.
Ikulu inahusika usibishe bwana hii ipo wazi na mfano mdogo uliopo ni huu:
Haiwezakani mtu aliyekataliwa na wananchi kuwa mbunge wao katika jimbo la arusha ateuliwe na huyo aliyekutuma kuandika taarifa hii kuwa balozi eti wetu nchi kenya!

Hii ni bangi na inavutiwa ikulu hii!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa YJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.

Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.

Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumuama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.

Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.

Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.

Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012
Kurugenzi imejaa upuuzi mtupu press released gani Hii ! Heri Paschal Mayalla upuuzi wake ungeweza leta mantic

Rt rev Masa
 
Naomba nibishe hodi hapa jamvini kwa ugeni wangu, japo nimekuwa msomaji wa muda mrefu sasa. Langu katika hili la Ikulu kutoa tamko mapema kiasi hicho, kinaleta utata hata kwa aliye na uweza mdogo sana kutafakari!

QUOTE=LATTICE BOND;3635161]Baada ya mahakama kutoa hukumu, Lema ametoa maoni akishutumu ikulu kushinikiza Mrema avuliwe Ubunge. Masaa machache sana baadaye ikulu ikatoa tamko/taarifa kwa vyombo vya habari.
Kuna matukio mengi sana yaliyoliweka taifa katika hali tete na hayakuwa kujibiwa ndani ya muda mfupi kiasi hicho!! mfano wa matukio ya aina hiyo ni:-
1. Ushiriki wa JK kwenye kashfa ya richmond
2. Ushiriki wa JK kwenye kifungo cha Babu Seya
3. Usiriki wa JK kwenye Wizi wa Twiga kwenda Uarabuni
4.
5.
.
.
.
Orodha ni ndefu!! na hoja zote hizo ama hazijawahi kujibiwa na Ikulu katika muda mfupi kiasi hicho au kutolewa ufafanuzi.
Kutokana na mizani hiyo,
Je, Tuamini kuwa Lema kasema kweli au hoja ya Lema ni hatari kwa usalama wa nchi hii?
TOA MAONI YAKO![/QUOTE]

n
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.

Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala
Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.

Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa
hukumuama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.

Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa
Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.

Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba
BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.

Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012

kweli wamekurupuka.

hizo red zote zinaashiria kuna kila aina ya ukurupukaji kujaribu kukanusha tuhuma za kweli.

hapo kwenye bluu nadhani aliyeandaa waraka huu HANA AKILI kwa herufi kubwa.
 
Mara baada ya kuwa mbunge Mh Lema amekumbana na misukosuko ya hali ya juu kiasi kila binadamu mwenye utu alikuwa anamuonea huruma! Lema amepigwa sana na askari, amewekwa ndani,mara zote amekuwa anawindwa ili auwawe na sasa kavuliwa ubunge!

Ikiwa kama kifungu alichohukumiwa nacho ni cha 114 tafsiri yake anazuiwa kujihusisha na mambo ya siasa kwa kipindi kisichopungua miaka 5.

Sababu ya yote haya ni yeye kudai haki ya wananchi wake! Alisimama kidete kuupinga utaratibu uliotumika kumpata meya wa jiji la arusha sababu iliyopelekea maauaji ya raia watatu hivyo kupelea kuchukiwa na rais, waziri mkuu na spika wa bunge (yeye mwenyewe amedai hivyo) Inasikitisha sana!

Inapotokea binadamu wa kawaida ukafanyiwa hivi!! unafanya nini sasa???

Makundi hatari ya kigaidi kama Alqaeda, Alshabab na hamas yalianza kwa mtindo kama huu aliofanyiwa Lema! mwenyewe nimeshuhudia watu kadhaa wakitoa machozi pale walipopata taarifa kuwa Mh Lema kavuliwa ubunge!! sijui wanachofikiria kwa sasa masikini.

Kaza moyo Bro. Lema kwani Umeshinda!! Yesu wa nazareti alifanyiwa madhila zaidi ya hayo! lakini leo duniani kote ni Kwa jina lake!

God bless our lovely mp: Lema

Viva Lema, Viva Cdm Aluta continua!
 
Serekali ya inaongozwa na vilaza kwanzia jk raymamu nape nawenzi magamba ayana aibu
 
wakuu ikulu imetoa taarifa kwa uma haipo kwenye hukumu ya lema kama baadhi ya watu wanavyodai ni shinikizo la kikwete'wamemalizia kwa kusema Lema hana adabu'nimeshindwa kuelewa maana ya hiyo taarifa

Hana adabu kwa Rais wala Ikulu, kuwahusisha na maamuzi ya mahakama, Ni kipi hujakielewa hapo?

Tena inafaa afunguliwe kesi mpya na akishindwa kuonesha jinsi Kikwete alivyoingilia hukumu ya mahakama aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Hata kama Ikulu ingetaka kujibu tuhuma za Lema, haina watu wenye uwezo wa kuandika vizuri kulingana na hadhi ya ofisi ya Rais? Hiyo habari kama vile imeandikwa mtaani. Hivi hakuna wahakiki wa habari za ofisi zetu nyeti?

Rais ****** unategemea nini?
 
Back
Top Bottom