'Leaning on my shoulders'. Why girls?

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,840
Mara nyingi ninapofanya safari zangu za kwenda mikoani huwa natumia mabasi..japo pia mara moja moja pale ambapo kipande kimeruhusu naweza kupanda Precision Air..lakini muda mwingi ni mabasi. Kila mara ninaposafiri kwa bahati nzuri au mbaya ninapata siti ambayo inakuwa na mdada hata kama ni siti za watu watatu basi at least atakuwepo mdada..kwa hili sijui hasa kwa nini inatokea hivi!!..

Kama zaidi ya mara tatu hivi ninapokuwa safarini imenitokea wadada ninaokuwa nimekaa nao siti moja kusinzia..inawezekana ni uchovu wa safari au la..sijui kwa kweli..but kinachonishangaza wadada hawa wanapokuwa wamelala hupenda kunilalia begani (leaning on my shoulder)..Mara nyingi ninakuwa sipendi kwa sababu inaniongezea mzigo..lakini wengi wao ninapowashtua kwa nini wananilalia hushtuka na kuniomba samahani..lakini haichukui muda utaona tena mtu kanilalia na saa zingine anakoroma kabisa na mate yanamtoka..Kuna siku nilipanga nimpe mtu nakozz but nikaghairi baada ya kumuamsha mara kibao na kuombwa samahani za kutosha tu..

Wakati nilidhani haya hutokea kwenye safari ndefu..kumbe nilikuwa najidanganya..juzi nikitoka Mwenge kwenda Tegeta dada mmoja tena kwenye daladala kanifanyia the same thing..kiukweli nilibaki kushangaa kwa sababu huu ulikuwa mwendo mfupi kiasi nikashindwa kuelewa huu usingiz wa huyu mdada umetokea wapi??..nilimind na kwa sababu sikupenda kuharibiwa siku ilibidi nisimame ili yeye aendelee kuuchapa!!

Sasa wakubwa najiuliza..hivi nyie wadada mnapotulalia hivi hamjui na sisi tunahisia??..na je ikitokea miye nimekulallia utanielewa?..au wababa wenzangu na nyie yanawakuta haya au ni mimi tu??...Vinginevyo mtafanya nifikirie maamuzi magumu...lol
 
acha kujipulizia pafyum za bei.. usioge then nenda safarini tuone kama kuna mdada atasogeza pua yake karibu na wewe

inawezekana unyunyu wa twin brother wangu mkali enh?sa ndo asijimwagie kisa wanamlalia kwenye mabasi!?mi nafikiri uhandsome wa pacha nao unachangia ahahhhahahah bega lake linaita kulalia itakua!ahahahahhahah shikamoo pacha !
 
My pacha snowhite mzima wewe?
Usingizi gani wa kulaliana bana..watu tuna stress zetu..tena na wewe utongezee za kwako!!
 
Last edited by a moderator:
My pacha snowhite mzima wewe?
Usingizi gani wa kulaliana bana..watu tuna stress zetu..tena na wewe utongezee za kwako!!

mi mzima pacha ,umenivunja mbavu na thread yako!ila kweli bana watu wanabore sana!sasa ukute mtu mwenyewe ndo anakoroma au ndo ule usingizi wa udenda!ah lazima uachie siti i see!
 
wanakulalia na wewe umeridhika tu rusha ngumi.....

Frankly hakuna kitu nachukia kama kulaliwa begani ninapokuwa safarini haijalishi jinsia , especially nisiyemjua...tena ukirudia nakukoromea kabisaaaaaaaaa

sasa wewe hujawa mkali aisee(ndo maana pacha wako kashtuka hapo)....

Au unyunyu unaopulozia mtamu kama mtakatifu ivuga alivyosema?
 
ahahahahhahhahhah BADILI TABIA unataka mu pacha azabe vibao wadada wa watu!?humtakii mema wewe!akizidiwa huwa ananyanyuka!lakini ameniacha hoi anavosema ''hivi nyie wadada mnapotulalia hivi hamjui na sisi tunahisia??.'' ahahahha hebu muulize pacha wangu huwa anapata hisia gani!mi naogopa atanichapa!.
 
Last edited by a moderator:
[MENTION]BADILIA TABIA[/MENTION] kama umenisoma vizuri nilisema ntafanya maamuzi magumu..nadhani hapo kwenye bold panahusika..naona upole wangu unaniponza ati!

wanakulalia na wewe umeridhika tu rusha ngumi.....

Frankly hakuna kitu nachukia kama kulaliwa begani ninapokuwa safarini haijalishi jinsia , especially nisiyemjua...tena ukirudia nakukoromea kabisaaaaaaaaa

sasa wewe hujawa mkali aisee(ndo maana pacha wako kashtuka hapo)....

Au unyunyu unaopulozia mtamu kama mtakatifu ivuga alivyosema?
 
mi mzima pacha ,umenivunja mbavu na thread yako!ila kweli bana watu wanabore sana!sasa ukute mtu mwenyewe ndo anakoroma au ndo ule usingizi wa udenda!ah lazima uachie siti i see!

Yaani we acha tu ndugu yangu..yaani unashangaa unalowana...kumbe mwenzio anajua kitu 'banco dodoma'
 
wanakulalia na wewe
umeridhika tu rusha ngumi.....

Frankly hakuna kitu nachukia kama kulaliwa begani ninapokuwa safarini
haijalishi jinsia , especially nisiyemjua...tena ukirudia nakukoromea
kabisaaaaaaaaa

sasa wewe hujawa mkali aisee(ndo maana pacha wako kashtuka hapo)....

Au unyunyu unaopulozia mtamu kama mtakatifu ivuga alivyosema?

Mimi hata mtu akizungusha mkono nyuma ya siti niliyokaa namtoa,itakuwa kunilalia?
 
Me huwa nachukia tabia ya wanaume kutanua miguu huwa namueleza kabisa kaka sogeza miguu yako usawa wa kitu chako,au anajitia kiwiko cha mkono kuweka kiunoni huwa nasogeza na mkono unaona mtu anajitia kuuvuta
 
Una bahati sana huyo dada hajala mayai ya kuchemsha pale chalinze na Morgoro au mahindi ya kuchemsha na keki na Juice, halafu alale ajisahau aachie ile kitu........siku njema ngoja nisaini out nifanye kazi kwanza
 
tatizo ni hako kapafyumu kako kazuri,na mvuto pia unachangia wanashindwa tu kukuambia,siku unasafiri mkoani nishtue mimi sintakulalia nitakuegemea hahahah SnowBall wenzako huzitafuta hizo bahati ati!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Me huwa nachukia tabia ya wanaume kutanua miguu huwa namueleza kabisa kaka sogeza miguu yako usawa wa kitu chako,au anajitia kiwiko cha mkono kuweka kiunoni huwa nasogeza na mkono unaona mtu anajitia kuuvuta

Kumbe tuko wengi tunaokereka safarini eeh?...sasa hiyo ya kiwiko ikoje?
 
... Ni hizi non-stop game za usiku za vijana wa kileo , huwaacha wadada hoi asubuhi! wapunguzieni wampate enough rest.
 
tatizo ni hako kapafyumu kako kazuri,na mvuto pia unachangia wanashindwa tu kukuambia,siku unasafiri mkoani nishtue mimi sintakulalia nitakuegemea hahahah SnowBall wenzako huzitafuta hizo bahati ati!!!!!!!!

Wewe Amsterdam itabidi tupasue anga..hizi safari za mikoani waaachie hawa wengine wanifanye godoro..hahahah
 
Last edited by a moderator:
Una bahati sana huyo dada hajala mayai ya kuchemsha pale chalinze na Morgoro au mahindi ya kuchemsha na keki na Juice, halafu alale ajisahau aachie ile kitu........siku njema ngoja nisaini out nifanye kazi kwanza

Ndugu yangu Elli yaani kero bin balaa..yaani ikitokea hivyo namuomba konda anihamishe aisee!
 
Last edited by a moderator:
Best SnowBall ukiona hivyo ujue unavutia ndo maana watu wanakulalia on the way to and fro kama hutapenda kufanyiwa hivo na abiria wengine kila usafiripo jaribu kukaa siti ya mmoja kwenye daladala ile ya mbele au kwenye mabasi pia ile siti ya mbele ila ndo usiwe na haraka koz ukikuta imekaliwa usubirie basi lingine lol. Pole ila mi skushauri uanzishe ugomvi tembea na pini au sindano tuu ikitokea umekaa nae siti moja mtu anakulalia unamchoma kidogo akistuka unajikausha kama sio wewe akikuuliza unamwambia hata hujui akirudia unamchoma tena hadi aache kuasinzia lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom