LEAK: Document ya hukumu ya Godbless Lema HAPA

Kwa Kwam maelezo ya mashahidi ni dhahili Batilda Buriani alitakiwa kufika mahakamani ili kuiridhisha mahakama kuwa yeye hajazaa nje ya ndoa; pia yaliyosemwa yamemzalilisha kijinsia. Mahakama kujiridhisha kuwa Lema alimkashfu Batilda pasipo ama Batilda mwenyewe kufika mahakamani kutoa ushahidi au Lowassa Au Mume wa Batilda sioni kama kuna msingi sahihi wa kufuta ushindi Especially on the following reference "There must be evidences without any reasonable doubt justifying the quoted sections!!" What I see here is a personal feeling of the Judge not ethical conduct of the same!
Kitendo cha judge kuridhika kwamba afisa mstaafu wa jeshi alikuwa mpita njia aliposikia yale maneno hakitoshi kuthibitisha kuwa aliyosema dhidi ya Lema ni kweli hasa unapozingatia public interest.
Wadai walikuwa na haki ya kufungua mashtaka lakini bado walilazimika kuonyesha angalau kiapo cha Batilda akithibitisha kuwa yaliyosemwa yamemdhalilisha/ au kumkashfu!!.
ENDAPO HII NDIYO NAKALA YA HUKUMU; BASI HAKUNA HAJA YA KWENDA MAHAKAMANI UNAPOONEWA NI BORA UCHUKUE SHERIA MKONONI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

Mkuu,
Wajibu wa kuthibitisha tuhuma ni kwa yule aliyezitoa. Wewe huwezi kumwita mtu mwizi halafu useme huyo uliyemwita mwizi eti ndio athibitishe kwamba sio mwizi, sheria haiendi hivyo.

Kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba Lema alisema hayo maneno basi alichotakiwa kufanya ni kwanza kupinga kwamba kwenye mikutano husika hakutumia hayo maneno na pili kuonyesha hayo maneno hayakuwa na madhara.

Vinginevyo kama ushahidi ulithibisha beyond resoanable doubt kwamba alitumia hayo maneno, ilikuwa sio muhimu kabisa kwa Batilda kutoa ushahidi.
 
Kweli umbumbumbu wa kutojua sheria, yaani hukumu iliyotolewa inakuwa SIRI?
Kweli JF kuna ma great thinkers
 
Hii hukumu ni dhaifu sana kwa vile haikutokana na physical evidence yoyote, bali imetegemea testimony ya mtu mmoja tu. Kesi ilikuwa inatosha kabisa kutupiliwa mbali baada ya mashahidi kushindwa kuwa consistent, jambo linaloonyesha kuwa walifundishwa.

Huyo shahidi aliyeaminiwa inawezekana yeye kwa vile alikuwa afisa wa jeshi akawa anajua kutunza kumbukumbu aliyofundishwa, lakini hakuna sababu yoyote ya kuamaini moja kwa moja kuwa analosema ni la kweli kwani yeye si malaika; yupo pale mahakani kama sehemu ya walalamikaji.

Ilikuwa ni jambo la ajabu kuwa ushahidi ulioaminiwa na mahakama wa Omari Bokolo ulikuwa ni tofauti na ule wa mlalamikaji wa kwanza halafu mahakama ikaona kuwa yeye ndiye mkweli kuliko mlalamikaji. Ni kosa kwa mahakama kufikiria nje ya ushahidi na malalamiko yaliyoko mbele yake. Baada ya mashahdi kujichanganya kuhusu tukio moja, ilikuwa ni wazi kuwa ushahidi wao kuhusu tukio hilo haukuwa na thamani tena.

Kwa maoni yangu, naona kama Jaji aliianza na presumption ya kuwa Lema ni mkosaji, na hivyo kuweka burden kwa Lema kuprove otherwise, ila kama angefuata utaratibu halisi wa kisheria wa kuanza na presumption of innocence kwa Lema na kuwaachia walalamikaji burden ya kuprove beyond reasonable doubts, basi kesi hii ilitakiwa iwe imekwisha kabla ya mashahidi wa utetezi kupanda kizimbani.
 
sio kamusi ya kawaida lazima iwe legal dictionary lugha ya sheria sio gramatical na inakuwa long setences
msiogope. Well sijaona strong evidence za kumtia Lema hatiani ushahidi una mashaka mengi haujakidhi vigezo vya kuthibitiswa pasipo kuacha mashaka.

jaji hajaangalia mazingira halisi ya madai na uhalali wa lema kuchaguliwa kihalali
jaji hajaangalia hali ya uchumi wa nchi na hasara na muda utakaotumika kurudia uchaguzi
jaji makini lazima aangalie yote hayo na sio sheria peke yake.

sijaona kama kulikuwa na ushahidi wa kurekodi kuthibisha matusi ya Lema kwa hali hii inawezekana hata mashahidi wanaweza kukaa na kutunga maneno. mahakama ilitakiwa kujiridhisha kwa ushahidi wa sauti pia sijaona hili.

mahakama ilitelezaa kwa hili. sidhani kama mahakama ilikuwa satsified kwa ushahidi uliotolewa .its politically motivated kabisa/
rufaa atashinda kwa asilimia mia moja kesi itafutwa,proceedings zote za High court zita be declared null and void.
lugha ya kimahakama ni ngumu kama sio mwanasheria lazima ushike kamusi.
 
i was the one who did post this document since this morning in the law forum, thank you for re posting the doc again..
 
Nafikiri mtakubaliana na mimi kuwa pia apande wa utetezu ulikuwa very weak. it seems Lema na wakili wake waliidharau hii kesi, selection ya mashaidi ilikuwa very weak too.

but all in all, hakukuwa na ushahidi wa kuridhisha kumtia lema hatiani (ushahidi haukuwa corrobotated kama mdau mmoja alivyoelezea hapo juu). Kwenye Appeal, Lema ajaribu kuweka wakili mzoefu especially kwenye maswala ya evidence, atachomoka tu.
 
wewe kweli mzee wa njaa! sasa wahaya wanausikaje kwenye hii hukumu. that was just one selfish judge, whose judgement has nothing to do with wahaya. there has been great haya judges eg. Hon Lugakingira has he then was, his judgements have been used in universities to instruct law students. so think twice before you start attacking hayas.
 
Back
Top Bottom