'Leaning on my shoulders'. Why girls?

Si afadhali mkaka aegemewe? Manake inzi kufia kidondani si kharamu. Unasafiri na mkaka afu anajidai kalala full kukuegemea. Kumtoa baru unashindwa na wewe uonekane gentlewoman, aaaaggghhh! Kazi sana!
 
Si afadhali mkaka aegemewe? Manake inzi kufia kidondani si kharamu. Unasafiri na mkaka afu anajidai kalala full kukuegemea. Kumtoa baru unashindwa na wewe uonekane gentlewoman, aaaaggghhh! Kazi sana!
eti kumtoa baru!umenikumbusha mbali sana na huu msemo!haupo siku hizi kwa kweli!
a.k.a kutoka nduki
a.k.a kuulaza
a.k.a kutoka mita
ahahahhahahhah kweli lugha ni kiumbe hai
 
Tehe tehe tehe.....huo huo wa kawaida kwa wenzio sio wa kawaida ati!

Hawa watu sweetlady watanifanya ninunue usafiri wangu...manake maisha gani ya kusumbuana??...ila kitu nilichogundua ni kwamba watu wanatake 'advantage' ya kila opportunity inayotokea..lakini kikubwa people let's us respect other people's feelings...usinitendee vile wewe ukitendewa utachukia...
 
Last edited by a moderator:
Mara nyingi ninapofanya safari zangu za kwenda mikoani huwa natumia mabasi..japo pia mara moja moja pale ambapo kipande kimeruhusu naweza kupanda Precision Air..lakini muda mwingi ni mabasi. Kila mara ninaposafiri kwa bahati nzuri au mbaya ninapata siti ambayo inakuwa na mdada hata kama ni siti za watu watatu basi at least atakuwepo mdada..kwa hili sijui hasa kwa nini inatokea hivi!!..

Kama zaidi ya mara tatu hivi ninapokuwa safarini imenitokea wadada ninaokuwa nimekaa nao siti moja kusinzia..inawezekana ni uchovu wa safari au la..sijui kwa kweli..but kinachonishangaza wadada hawa wanapokuwa wamelala hupenda kunilalia begani (leaning on my shoulder)..Mara nyingi ninakuwa sipendi kwa sababu inaniongezea mzigo..lakini wengi wao ninapowashtua kwa nini wananilalia hushtuka na kuniomba samahani..lakini haichukui muda utaona tena mtu kanilalia na saa zingine anakoroma kabisa na mate yanamtoka..Kuna siku nilipanga nimpe mtu nakozz but nikaghairi baada ya kumuamsha mara kibao na kuombwa samahani za kutosha tu..

Wakati nilidhani haya hutokea kwenye safari ndefu..kumbe nilikuwa najidanganya..juzi nikitoka Mwenge kwenda Tegeta dada mmoja tena kwenye daladala kanifanyia the same thing..kiukweli nilibaki kushangaa kwa sababu huu ulikuwa mwendo mfupi kiasi nikashindwa kuelewa huu usingiz wa huyu mdada umetokea wapi??..nilimind na kwa sababu sikupenda kuharibiwa siku ilibidi nisimame ili yeye aendelee kuuchapa!!

Sasa wakubwa najiuliza..hivi nyie wadada mnapotulalia hivi hamjui na sisi tunahisia??..na je ikitokea miye nimekulallia utanielewa?..au wababa wenzangu na nyie yanawakuta haya au ni mimi tu??...Vinginevyo mtafanya nifikirie maamuzi magumu...lol
mkuu huwa ukienda kukata tiketi kitu cha kwanza ni kuomba bus agent akupe seat na mrembo,so hayo ni baadhi tu matunda ya maombi yako!samahan napita tu
 
Hawa watu sweetlady watanifanya ninunue usafiri wangu...manake maisha gani ya kusumbuana??...ila kitu nilichogundua ni kwamba watu wanatake 'advantage' ya kila opportunity inayotokea..lakini kikubwa people let's us respect other people's feelings...usinitendee vile wewe ukitendewa utachukia...

Mie naomba wazidi kukulalia ili upate hasira za kununua usafiri wako lol

Unachokisema ni kweli SnowBall ......kila mtu lazima amfanyie mwenzie kile ambacho hata yeye angependa kufanyiwa.
 
Last edited by a moderator:
SnowBall pacha wa mlongo wango snowhite, acha kwenda gym, labda mabega yanavutia kulaliwa, lol!
ila kwa kweli sipendi mtu anilalie safarini. hao dawa yao akianza kusinzia kama umekaa siti ya dirishani unampisha then unamwambia alalie dirisha
 
Last edited by a moderator:
Hawa watu sweetlady watanifanya ninunue usafiri wangu...manake maisha gani ya kusumbuana??...ila kitu nilichogundua ni kwamba watu wanatake 'advantage' ya kila opportunity inayotokea..lakini kikubwa people let's us respect other people's feelings...usinitendee vile wewe ukitendewa utachukia...
yaah haipendezi kusema ukweli !
 
mkuu huwa ukienda kukata tiketi kitu cha kwanza ni kuomba bus agent akupe seat na mrembo,so hayo ni baadhi tu matunda ya maombi yako!samahan napita tu

Mkuu sijawahi kuomba kwa makonda aisee cuz mimi mpango wangu ni kusafiri..ntakaa na nani hiyo ni ya wenye mabasi..
It just happens coincidentally...
 
SnowBall pacha wa mlongo wango snowhite, acha kwenda gym, labda mabega yanavutia kulaliwa, lol!
ila kwa kweli sipendi mtu anilalie safarini. hao dawa yao akianza kusinzia kama umekaa siti ya dirishani unampisha then unamwambia alalie dirisha
hahahahhahhahhha pacha wangu mwacheni jamani!sa kwani kama wifi yangu ndo anapenda kifua cha kulean on!akhu aanze tu kumkosesha raha my wee wangu!nimekumbuka wimbo wa michael bolton 'lean on me" BAK yuko wapi aniwekee jamani
 
Last edited by a moderator:
Si afadhali mkaka aegemewe? Manake inzi kufia kidondani si kharamu. Unasafiri na mkaka afu anajidai kalala full kukuegemea. Kumtoa baru unashindwa na wewe uonekane gentlewoman, aaaaggghhh! Kazi sana!

Hahahaha lol...... SnowBall hataki hayo mambo ya inzi kufia kidondani lol......mke mwenza mwenzio mie na huu ukimbao mbao wangu huwa nawatoa baru........kunilalia iwe mara moja tu.....hiyo ntajua ni bahati mbaya.....ukirudia mara ya pili walahi huna bahati manake ntakusokomeza kama umekaa upande wa dirisha waweza jigongeza asee!
 
Last edited by a moderator:
SnowBall pacha wa mlongo wango snowhite, acha kwenda gym, labda mabega yanavutia kulaliwa, lol!
ila kwa kweli sipendi mtu anilalie safarini. hao dawa yao akianza kusinzia kama umekaa siti ya dirishani unampisha then unamwambia alalie dirisha

Dada yangu [MENTION]Fixed Point[/MENTION] usiwe na wasiwasi nimeshajua namna ya kudeal na hawa viumbe...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom