Lema aushukia Mwenge

KML

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
861
133
Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika kata za Chienjele na Likunja katika Wilaya ya Ruangwa, Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ni aibu kwa Serikali kukimbiza Mwenge kwa gharama ya Sh bilioni moja na kwenda kufungua zahanati ya kijiji isiyozidi Sh10 milioni.

Alisema ni muafaka kwa Serikali kujitathmini kama suala hilo la kukimbiza Mwenge linahitajika wakati huu ambao nchi inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei huku wananchi wakiendelea kukosa huduma za msingi.

Alisema kama wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara wangekuwa na nia ya kuwatumikia wananchi ipasavyo, wangekataa nafasi za uwaziri walizopewa kwa kuwa haziwasaidii chochote wananchi wao zaidi ya kuwafunga midomo wabunge waliotumwa kuwasemea katika shida mbalimbali za majimbo yao.

Source: Mwananchi
 
Waeleza jembe Lema,mwenge unaeneza njaa sitakagi kuona hata picha yake.
 
Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika kata za Chienjele na Likunja katika Wilaya ya Ruangwa, Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ni aibu kwa Serikali kukimbiza Mwenge kwa gharama ya Sh bilioni moja na kwenda kufungua zahanati ya kijiji isiyozidi Sh10 milioni...
Hivi wakimbiza mwenge wanapatikanaje?
 
Mh. Lema, haya maneno yako yananiumiza moyo wangu sana na ukizingatia nalipa kodi ya PAYE hata kabla ya mshahara wangu kunifikia na hivi ndivyo zinavyotumika yaani kutumia mabilioni kufungua vitu vidogo vidogo kama hivi. Mungu tusaidie. God bless Godbless Lema. Amen.
 
mbaya zaidi kwa kule vijijini wanawatoza elfu tano eti ya mchango wa mafuta ya mwenge jamani watu walivo na shida kule bado mnawatoza na ela this is not fair kwakweli...yani kuna watu ata motoni wakipelekwa bado wanapendelewa sijui ata wawekwe wapi
 
Kwanza huu mwenge unatuangazia nini, sisi kitambo tumeshaiona nuru iliyotufunua tukawamulika maaudi wa maendeleo ya nchi.
Watoto walale na njaa, baba anajenga kitambi bar.
May God Bless Godbless Lema.
 
mbaya zaidi kwa kule vijijini wanawatoza elfu tano eti ya mchango wa mafuta ya mwenge jamani watu walivo na shida kule bado mnawatoza na ela this is not fair kwakweli...yani kuna watu ata motoni wakipelekwa bado wanapendelewa sijui ata wawekwe wapi

Tena iyo elfu tano mzazi akishindwa kulipa mtoto anatolewa darasani mpaka pesa ipatikane.
Tunajenga tuna bomoa??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huku Lindi watu wana mwamko mkubwa sana na mwenge wa uhuru. Jana tuliipokea vyema hapa stand. Leo ndio tunausindikiza. Huu mwenge unajenga sana umoja wetu kitaifa.
 
mbio za mwenge ni wizi wa wazi wazi. Hautusaidii kitu, kuna mtu aliwahi kusema akiwa rais kitu cha kwanza ni kuuweka mwenge kwenye jumba la makumbusho. Si hoja ya Lema ni ya kweli, kuuendekeza mwenge ni kuwazidishia watanzania matatizo
 
Huu mwenge unajenga sana umoja wa matumbo yetu kitaifa.
 
Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika kata za Chienjele na Likunja katika Wilaya ya Ruangwa, Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ni aibu kwa Serikali kukimbiza Mwenge kwa gharama ya Sh bilioni moja na kwenda kufungua zahanati ya kijiji isiyozidi Sh10 milioni.
Alisema ni muafaka kwa Serikali kujitathmini kama suala hilo la kukimbiza Mwenge linahitajika wakati huu ambao nchi inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei huku wananchi wakiendelea kukosa huduma za msingi.
Alisema kama wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara wangekuwa na nia ya kuwatumikia wananchi ipasavyo, wangekataa nafasi za uwaziri walizopewa kwa kuwa haziwasaidii chochote wananchi wao zaidi ya kuwafunga midomo wabunge waliotumwa kuwasemea katika shida mbalimbali za majimbo yao.

Source: mwananchi

Lema tangia avuliwe ubunge akili yake haiko sawa, mara waraka wa ikulu na ikulu walivyo makini wala hawakumjibu chochote kwani walimjua ni hamnazo. Leo amekuja na mwenge. Mwenge kwa mwaka huu unategemea kufungua miradi ya nchi nzima yenye thamani ya Tshs 93 bilioni. Sasa ww Lema ukitumia Tshs 1 bn , kuleta miradi ya Tshs 93 bn shida iko wapi ?
 
Hongera Lema kwa kuliona hilo.Cha Muhimu na mshauri Lema na CDM wakomboe nchi washike dola hayo mambo yote watayarekebisha.
 
mbio za mwenge ni wizi wa wazi wazi. Hautusaidii kitu, kuna mtu aliwahi kusema akiwa rais kitu cha kwanza ni kuuweka mwenge kwenye jumba la makumbusho. Si hoja ya Lema ni ya kweli, kuuendekeza mwenge ni kuwazidishia watanzania matatizo

Sasa HATOKUWA !
 
Lema tangia avuliwe ubunge akili yake haiko sawa, mara waraka wa ikulu na ikulu walivyo makini wala hawakumjibu chochote kwani walimjua ni hamnazo. Leo amekuja na mwenge. Mwenge kwa mwaka huu unategemea kufungua miradi ya nchi nzima yenye thamani ya Tshs 93 bilioni. Sasa ww Lema ukitumia Tshs 1 bn , kuleta miradi ya Tshs 93 bn shida iko wapi ?

Hapo kwenye red ,umtakeradhi Lema please sio kauli nzuri
 
Lema ana hasira za kubwagwa ubunge kwa lugha yake chafu. Ajifunze na asiendelee na lugha zake za utata yakaja mkuta mengine.
 
Huku Lindi watu wana mwamko mkubwa sana na mwenge wa uhuru. Jana tuliipokea vyema hapa stand. Leo ndio tunausindikiza. Huu mwenge unajenga sana umoja wetu kitaifa.

unapokeshea ngono hufanyika kuliko kawaida hivyo unaeneza ukimwi. Mwaka 2006 kijiji cha Kisorya Bunda uliacha kondomu zilizotumika nyingi mpaka shuleni watoto wakaokota siku nzima! So pathetic
 
Lema tangia avuliwe ubunge akili yake haiko sawa, mara waraka wa ikulu na ikulu walivyo makini wala hawakumjibu chochote kwani walimjua ni hamnazo. Leo amekuja na mwenge. Mwenge kwa mwaka huu unategemea kufungua miradi ya nchi nzima yenye thamani ya Tshs 93 bilioni. Sasa ww Lema ukitumia Tshs 1 bn , kuleta miradi ya Tshs 93 bn shida iko wapi ?

Hivi mkuu, bila huo mwenge miradi haiwezi kuzinduliwa?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom