Lazima wawajibike

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Niko katika nchi za watu , nimekaa nasoma majukwaa mbali mbali ya mitandao ya afrika mashariki lakini haswa nasoma ya kitanzania ninapotoka na kuishi mimi , mengi ya kitanzania yanaongelea shutuma tu kuhusu viongozi na watu wengine wa tanzania wanavyofanya mabaya kuhusu nchi yao na wananchi wao , wanamtandao ni kulalamika tu kila siku , kila wakati wanakata tamaa lakini wengi wanafikiri kwamba mwaka 2010 ndio watatoa fundisho pengine watachagua viongozi ambao watakuja kuokoa jahazi hili , ulalamishi wote huu unatokana na jinsi wale waliopewa madaraka na wale waliochaguliwa na raisi kutokuwajibika na shuguli zao ipasavyo kama jamii zingine zinavyofanya duniani haswa kwa nchi zilizoendelea .

Hapa burundi imetangazwa habari ya kuuwawa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino , wengi wamekimbia nyumba zao na kwenda vituo vya polisi au sehemu zingine ambazo wanafikiri kwao ni salama , polisi wa hapa na vyombo vya usalama vimeanza msako kusaka watu hawa na wanaweza kulazimika kuvuka mpaka kama watakuwa na uhakika huo watu hao wamekimbilia tanzania au nchi nyingine yoyote ya jirani kuwatafuta na warudishwe burundi kuja kujibu tuhuma zinazowakabili --- hili no onyo kwa Nchi jirani yao ya tanzania ambayo inasemekana kwamba maalbino hao wanauwawa kwa ajili ya bishara za madini haswa Tanzania na Kongo chochote kinaweza kutokea siku za karibuni maeneo ya mpakani mwa nchi hizi .

Viongozi wa hapa walivyosikia habari hizi mara moja walifika maeneo ambayo maalbino hao wamejificha wanashirikiana na wananchi wa huko pamoja na watu wengine kuweza kusaidia watu hawa pamoja na kuwasaka wahalifu hawa , ni tofauti sana na tanzania ambayo suala hili sasa limeanza kusahaulika , yule mwandishi wa habari wa BBC ambaye alifuatilia suala hili na kuliweka wazi kajificha wala haongelei tena suala hili , vyombo vya usalama havitoi taarifa zozote zile kuhusu suala hili na hata viongozi wa mikoa hiyo ambayo vitendo hivi vinaendelea nao wamekaa kimya tu .

Wakati wa sikukuu siku karibu 2 zilizopita kulitokea katika ukumbi wa burudani mkoani Tabora , kipindi hicho raisi alikuwa dar es salaam , alichofanya yeye ni kutoa pole na pesa kidogo kwa ajili ya pole kwa kila familia , raisi kiongozi wa nchi akaendelea na sherehe mjini dar es salaam kawaachia watu hao wa TABORA kazi yao wazike watu wao na uchunguzi ufanyike si ameshatoa pole bwana na hela si ameshatoa bwana wananchi wa tabora nao wamekubali kwa mikono miwili pesa hizo na pole hiyo ya raisi .

Hili ni janga kubwa raisi alitakiwa aende TABORA angalau asaidie shuguli kidogo pale au sio huyu raisi aliyeenda huko huko tabora kuomba kura na kuahidi makubwa mbona leo wamepata shida hizo hataki kwenda ? si ndio huyu huyu raisi huwa anaenda kwenye misiba ya rafiki zake mikoa ya jirani na hapo ? kwanini ameshindwa kwenda TABORA wakati huu kuna nini ? lazima kutakuwa na jambo fulani .

Basi kwa mtindo huu na mitindo mingine mingi ya viongozi wetu wa kutoa pole na pesa wajue pesa zinaisha na pole huwa inapoa lakini unapoonyesha angalau sura yako kwa mfiwa unaandika historia na kuwapa moyo wale wote waliokuwa pale na utendaji wa kazi huenda kwa kasi zaidi ya matarajio ya wengi .

Kwahili kuna watu wanatakiwa wawajibike moja kwa moja bila kupoteza muda na wajiandae kufikishwa katika vyombo vya sheria
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom