Lema apigwa stop kukampeni Meru

KUNDI LA WAZEE WA MERU WAMEMTAKA BW GODBLESS LEMA KUTOSHIRIKI KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUZIBA NAFASI IIYOACHWA WAZI NA MAREHEMU J SUMARI ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO HILO KWA TIKETI YA CCM.

SABABU WANASEMA ALITOA MATAMSHI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU KWAMBA "SASA SUMARI AMEKUFA HILI JIMBO LAZIMA LICHUKULIWE NA CHADEMA" KWA HIYO AMEWAVUNJIA HESHIMA'

HABARI ZAIDI SOMA HAPA:DailyNews Online Edition - Meru elders ban MP Lema

Hebu usinichafue roho, au ndo magamba wanakitafuta mahakamani ili wawazuie wakuu wasishiriki kampeni arumeru mashariki?
 
KUNDI LA WAZEE WA MERU WAMEMTAKA BW GODBLESS LEMA KUTOSHIRIKI KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUZIBA NAFASI IIYOACHWA WAZI NA MAREHEMU J SUMARI ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO HILO KWA TIKETI YA CCM.

SABABU WANASEMA ALITOA MATAMSHI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU KWAMBA "SASA SUMARI AMEKUFA HILI JIMBO LAZIMA LICHUKULIWE NA CHADEMA" KWA HIYO AMEWAVUNJIA HESHIMA'

HABARI ZAIDI SOMA HAPA:DailyNews Online Edition - Meru elders ban MP Lema

Hawa wazee, view zao za chama kilichotuletea uhuru simeshapitwa na wakati. Ni bora wanyamaze wa waache kizazi kipya wafanya kazi zao. Uhuru Lema anaupigania ni kwa ajili ya watoto wao na wajukuu zao. nashangaa kwa nini wanapenda maisha ya uprimitive kama mazinjatropazi.
 
Gazeti ni la kususia kulinunua wanunue CCM wenyewe kwani linaandika vitu vya ovyo kuliko hata Uhuru na Mzalendo.

kwa hiyo baada ya wazee wa meru kuandika barua ya kumpiga stop Lema mlitaka isiandikwe au?
sasa wengine tungejuaje? na hata kama kuna hujuma mnazodai, zitajulikanaje zisipoandikwa?
naanza kupata wasi wasi na thinking capacity ya baadhi ya watu humu!
 
CDM wana strategies nyingi and efficient kulichukua jimbo la Arumeru, si vizuri kuziweka jamvini despite the fact that they have always been transparent. For sure, EL and his In-law will consume a lot and finally becomes the best loosers
 
Mi nilijua amepigwa stop kwa amri ya mahakama kumbe ni CCM, hii ni sawa na kwenda uwanja wa vita huku ukiwaambia adui kuwa marufuku kuja na silaha kali, ebo! sasa wewe kama unaogopa silaha kali unataka vita ya nini?, si uingie mitini tu uache adui achukue nchi.

Hii inanikumbusha enzi za 'cha ndimu' mtu akija amevaa daluga tunamwambie avue la sivyo hatuchezi nae mpira.

Ha ha ha haaaaaa!
 
Hicho ni kiwewe huwezi kuichagulia wachezaji timu pinzani eti usimpange Lunyamila kichekesho cha mwaka.

CCM wameonyesha weakness ya hali ya juu katika medani za siasa.
 
masaburi kazini,daily news siku hizi full udaku,halikuwa na sifa ya marehemu kwamba ni mzuri baada ya kuondoka,lilikuwa zuri,leo hata panya hatengenezei kiota chake anapozalia,linanuka,linanuka,limeoza.
 
Ni kifungu gani kwenye katiba kinachowapa hawa wazee wa Arumeru mamlaka ya kutoa hukumu kwa mtuhumiwa? Hata kama Lema amewaudhi kwa nini wasifuate mkondo wa sheria?. Leo hii watanza wazee wa Arumeru, kesho nani? Mwishoni tutajikuta tuna tatizo kama jirani zetu Kenya.

Lakini haya ndio madhara ya siasa za mtandao 2005. Wanamtandao walitumia mbinu chafu sana, wakaegemea makabila, dini kupata kura. Dr Salim Ahmed Salim alikuwa ni victim number 1 pale walipomuita mwarab. Dhambi hiyo hiyo ya ubaguzi sasa inapandikizwa Arumeru. Nilidhani wazee ni watu muhimu kwenye jamii lakini hawa wazee wa Arumeru wanaonekana kuwa hatari kwa uhai wa taifa hili. Wanataka tusambaratike kwa sababu ya ulevi wa madaraka? Wazee wa hovyo kabisa hawa.

Hii tabia inatakiwa ikemewe kwa nguvu zote kabisa na CHADEMA kama wataona inafaa wawasilishe malalamiko rasmi kwa vyombo husika ili kuondoa hii cancer kwenye jamii ya watanzania kabla haijasambaa.
 
Kama Lema alitoa matamshi hayo, mbona alitoa ukweli mtupu! Hakuna sababu ya msingi hapo na hizi ni kampeni za CCM kupitia vyombo vya serikali
 
Mnalumbana na kauli za wazee!! Hao wazee ndo wapiga kura peke yao? Kwanza utakuta ni mtu mmoja tu aliendika hiyo barua, ila kwa mgongo wa wazee. Sio kila thread ni ya kujibu wakuu, nyingine ni uchokozi tu!
 
CDM wana strategies nyingi and efficient kulichukua jimbo la Arumeru, si vizuri kuziweka jamvini despite the fact that they have always been transparent. For sure, EL and his In-law will consume a lot and finally becomes the best loosers
Hongera sana kamanda kwa kuligundua hili tumekuwa wawazi mno hasa kupitia JF...mwisho wasiku tunaaniaka Silaha zetu....
 
Mi nilijua amepigwa stop kwa amri ya mahakama kumbe ni CCM, hii ni sawa na kwenda uwanja wa vita huku ukiwaambia adui kuwa marufuku kuja na silaha kali, ebo! sasa wewe kama unaogopa silaha kali unataka vita ya nini?, si uingie mitini tu uache adui achukue nchi.

Hii inanikumbusha enzi za 'cha ndimu' mtu akija amevaa daluga tunamwambie avue la sivyo hatuchezi nae mpira.

Umenikumbusha mbali sana
 
Kwani meru ni state inayoongozwa na hao wazee?Lema anaongozwa na sheria si wazee waliotumwa na ccm!

Hao ni wazee gani? msisahau wale wazee wa Dar ambao JK huwatumia kutolea matamko, kama ni design hiyo ya wazee kamma wa Dar, basi Meru hakuna wazee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom