Lazima tukubali "HAKUNA RAISI BORA KAMA MWINYI"

Mzee wa kurekebisha

Senior Member
Sep 29, 2012
178
169
Katika utawala wake ndipo watu wengi wa hali ya chini kama, Wamachinga
na wafanyabiashara ndogondogo waliweza kujenga na kufanya mambo mengi
ya Maendeleo, dhana ya kujiajiri ilikuwa inawezekana. Toka aondoke madarakani
kila kitu kimebadilika na nchi imekuwa chungu sana.
HUYU NDIYO RAISI BORA KULIKO WOTE WALIOWAHI KUONGOZA TANZANIA.
 
HUYU NDIYO RAISI BORA KULIKO WOTE WALIOWAHI KUONGOZA TaANZANIA.

Mashudu
 
na ndiyo rais pekee ambaye wakati anaongoza mfumuko wa bei uligonga asilimia 25, kwa karibu anafuatiwa na kikwete kwa sababu miezi michache iliyopita inflation ilifika asilimia 19.5

hawa ndio marais ambao sera zao za uchumi zilikua/zimekua mbovu kuliko marais wote tanzania
 
Acha unafiki wewe unajua kabisa mwanaheri ndo aliyeua uchumi wa nchi yetu leo unajidai umemsahau kwa kivuli cha dini jiangalie oh
na ndiyo rais pekee ambaye wakati anaongoza mfumuko wa bei uligonga asilimia 25, kwa karibu anafuatiwa na kikwete kwa sababu miezi michache iliyopita inflation ilifika asilimia 19.5

hawa ndio marais ambao sera zao za uchumi zilikua/zimekua mbovu kuliko marais wote tanzania
 
Katika utawala wake ndipo watu wengi wa hali ya chini kama, Wamachinga
na wafanyabiashara ndogondogo waliweza kujenga na kufanya mambo mengi
ya Maendeleo, dhana ya kujiajiri ilikuwa inawezekana. Toka aondoke madarakani
kila kitu kimebadilika na nchi imekuwa chungu sana.
HUYU NDIYO RAISI BORA KULIKO WOTE WALIOWAHI KUONGOZA TANZANIA.
Umeamua kuchekesha?
Hiyo conclusion yako ni simple mno na imekoSa vigezo vya muhimu. Huwezi kupima uwezo na ubora wa rais kwa kigezo cha watu kujenga nyumba ... u need to do more work broda.
 
na ndiyo rais pekee ambaye wakati anaongoza mfumuko wa bei uligonga asilimia 25, kwa karibu anafuatiwa na kikwete kwa sababu miezi michache iliyopita inflation ilifika asilimia 19.5

hawa ndio marais ambao sera zao za uchumi zilikua/zimekua mbovu kuliko marais wote tanzania

Mambwiga ndocha lala
 
Na ndio Raisi pekee baada yakumaliza muda wake wa uongozi akaambulia Makofi!
 
Katika utawala wake ndipo watu wengi wa hali ya chini kama, Wamachinga
na wafanyabiashara ndogondogo waliweza kujenga na kufanya mambo mengi
ya Maendeleo, dhana ya kujiajiri ilikuwa inawezekana. Toka aondoke madarakani
kila kitu kimebadilika na nchi imekuwa chungu sana.
HUYU NDIYO RAISI BORA KULIKO WOTE WALIOWAHI KUONGOZA TANZANIA.
Aliacha deni la taifa likiwa Dolari ngapi?
 
Talking in figures......see How we have grown economically between the ''presidents''

image2.gif
 
Katika utawala wake ndipo watu wengi wa hali ya chini kama, Wamachinga
na wafanyabiashara ndogondogo waliweza kujenga na kufanya mambo mengi
ya Maendeleo, dhana ya kujiajiri ilikuwa inawezekana. Toka aondoke madarakani
kila kitu kimebadilika na nchi imekuwa chungu sana.
HUYU NDIYO RAISI BORA KULIKO WOTE WALIOWAHI KUONGOZA TANZANIA.
schlechte offenen Geist
 
halafu tunaahidiwa maisha bora kwa kila mtu. mie bado nasubiri kuona hiyo ahadi, mbona haifiki??
 
Mwanzisha mada anaweza kuwa na hoja kama akiwaambia maneno haya watu walioyashudia maisha ya mwishoni ya Rais Julius Kambarage kwa maana katika kipindi cha huyo mtu nchi ilikuwa shaghala baghala lakini akiwaambia watoto ambao wameanza kubalehe kipindi cha Mkapa hawataweza kuelewa.

Mwinyi aliikuta nchi ikiwa haina wafanyabishara, angekusanya kodi kutoka kwa nani? alimkuta ng'ombe kakondeana akaanza kulisha majini hadi aliponona kwa muda wa miaka 10, ndipo alipokuja Mkapa na kukamua maziwa, watu hawakumbuki na wengine hawajui.

Kipindi cha Mwalimu ilikuwa ni vigumu kwa wakazi wa Iringa kuleta mahindi Dar walikuwa wakikamatwa kama wahujumu uchumi, watu walikuwa wakivikataa viroba vyao vya mahindi na viazi wakati Dar watu walikuwa wakila unga wa Yanga ambao ulikuwa mtamu kwa marahage tu, unga ambao tuliambiwa huko Marekani Regan alikuwa akiwalisha farasi wake na mwalimu akamuomba na kuja kutuletea.

Hebu muulize mtu wa Iringa na Morogoro kama anaujua unga wa Yanga aka chakula cha farasi ambacho Dar tulikuwa tukipanga foleni na kupewa kwa kaya. Narudia tena watoto waliobarehe kipindi cha Bichwa (Mkapa) hawawezi kujua mambo haya.

Kipindi cha Nyerere tulikuwa tunapiga mswaki kwa mkaa badala ya dawa ya meno, dawa ya mbu tulikuwa tukichoma vifuu, viatu tulikuwa tukikata matairi ya gari kama unavijua vile viatu vinavyotumiwa na Wamasai maarufu kama makatambuga.... aaah hata mkate tulikuwa hatuwezi kula mpaka kwa foleni. Lakini alipokuja Mwinyi mambo haya aliyakomesha na kuondoa vizuizi vya barabarani na kuwaambia Watz walioko nje kuwa wasilete tena sabuni za kunukia kwa ndugu zao bali waje kujenga nchi, mimi siongelei mada hii kwa ajili ya udini wala ukabila kama kuna mtu aliyekuwa na utambuzi wa mambo tangu miaka ya 70 & 80 anaweza kuongea chochote.

Mwalimu aliiharibu nchi hii baada ya kuamua kupigana vita na Idd Amin akatoa miezi 18 ya kufunga mkanda baada ya vita lakini hadi alipokuja mwinyi siye tulikuwa tukifunga mkanda mwenzetu kwa kuwa alikuwa Ikulu alikuwa akilegeza.
 
na ndiyo rais pekee ambaye wakati anaongoza mfumuko wa bei uligonga asilimia 25, kwa karibu anafuatiwa na kikwete kwa sababu miezi michache iliyopita inflation ilifika asilimia 19.5

hawa ndio marais ambao sera zao za uchumi zilikua/zimekua mbovu kuliko marais wote tanzania

Mshauri wake wa mambo ya uchumi alikuwa ni Prof. Ibrahim Lipumba !!
 
Back
Top Bottom