Lazima niwe mkweli mbele za Mungu, hakika Kikwete umenikuna kwa hili!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Kwa heshima na taadhima nachukua nafasi hii kukusifa Dokta wa Heshima (UDOM), Kanali, Mheshimiwa Sana Jakaya Mrisho Kikwete kwa mengi uliyoifanyia nchi hii tangu ushike hatamu ya uongozi wa juu kabisa.

Yapo mengi tena sana uliyoifanyia nchi hii kama vile kuwapa nafasi za uongozi kwenye chama unachoongoza na serikali wahujumu uchumi (mafisadi) ambao wamekivuruga na kukivua nguo chama na serikali yako. Kupitia hilo, watanzania tumejifunza kwa vitendo kwamba uongozi na biashara haviendi pamoja. Lakini kubwa kuliko yote ni FUNDISHO UTAKALOTUACHIA KUHUSU UMUHIMU WA KUPIGA KURA NA UMUHIMU WA KUTAFAKARI KWA KINA KABLA YA KUPIGA KURA.

Kupitia kwako watanzania tumejifunza kuwa kumbe umaarufu wa mgombea unaweza ukatengenezwa kirahisi tu kwa fedha za wahujumu uchumi kupitia vyombo vya habari na ukawasukuma wengi kumpigia kura. Wakati wa uchaguzi uliokuweka wewe madarakani watu waliacha kutafakari historia yako kiutendaji na kitabia na uzalendo wako kwa nchi wakaiishia kushabikia ulimbwende na ujana wako wa bandia. Sasa cha moto wanakiona.

Ama kweli wazee wetu hawakukosea walipotuasa ''baniani mbaya lakini kiatu chake dawa''

Mungu akubariki sana.
 
Double G,

Hapo umenena,! Ukweli ni kuwa uchaguzi wa urais awam ya nne pamoja na kwamba utatupa kazi kuponya makovu yake.lakini pia umetoa fundisho kuwajaribu wale wote wanaotaka kutawala....siyo kuona uso wa bashasha na kudhani huyo ndiye?...manake ilifikia hatua tukawa vipofu kwa kushabikia na kuchagua eti handsome na eti kijana?.?

Naamini ni fundisho......
 
Mkuu tumejifunza sana. Kufanya kosa siyo kosa ila kurudia kosa hapo Tutakuwa siyo tu TWATENDA kosa AU TWAFANYA ujinga, bali itakuwa "ashakumu si matusi" TU-wapu..." SAMAHANI, HASIRA JAMANI!!!!!!
 
Haha haha nafurahi kama mazuri vile! Mie nampa pole na si shukurani maana katuweka pabaya sana, hakika 2lifanya kosa na hatutorudia.
 
Hii ingeleta maana sana kama watanzania hawauzi kura kwa T-shirts na Kofia kule vijijini kuliko na Idadi kubwa ya wapiga kura.
 
mimi nimejifunza sana hapo,bora nisipige tena kura nchi hii!

Topthinker umekosea. Kupiga kura ni muhimu tena sana. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuepukana na viongozi wa aina hiyo. Usiache watu wasiotafakari na kuona mbele ndiyo wawe wapiga kura pekee. Think twice!
 
mkuu tumejifunza sana. Kufanya kosa siyo kosa ila kurudia kosa hapo tutakuwa siyo tu twatenda kosa au twafanya ujinga, bali itakuwa "ashakumu si matusi" tu-wapu..." samahani, hasira jamani!!!!!!

kama mnakumbukuka tension na uchungu wakati matokeo ya uraisi 2010 yakitangazwa!

Kama yule babu wa tume ya uchaguzi mmemsahau basi nyie subirini tu!
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia kubadili jina bila kutafakari linawqeza kukuletea balaa.
Mimi nitaililia tanganyika mpaka siku ya kufa kwangu.
 
Siku moja ukombozi wa kweli utakuja Tanzania ambapo
maslahi ya nchi yatakuwa kwanza, uadilifu utakuwa ni
sifa ya kujivunia na ufisadi utakuwa ni jambo la aibu.
 
mkuu umenena jambo la maana saana tuu. sijui watu walologwa yaani shauku ilikuwa kubwa lkn hakukuwa na concrete reason kwa nini anapendwa.
 
Ni kweli kabisa Gosbert. Ona sasa urais umegeuzwa kuwa mradi. Hatukuzoea kusikia watoto wa marais wakiwa na miradi ya ajabu ajabu lakini leo Ridhiwan inasemekana ni miongoni mwa mabilionea wa nchi hii!
 
huyu ni sawa na mwana ukome, basi nimekoma mama sitorudia tena, nisamehe.
 
Topthinker umekosea. Kupiga kura ni muhimu tena sana. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuepukana na viongozi wa aina hiyo. Usiache watu wasiotafakari na kuona mbele ndiyo wawe wapiga kura pekee. Think twice!
Tatizo la kutopiga kura ndio hasa linalotuletea matatizo, kama mtu unakereka na uongozi uliopo madarakani ni bora tuhamasishe wale wote wa namna hii wapige kura ya kukikataa hicho chama.

Huu ndio uwe mkakati wetu wa kwanza sote tunaoelewa na kuchambua masuala uongozi na siasa kwa ujumla la sivyo itabakia kuacha watu wanasusia kupiga kura kitu ambacho sio dawa hata kidogo, kampeni hii ikianza sasa na kwa nguvu hakika tutawaondoa viongozi waovu hii ni njia nzuri kuliko zote, njia iliyotumika na nchi za kiarabu huwa ina matatizo ya kiuchumi na kisiasa pia, kwani hata waovu pia watajitokeza kutaka madaraka.
 
Watanzania bado tuna kazi nzito ya kuelimishana. Kama mtu anajiita topthinker haoni umuhimu wa kupiga kura, ukombozi utapatikana kweli!!
 
Back
Top Bottom