Lawrence Masha: Kutoka Uwaziri hadi kukusanya takataka Dar

Bagram Army

Member
Apr 16, 2012
48
7
Leo nimemsikia aliepata kuwa waziri wa Mambo ya ndani Lawrence Masha akihojiwa na EATV akasema anafanya kazi ya kukusanya/kusomba taka toka ktk makazi ya watu, alikana kuwa alikuwa anafanyia kazi zake ROSE GARDEN ila alikubali kuna wakati alikuwa anashinda pale na akasema alikuwa anaenda pale na chupa yake ya chai anakaa hadi usiku mnene.
Lakini pia kuna tetesi toka Mwanza kuwa alikuwa akienda club anasindikizwa na Defender mbili za polisi na zinalinda club mpaka atakapoondoka, bado ana ndoto za kutumikia umma kama watu watamuomba.

My take: Sikio la kufa...
 
Masha anaweza kuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini nimependa jitahada zake za kuleta magari ya kisasa kuzoa taka. Tumechoka na malori yanayomwaga matakataka njiani. Kazi nzuri kijana Lau, ukisafiri iga mazuri.
 
Hata mimi nakubali ujasiri wa kuendelea kula maisha bila kutegemea ubunge, uwaziri au kuhemea vyeo vya mezani vinavyogawiwa kama njugu siku hizi.
 
You guys have failed to understand Lau... he is a great success businesswise

Kampuni yake ni kubwa, bado ni lawyer (sio ganga njaa), na majibu aliokua akitoa kama ulimsikiliza vyema alikua anakebehi wauliza maswali zaidi ya kuweka vitu wazi

Ati anatoka na chupa ya chai home kwenda kushinda rose garden hadi usiku mnene!!

He is way too ahead of the game

kazi kwenu
 
Usimdharau mtu na kazi yake,anaokota taka for special mission ya upelelezi
 
hapo kashuka?

Nadhani kazi anayoifanya kwa sasa tunahitaji aifanye kuliko kazi ya waziri (ambayo nadhani wewe ndo unaiona ilimpandisha).

Go Masha, kuwatumikia wananchi sio lazima uwe head wa wizara au mbunge.
watanzania tuna very poor indicators za kupima success

sijui nijivunie uanasiasa au biashara yangu mwenyewe??? wasio na vision watasema uanasiasa...

tuna matatizo makubwa sana aisee
 
You guys have failed to understand Lau... he is a great success businesswise

Kampuni yake ni kubwa, bado ni lawyer (sio ganga njaa), na majibu aliokua akitoa kama ulimsikiliza vyema alikua anakebehi wauliza maswali zaidi ya kuweka vitu wazi

Ati anatoka na chupa ya chai home kwenda kushinda rose garden hadi usiku mnene!!

He is way too ahead of the game

kazi kwenu


We Ulimwelewaje?? Fafanua... Kampuni kubwa kwani nani kauliza?
 
Back
Top Bottom