Lazima tumkosoe Kikwete, Slaa na wengine

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
HIKI NDICHO KIZAZI CHETU……….

Siku zote nimekuwa nikisema kwamba, hakuna dhambi kukosoa mtu anapokuwa amefanya kosa. Mtu yeyote anaweza kukosolewa, ni mmoja tu asiyeweza kukosolewa, huyu ni Mungu muumba Mbingu na nchi.

Lakini ninajua, tena nina uhakika kwamba hata Barack Obama anakosolewa, Jakaya Kikwete anaweza kukosolewa, Wibroad Slaa, Freeman Mbowe, Ibrahim Lipumba na wengine wote wanaweza kuk...osolewa. Sababu ni rahisi sana, hawa ni binadamu, sio miungu, sio malaika, sio viumbe kutoka sayari za mars, Jupiter au jua. Wanaweza kukosea na wanapaswa kuwa tayari kukosolewa.

LAKINI: Kuna namna ya ukosoaji inakosa adabu, nadiriki kutamka hapa kwamba idadi kubwa ya WANATANURU vijana (sio wote) hawana adabu katika kueleza hisia zao, kujenga hoja zao na matokeo yake wanamkosea hata Mwenyezi Mungu.

Kwa mfano Rais Kikwete mtu, ana familia yake, ana mke na watoto, Dr. Slaa ni mtu, ana ndugu jamaa na marafiki zake, ana watu wanao mheshimu katika jamii, Mbowe, na viongozi wengine ni watu, hata kama wewe huwaheshimu wanaheshimika na wengine. Unaruhusiwa kuwakosoa lakini uwe na adabu, unaruhusiwa kuwakosoa lakini usiwatukane matusi.

Ukosoaji wako usilenge kuwadhalilisha, ulengekutafakarisha, kufikirisha na kuleta mabadiliko yanayotakikana. Vinginevyo UNAKUWA MPUUZI NA MPUMBAVU KAMA YULE UNAYEMDHANIA KUWA NI MPUUZI NA MPUMBAVU!

NAWASILISHA!See More
.
 
t2015ccm Mkuu umeshuka vizuri sana ila hapa siku hizi sio home of GT tena hapa ni bwawa la kambare ndevu family nzima'kama huamini siumemtaja malaika wao mkuu Slaa subiri uone majibu
 
Last edited by a moderator:
umenena vyema mkuu, mambo mengine ni uungwana tu wala haihitaji kufundiswa.
Unapotukana mtu unakuwa umejitukana mwenyewe coz unaonyesha ulivyo na uwezo mdg wa kujenga hoja na kuchambua mambo.
 
Marufuku kumkusoa Slaa, wengine ruksa ukimkosoa Slaa utaambiwa una bifu naye...
 
Tatizo ni malezi, kunawengine hawaheshimu wazazi wao itakua mtu baki. Cha ajabu zaidi hawa jamaa wote wanaheshimiana lakini anakuja kijana asie hata na kadi ya chama anarusha matusi yasio na mpango. Slaa,JK na Mbowe wote wanasiasa,leo na kesho wanaweza kushirikiana kuongoza hii nchi wote tukabaki kama mafala vile.
 
Watu wengi walikuwa wamebanwa na muda ukifika kwa GAS and TEMPERATURE kuwa kubwa in a constant volume, basi mtu analipuka. Haya yalianzishwa na CCM wako hao hao baada ya kuona wameanza kuzidiwa POINT na wao wakaanza kurusha matusi. Siyo kweli ni Chadema ndiyo walianza kumshambulia Kikwete au sijui nani wa Chadema.

Sasa ukiangalia Newton's Law of Motions: In Every action, there is Equal and Oposite Reaction.

Kwenye Siasa inabidi uwe na Ngozi ngumu kama ya Tembo (sikumbuki nani alisema). Kama ukishindwa kuvumilia joto la Jikoni, basi kimbia mbali sana. Umeona nani anamtukana Sallim Ahmed Sallim?
 
Ndugu t2015ccm, ulichoongea ni cha msingi sana ili viongozi wetu wajue mapungufu yao na kujirekebisha na hatimae tusonge mbele.Ila hili tatizo hata wewe unalo, hebu jaribu na wewe kujiangalia kwanza kabla ya kulaumu wengine
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada nakubariana nawe 100% kuwa lazima tuwa heshimu viongozi wetu na ni busara kuheshimiana!

Lakini usitegemee ni muheshimu mtu wa upande wako wakati wewe humuheshimu wa upande wngu! Ni vyema tukajirekebisha na tukianza na wewe mtoa mada!

Na kushuru kwa kutoa ushauri mzuri ambao na wewe una kuhusu.
 
Back
Top Bottom