Lema apigwa stop kukampeni Meru

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
KUNDI LA WAZEE WA MERU WAMEMTAKA BW GODBLESS LEMA KUTOSHIRIKI KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUZIBA NAFASI IIYOACHWA WAZI NA MAREHEMU J SUMARI ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO HILO KWA TIKETI YA CCM.

SABABU WANASEMA ALITOA MATAMSHI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU KWAMBA "SASA SUMARI AMEKUFA HILI JIMBO LAZIMA LICHUKULIWE NA CHADEMA" KWA HIYO AMEWAVUNJIA HESHIMA'

HABARI ZAIDI SOMA HAPA:DailyNews Online Edition - Meru elders ban MP Lema
 
Na hakika litaenda kwa Chadema!hao wazee waendelee na kunywa kahawa,ndo wanaotuharibia siku zote.
 
Mi nilijua amepigwa stop kwa amri ya mahakama kumbe ni CCM, hii ni sawa na kwenda uwanja wa vita huku ukiwaambia adui kuwa marufuku kuja na silaha kali, ebo! sasa wewe kama unaogopa silaha kali unataka vita ya nini?, si uingie mitini tu uache adui achukue nchi.

Hii inanikumbusha enzi za 'cha ndimu' mtu akija amevaa daluga tunamwambie avue la sivyo hatuchezi nae mpira.
 
Wamempiga marufuku wao kama nani?wanaleta sheria za majumbani kwao kwenye siasa,mamlaka yao yanaishia CCM na majumbani kwao tu.
 
Daily news la Ally Mkubwa ha ha Dr Slaa will never be a fifth president,nchi imeanguka,Serikali imezidi kuwa rojorojo hana aibu mpaka leo anashabikia chama ipo siku bwana Ally mkubwa utayaona
 
Ma.ga.mba at work again,baada ya Lema kuwa kivutio pale msibani kiasi cha kila mtu hasa vijana kutaka kushikana mkono na Lema mpaka Katibu wa CCM wilaya ya Arumeru kuanza kuwazuia na kutaka kusabisha tafrani CCM walitishika sana...sasa wameona wawatumie hao wazee ili tu Lema asishiriki kampeni kwa kuhofia mvuto alio nao...

kwanini hao wazee wasinge mwita katika kikao chao waka mweleza alivyowakwaza(kama ni kweli) na kumpa nafasi ya kujitetea...ninavyoamini sifa na kazi za wazee ni pamoja na kushauri,kuonya na kusamehe...sasa napata shaka na aina hii ya wazee wakukaa kikao na kutoa adhabu moja kwa moja...kidogo ninge amini kama ingelisikika kuwa...Wazee wamemtaka Lema awaombe radhi..akakaidi..then wafanye uamuzi kama huu.

Kikatiba pia hawa wazee hawana mamlaka kama hayo na ikizingatiwa pia marehemu Sumari hakuwa mbunge wa wazee pekee,alikuwa mbunge wa makundi yote(vijana,wazee,wasomi,wasio wsomi nk),na ndivyo atakavyokuwa mbunge atakayechaguliwa tena hapo 1 April...sasa sijui hawa wazee wanapata wapi mamlaka ya kuwasemea wana Arumeru wote.

Lema tia timu Arumeru muda ukifika ni haki yako kikatiba kamanda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom