Lema akutana na Meya wa jiji la London nchini Uingereza

arusha 1

Senior Member
Dec 29, 2011
147
45
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini kabla ya jk kumfanyia uhuni na kuingilia uhuru wa mahakama Mh Godbless Lema, Amewasili mjini Londoni Uingereza.

Kuwasili kwa kamanda lema hapa uingereza na kukutana na Meya wa jiji hili la Londoni hapo j4 nikielelezo tosha kuwa kamanda huyo anafanya siasa za kimataifa kwasasa. Lema amewasili jana akitokea Tanzania.

Lengo lingine la safari hii ya kamanda Lema ni Uzinduzi wa M4C unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam tarehe 10/08/2012. Baada ya uzinduzi huwo Lema na Timu yake ya M4C vile vile inategemewa kwenda kwenye mataifa mbalimbali duniani kupeleka ujumbe wa M4C kwa watanzania waishio nje ya Tanzania, Lema atazindua matawi takribani saba nchini uingereza, atawasili jiji Dar es salaam siku ya alhamisi kwaajili ya uzinduzi huwo.

Vile vile Katibu wa Chadema toka Marekani anatarajia kuwasili nchini Tanzania siku ya kesho ambapo atapokewa na Mkt wa M4C Dar es salaam Bw Alex Mayunga na kamati yake pamoja na Katibu wa Chama Bw Kilewo.

Kuwasili kwa Katibu huyo toka nchi marekani ni muendelezo wa wageni mbalimbali toka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria tukio hilo kubwa na lakihistoria ukiachia lile la Arusha kipindi cha kampeni. Changia M4C kupitia Namba 111333 tulikomboe taifa letu, Lengo ni kukusanya 5 bil, inawezekana

Update: 1

Kwasasa lema anazungumza na watanzania Maeneo ya Thatched house public jijini Londoni, ni zaidi ya watanzania 70... Tutaendelea kuwajuza kinachoendelea. Safari imekuwa na mafanikio makubwa sana kwa lema kisiasa pamoja na chadema. Amepokelewa kwa heshima sana kwa ushirikiano wa waingereza pamoja na Watanzania.

Lema ananguvu sana hatukutegemea kuwa Waingereza wanamjua Lema.

Update 2:
Kwa wale Wanaopiga kelele kuhusu CV ya Lema. Hii hapa:Adv diploma HR na diploma project management , certificate management of leadership na mwanafunzi BBA
 
Haya bhana! Sasa matawi 7 uk yanasaidia nini wakati hawataruhusiwa kupiga kura? Chama kimeona kuna umuhimu wa kwenda uk wakati hapa Tz sehemu za vijijini ndio kwanza hata balozi wa nyumba 10 kutoka cdm hamna? Naipenda cdm lakini si kwa mtindo huu!
 
tarehe 10.08 kunauzinduzi wa M4C tena Dar kwani iliyofanyika hapo awali siyo uzinduzi?..all the best kamanda lema.
 
Haya bhana! Sasa matawi 7 uk yanasaidia nini wakati hawataruhusiwa kupiga kura? Chama kimeona kuna umuhimu wa kwenda uk wakati hapa Tz sehemu za vijijini ndio kwanza hata balozi wa nyumba 10 kutoka cdm hamna? Naipenda cdm lakini si kwa mtindo huu!

Ufadhili.
 
katiba ndiyo kwanza inatengenezwa na wale ni watazaiwameenda kutafuta riziki..
 
lema go go go... we are behind you .worry no body arusha tuko nawewe
 
lema ni zaidi ya mkalimani. jeshi la mtu mmoja bora ujumbe ufike lugha sio kigezo. kwani nchemba anajua kiingilishi
 
Mlio ughaibuni muweke kwenye maoni katiba mpya kuwa mpige kura online au ubalozini(kuchakachuliwa nje nje sasa labda mhesabu hapo hapo)....
 
Back
Top Bottom