LEAK: Document ya hukumu ya Godbless Lema HAPA

OMBI: Jamani tusi-reply with a quote hii habari. Ni ndefu mno, mtawatesa wanaotumia simu.
 
Hii hukumu haikuandikwa na Rwakibarila, Imeandikwa na Dr Masumbuko Lamwai, Rwakibarila kapewa desa tu hapo na kusoma na kuandika jina lake. Hii ni 'miscarriage' kubwa sana ya justice kuwahi kutolewa na mahakama kuu.


Kama Mkapa hivi sasa kafungua mdomo na anaongelea/jitetea na madudu yake aliyoyafanya huko nyuma basi bado naamini kuna siku huyu Rwebangira atafungua mdomo wake na kuwaelezea watanzania nini kilichojiri mpaka akaweka historia hii
 
Jf ni kiboko! kila kitu ukitaka unapata humu!

Thanks Maxence,*
Thanks Mike and others for being the Jf founders

Jf: The Home Of Great Thinkers
 
kweli kizungu kinatisha, maana wachangiaji hapa siwaoni.


jamani iatafsiriwe kwa kiswahili

Wewe huchangii halafu unasema Kidhungu kinatisha. Sasa jijui unataka kusema umejiweka kwenye group ipi hapa.............. Jisemee mwenyewe siyo JF!!
 
Haya wanashetia wetu tusaidieni, mafafanuzi ya hukumu hii, lakini pia tunaomba utetezi wa Lema kutoka kwa wakili wake tulinganishe na hukumu!
 
please!!!: what does S.114(1)-(7) of The National Election Act is all about?
 
Wadau nimepitia hukumu ya huyu jaji na ninaona inamapupungufu makubwa. Hakukuwa na ushahidi wa kiwango cha kutosha kuweza kuthibitisha kama kweli yale maneno yalitamkwa na LEMA. Ushahidi umetolewa wa mtu mmoja mmoja kwa kila tukio. Kisheria ushahidi huu ni sharti uungwe mkono vilivyo na ushahidi wa mtu au watu wengine yaani uwe collaborated. Hili katika kesi hii halikufanyika there is no collobarative evidence on all the alleged events!. Suprisingly, katika siku za leo hii nilitegemea maneno yao yaungwe mkono na picha ya video etc au recorded speech lakini hili hakuna na jaji kaliachia na kudhani wamethibitisha madai yao on balance of probability

Pili Walalamikaji hawakwenda kuthibitisha ni vipi maneno yale yamewaathiri wao kama wapiga kura katika huo uchaguzi ukizingatia wengine wanakiri katika ushahidi wao hawana chama wala maslahi yeyote ni vipi sasa wameathirika? Na kama wakisema Buriani ndiyo ameathirika then wao hawan haki ya kulalamikia hilo yao cause of action. Kwani kwa tasfiri ya jaji mtu yeyote mwenye kitambulisho cha kupiga kura anahaki ya kuleta malalamiko yeyeto dhidi ya mgombea. Nadhani hii sio tafsiri sahihi lazima kuwe na mipaka ya kile mlalamikaji anachokileta na kipimo kiwe yeye kama yeye ameathirika vipi...

Kwa sasa ni haya wadau tuendelee na analysis ya judgememt!

Mkuu sio "collaborated" ni "corroborated!" (Refer your Legal/Law Dictionary if you have one). Otherwise, nakuunga mkono kuwa mkanda wa video au sauti ungetolewa kama ushahidi! Halafu sijaona mahali alipozuiwa Lema kugombea kwa miaka 5, unless kuna sehemu nimeruka!
 
Haya wanashetia wetu tusaidieni, mafafanuzi ya hukumu hii, lakini pia tunaomba utetezi wa Lema kutoka kwa wakili wake tulinganishe na hukumu!

Kitu gani kitafsiriwe Mkuu? You mean English - Swahili translation? Au tafsiri ya vifungu tu vya Sheria vilivyotajwa ukilinganisha na facts za kesi?
 
kweli sina welewa sana wa sheria lakini kwa haya sizani kama kunachochote cha kusababisha lema aachishwe ubunge. may be let us wait the man how know laws
 
Nashukuru kwa kupata hukumu hii. kama ndio nakala halisi ya mahakama, kama mwanasheria nimesoma critically facts na issues za judge alizotumia kufikia uamuzi wake. Kisha nimegundua mapungufu yafuatayo-
1. Judge anakiri Kamanda G. Lema hakutamka maneno hayo BINAFSI bali wawakilishi wake, hivyo nilitarajia judge angekuwa na additional issue ya kumtambua nani aliyetamka maneno hayo kwa niaba ya G. Lema; hakuna popote nilipoona anatajwa mtu huyo;

2.Jambo la pili ambalo judge hakulitatua ni kuhusu huyo mtu aliyetamka maneno ya kashfa dhidi ya mgombea wa CCM je alitamka maneno haya kwa kibali na ruhusa ya Kamanda G. Lema,je Lema alijua hayo yamesemwa na akayakubali kwamba hata ingekuwa yeye angefanya hivyo, maswali haya naona bado hayajajibiwa katika hukumu hiyo ya jaji, ndio maana alifikia uamuzi huo

3. Suala jingine ambalo jaji alitakiwa kulitolea tafsiri endapo kosa la jinai alilotenda A anaweza kuhukukumiwa B bila ya kushirikiki katika kosa hilo kufanyika,

4. Maneno mengi yaliyosemwa naona ni alleged defamation ambayo ina taratibu zake na fidia hutolewa pale inapodhibitika, itafaa CDM kuanza mchakato wa kuomba amendments ya kifungu hiki kwani kimejumuisha masuala mengine ambayo yanasimamiwa na sheria zingine na yana utaratibu wake wa fidia. hii itakuwa iliwekwa kwa makusudi na tayari huenda watu wa kutamka ovyo waliandaliwa bila upinzani kujua ili kupata sababu ya kutengua wabunge wa upinzani

Kwa mtizamo wangu haya masuala matatu yakitizamwa kwa upana wake kamanda G. Lema atarejea Bungeni hivi karibuni

CDM waongeze bidii ili kamanda arejee mjengoni kabla ya mjadala wa KATIBA MPYA

mm napita

Ili uweze kumshinda adui yako unapaswa kufahamu uwezo/fikra/mawazo na mbinu zake
 
Umejuaje? Lakini c kidhungu tatizo si wote tumesoma sheria, wengine ni ma Dr, Acc. Au etc
Wakati mwingine tuacheni utumwa wa fikra, ni kweli hicho kizungui kigumu, je kutojua kizungu ni tatizo? au ndiyo kuendelea kutawaliwa na wakoloni hadi kwenye bongo zetu, ningetamani mngesema kaaa, wakati mwingine hizi hukumu ziwe za kiswahili, hivyo hiyo Lugha pale mahakamani inatekelezwa Uingereza? tuacheni ushamba
 
Naomba kuuliza kwa wale weledi wa mambo ya sheria.

Hii hukumu imeletwa na mleta mada kama doc ambayo imevuja, je kweli imevuja au mtuhumiwa ana haki ya kupewa nakala ya hukumu ? na kama ana haki na amepewa na mahakama sasa imevujia wapi?
 
Kwa Kwam maelezo ya mashahidi ni dhahili Batilda Buriani alitakiwa kufika mahakamani ili kuiridhisha mahakama kuwa yeye hajazaa nje ya ndoa; pia yaliyosemwa yamemzalilisha kijinsia. Mahakama kujiridhisha kuwa Lema alimkashfu Batilda pasipo ama Batilda mwenyewe kufika mahakamani kutoa ushahidi au Lowassa Au Mume wa Batilda sioni kama kuna msingi sahihi wa kufuta ushindi Especially on the following reference "There must be evidences without any reasonable doubt justifying the quoted sections!!" What I see here is a personal feeling of the Judge not ethical conduct of the same!
Kitendo cha judge kuridhika kwamba afisa mstaafu wa jeshi alikuwa mpita njia aliposikia yale maneno hakitoshi kuthibitisha kuwa aliyosema dhidi ya Lema ni kweli hasa unapozingatia public interest.
Wadai walikuwa na haki ya kufungua mashtaka lakini bado walilazimika kuonyesha angalau kiapo cha Batilda akithibitisha kuwa yaliyosemwa yamemdhalilisha/ au kumkashfu!!.
ENDAPO HII NDIYO NAKALA YA HUKUMU; BASI HAKUNA HAJA YA KWENDA MAHAKAMANI UNAPOONEWA NI BORA UCHUKUE SHERIA MKONONI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Kazi, hiyo sec inampa G ban, yaani asishiriki uchaguzi! Lakini sec hiyo ni kwa ajiri ya makosa yanayohusiana na rushwa!
 
Mtiririko wa hukumu toja juu umeonekana kuegemea upande....

Yote katika yote huu ushahidi wa mdomo tu bila hata CD kama ya Lusinde mbona utaumiza wengi!!!!!!
 
Back
Top Bottom