Home
Habari za Kitaifa
Personal Tech
KIKWETE HAKAMATIKI
KIKWETE HAKAMATIKI
Monday, 01 November 2010 00:24 administrator
* Dk. Willibrod Slaa aongeza kasi
* Profesa Lipumba anajikongoja
Na Waandishi Wetu
MATOKEO ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini jana, yanaonyesha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete, anaongoza kwa kura nyingi. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa katika baadhi ya vituo, yanaonyesha Rais Kikwete amewaacha kwa mbali wapinzani wake wanaowania kushika dola. Awali, akipiga kura katika kituo cha Msoga Shuleni, kata ya Msoga, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, Rais Kikwete alisema ana uhakika atashinda kwa kishindo. Akiwa ameongozana na mkewe, Mama Salma, Rais Kikwete alipiga kura kituoni hapo saa 5.39 asubuhi, kwa kutumia kitambulisho chake namba 487314557, ambapo aliongozwa na karani Gerald Muya.
Baada ya kukamilisha taratibu za kupiga kura, alizungumza na waandishi wa habari na waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Aliwataka wananchi kuheshimu maamuzi yaliyofanywa na Watanzania, kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.
Rais Kikwete akizungumza na waangalizi wa uchaguzi wa SADC, alisema ana matumaini kuwa serikali yake imefanya kazi kubwa katika utawala na kwamba, anaomba amani. Alisema amefurahishwa na hali ya amani na utulivu iliyoonyeshwa katika vituo vya kupigia kura katika maeneo mbalimbali nchini.
Wagombea wa nafasi ya urais ni Kikwete wa CCM, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi), Peter Mziray (APPT MAENDELEO), Mugahywa Muttamwega (TLP) na Fahmi Dovutwa (UPDP), ambaye alitangaza kujitoa.
Matokeo ya awali yanaonyesha ifuatavyo:
Kata ya Makumbusho, jimbo la Kinondoni