Lema akwepwa; Atakiwa kuleta ushahidi kwa maandishi siyo kuhutubia!

WADAU HIVI SISI WANANCHI TUTAIPATAJE HIYO REPORT NA SIE TUJISOMEE AU BUNGE LAWEZA LISIRUHUSU SIE WENGINE TUSIITIES MACHONI ETI JAMANI WALE WENYE UELEW NA HILI TUHABARISHENI..........:clap2::clap2::clap2:
 
ni uamuzi wa busara maana hakawii kuporomosha matusi yule mchaga! bunge lina hadhi yake bwana sasa hayo matusi yake ni bora ayaandike halafu ayasome aone yana sound vipi! TV zinaangaliwa na watoto siku hizi ala!

Hulazimishwi kutoa pumba pls kama huna la kuchangia ni vema ukajipitia zako ukaacha watu waendelee na discussion zao
 
Topic kama hizi zingenoka sana kama angeliwapo MALARIA SUGU ah uko wapi kaka njoo utetee jahazi wanalizamisha hawa.

Kama malaria imeshindikana unategemea kuna mtu hapo? acheni kuwaita wafu jamani mnataka kuleta mizimu hapa ikatusumbua buuure
 
wabunge wenu wana pupa na wamejaa ulimbukeni! na inabidi muwatahadhalishe mapema! bungeni si mahali pa matusi na dharau! waambieni uchaguzi umekwisha tunataka kusikia hoja sio matusi! shame on you CHADEMA kutupelekea wahuni bungeni

lakini vile vile sio mahali pa kukaa na kupiga meza kwa kila ambalo halina maana, kupiga vijembe, kulala na kuitikia kila kitu ndio mzee, na mwisho kuchukua posho kubwa wakati wananchi wanahangaika kupata kilo ya sukari kwa 2000/-, kutokula sawasawa na dawa hakuna mahospitalini, maji tusahau, umeme tumezoea if i keep going on i will cry........................
 
mkuu ... nashukuru kwa mchango ulioshiba busara ...kula tano yangu instantly

mkuu ..naona maandishi ya post yako yana rangi ya red au ndio unasherehekea valentine humu JF kimtindo ... hhaa haaa
 
Wafiche wachakachue, ukweli utajulikana tu, kuwa kaka PINDA ALIDANGANYA BUNGE NA WATANZANIA
 
Anna Makinda alitangaza ndani ya bunge kumtaka Lema alete ushahidi dhidi ya Pinda hakukuwa na barua toka kwa Anna Makinda, hivyo Lema akatae kuandika barua hiyo na kuhakikisha anatoa ushahidi huo ndani ya Bunge ili Wabunge na Watanzania wote tusikie ushahidi huo. Asituletee mambo ya kuandikiana barua ndani ya Bunge hakustahili kuwepo na siri yoyote kuhusu ushahidi dhidi ya Pinda.
 
hUYO KALAGABAHO NDIO MWANACCM WA WAPI? HATA KWENYE UKWELI ANAPINDISHA MANENO?ACHA UNAFIKI UMELEWA? KINACHOTAKIWA NI LEMA AWASILISHE USHAHIDI WAKE WEWE UNASEMA CHADEMA TUMEPOELEKA WAHUNI WAHUNI WAKO WAPI? WE UNA AKILI KULIKO WATU WOTE WA ARUSHA WALIOMPA LEMA USHINDI.SHAME ON U, MWANGALIE VILE ACHA USHABIKI WA KIJINGA UNAISHI KARNE GANI WEWE?
 
unaweza kutuambia iwapo huyo mdau ana akili timamu au anavyeti vya mirembe?

Nini point yako sasa? Mtu katoa hoja we unaleta habari za vyeti vya mirembe! Kwani uongo kuwa Mh Lema kaambiwa atoe ushahidi kwa maandishi?
 
Wakuu wa JF,
Habari kutoka mjengoni zinatabaisha kuwa ccm wameshtukia dili utetezi wa Mh.Gobless Lema (Chadema) dhidi ya hoja ya spika wa bunge mh Anne Kitoto cha ndege. Spika amenukuliwa kuliambia bunge kuwa mh lema sasa atatakiwa kujitetea kimaandishi na siyo kuhutubia bungeni kama ilivyopangwa. Wadau wa karibu na hilo lichama konge barani africa ambalo siku si nyingi tutashuhudia anguko lake wanaseama ccm wamesense kuendelea kuharibika kwa public image yake ndo maana wameona walikwepeshe hilo kombora (Long range missile) kwa style hiyo.

Source; Mdau aliyeko bungeni
Hata mimi nilikuwa bado naushangaa ujasiri wa Makinda wa kumtaka Lema afafanue kauli za uongo za Waziri Mkuu Pinda Bungeni. Kwa hakika hatua hiyo ingeupaishia umaarufu kijana huyu na kummaliza kabisa Pinda kiasi kwamba asingeaminika tena machoni pa watanzania.
Mtu yeyote anayefuatilia kauli za viongozi wakuu wa nchi hii haswahaswa Kikwete na Pinda kamwe hatashindwa kufafanua kauli za uongo mpevu wa viongozi hao. Ndiyo maana nilikuwa naushangaa ujasiri wa mama huyu wa kutaka kukimaliza chama chake kinamna na kumpa umaarufu kijana shupavu huyu. Sijui nani kawashtua. Hata hivyo umma utataka kujulishwa utetezi wa Lema ulikuwaje?
Nina uhakika utetezi wa Lema hautatangazwa hadharani na wakifanya hivyo Pinda atakuwa amedhoofishwa kisiasa. Nadhani CCM wanataka kutuzalishia kijana maarufu mwingine kama walivyofanya wakati fulani kwa Zitto.
My Take: Ubabe kamwe hautaisaidia CCM kuuvuruga umaarufu wa CHADEMA bali utafanya kinyume chake yaani kuipa CHADEMA umaarufu zaidi. Dawa hapa ni viongozi kuchunga kauli zao na si kuropoka tu kama wanaongea na chekechea. Tanzania ya leo ni ya watu wenye uelewa mpana. Kuwepo Bungeni au kuwa waziri hata Rais si kwamba unawazidi watanzania wote uwezo wa kufikiri.
 
Now Whats Next...?
Lema Kuandika Barua...., Speaker Kukaa Nayo Ofisini...., Nothing Happens Till 2015
Same Old Same Old Story...
 
Wakuu wa JF,
Habari kutoka mjengoni zinatabaisha kuwa ccm wameshtukia dili utetezi wa Mh.Gobless Lema (Chadema) dhidi ya hoja ya spika wa bunge mh Anne Kitoto cha ndege. Spika amenukuliwa kuliambia bunge kuwa mh lema sasa atatakiwa kujitetea kimaandishi na siyo kuhutubia bungeni kama ilivyopangwa. Wadau wa karibu na hilo lichama konge barani africa ambalo siku si nyingi tutashuhudia anguko lake wanaseama ccm wamesense kuendelea kuharibika kwa public image yake ndo maana wameona walikwepeshe hilo kombora (Long range missile) kwa style hiyo.

Source; Mdau aliyeko bungeni

Lema ni kombora kali,wangelipuliwa!
 
ni uamuzi wa busara maana hakawii kuporomosha matusi yule mchaga! bunge lina hadhi yake bwana sasa hayo matusi yake ni bora ayaandike halafu ayasome aone yana sound vipi! TV zinaangaliwa na watoto siku hizi ala!

Una ushahidi gani kama alitaka kuporomosha matusi? na mbona umemtaja kwa kabila? wachaga walio ccm hawatukani kama kweli uchaga ni tatizo? Na hata kama akitukana si kuna taratibu zake? au siku hizi bunge linaendeshwa kwa hisia?
 
Turudi kwenye kanuni za bunge. Ikiwa mbunge anatakiwa kutoa ushahidi, anatakiwa kuuwakilisha kwa njia gani? Tafadhali wanaojuwa watujulishe na ikiwezekana pia rejea za matukio mengine kama hayo huko nyuma. Kwa mfano, mbunge gani kabla aliwahi kuwakilisha hoja zake kwa kauli zikakubalika au kukataliwa.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa waziri mkuu hakulidanganya bunge tu bali alijaribu kuihadaa dunia kuwa serikali haikuwa na makosa kwenye mauaji ya Arusha.
Kumtaka mheshimiwa Lema kutoa ushahidi wake kwa maandishi ni kutaka kuepusha aibu kubwa inayomkabili waziri mkuu.
Kama si kukurupuka kwa Anna Makinda leo hii tusingefika huku.
Ni dhahiri kuwa Lema ni lazima ataadhibiwa baada ya uchakachuaji wa kanuni na kumsitiri waziri mkuu. Inaeleweka wazi kuwa wananchi wanasikilizia kama Lema hataadhibiwa hata kama ushaidi wake hautasikilizwa itakuwa uthibitisho kuwa tulidanganywa na waziri mkuu.
Ningependa kumshauri Lema atoe nakala ya ushahidi wake kwa vyombo vya habari ili walau kuzuia uchakachuaji wa maelezo.
 
Back
Top Bottom