Lawama zinauma!

Sokwe Mjanja

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
576
297
Kwenye mapenzi kweli lawama zikiongezeka zinaumiza sana yaani, kila mara mtu unaonekana hauaminiki, unafanya vitu vingi tu tena vikubwa kwa ajili ya future lakini kila mara ni kuonekana mkosefu tu!
kweli Mapenzi ya mbali ni issue!
Hakika ladha ya mapenzi huwa inapungua sana kunapokuwa hamna trust............
 
the boss umenena vyema
hata mim ninakatabia cha hasira sana na kununa
mara kulaumu ooh hunijali mara mambo kibao kumbe nime miss tu
kwa hyo mshikajai usijisikie vibaya thts the way we are

Hiyo ni sawa na inapendeza sana Shalis ila point yangu ni kuwa kwa nini inakuwa ngumu kuwa na trust? Unajua mtu usipoaminiwa kwa kila kitu narudia tena kwa kila kitu ufanyacho inaweza kupelekea kuona huna thamani na ukawa hujali tena maana ukifanya vyema unalaumiwa ukifanya fyongo unalaumiwa then ufanye nini sasa, though haina maana kufanya ndivyo sivyo
 
Si ndio itakuwa balaa zaidi kiongozi? Tunaweza tukashindwa kutimiza hata hayo malengo yenyewe tuliyojiwekea aisee
Pole sana dear, naona umeumizwa sana ila sometimes jiulize ni kipi unaweza kufanya ili kurudisha trust. Mara nyingi ni kwa kuongea na kwakumwambia muhusika kua hujaridhika na attitude yake.
Mi najua namna nzuri ya kurudisha trust ni kuacha kuahidi vitu. Hata kama unauhakika wa kuvitekeleza, bora usiseme alafu unatekeleza tu kama surprise. Ukiahidi kitu alafu kwa sababu moja au nyingine unashindwa kutekeleza, katika mazingira ambapo trust inacheza, unaweza kuivunja kabisa na ikawa balaa.
Pia naona ni kama mtu mwenyewe yupo mbali, ukianza kusema mapenzi ya mbali ni tabu, utashindwa kuvumilia hadi atakapo rudi. Just relax.Hujui hali yake kule ikoje na hujui ni kitu gani kilimfanya kureact hivo. Nobody is perfect darling... we just try our best, and we are sorry when we are not up to the expectations.
 
Mara nyingi haya mabo huja kwa sababu mbalimbali
1. Mara nyingi mtu akitendwa sana na akafikia wakati wa kukata tamaa kuwa hamna mwaminifu then unapokuwa nae kila wakati yeye huona kuwa ndo walewale na huendelea kuwaza mabaya akidhani utamtenda pia
2. Mara nyingi tabia hiyo ya kulalamikia haiji hivi hivi, inawezekana lipo jambo ulilowahi kumtendea mwenzako ambalo likampotezea uaminifu aliokuwa nao kwako, anaweza kuwa alikuambia amesamehe lakini ki ukweli bado linamuuma, so kila wakati hilo ndo linakuwa sababu ya kukufikiria mabaya tu
 
ukiona mwanamke ana lalalma sana ujue ndo kakumiss sana...
wengine wako hivyo..aisee...hawako direct..

Dah, huu ni ukweli kabisa, yaani nilikua nikipitisha siku3 tu mwenzangu analaumu, mara anadai simpendi, mara asusie charting, Ila nikikutana nae tu yote yameisha, basi nilipogundua hilo tu lawama zikianza tu lazima nimtafute, teh teh teh, mapenzi baana!
 
Kwa kweli lamwaza zinakera sana. One of my co-workers, huwa anasema kwamba mkewe hana jema, most of the times ni kulalamika na kutafuta makosa. Kila akifanya mazuri mkewe hayaoni, yuko busy na makosa tuu.... the guy is fed up!!!

Kwa kweli, na sisi wakina dada/,mama, hebu tujiangalie, tuwape basi credit hata kidogo ndio unasema hilo kosa lalko, sio makosa tu kila wakati.

Kuna mwana pyscolojia mmoja alisema kwamba, mtu ambaye anaona makosa all the time ni NEGATIVE MINDED na in future, such a person is likely to be frustrated...the one who expect more than reality....

Pole zako kaka
 
Well said mpendwa! Na huwa inauma sana mnapopanga kitu kwa future alafu unaamua liwalo na liwe unatekeleza part yako alafu hapo hapo anachunguza anaanza ku develop negatives na inaibua ugomvi hasa! Anafikia mahali anasema kama ulifanya ni kwa ajili yako!
 
Songíto;2670312 said:
Mara nyingi haya mabo huja kwa sababu mbalimbali
1. Mara nyingi mtu akitendwa sana na akafikia wakati wa kukata tamaa kuwa hamna mwaminifu then unapokuwa nae kila wakati yeye huona kuwa ndo walewale na huendelea kuwaza mabaya akidhani utamtenda pia
2. Mara nyingi tabia hiyo ya kulalamikia haiji hivi hivi, inawezekana lipo jambo ulilowahi kumtendea mwenzako ambalo likampotezea uaminifu aliokuwa nao kwako, anaweza kuwa alikuambia amesamehe lakini ki ukweli bado linamuuma, so kila wakati hilo ndo linakuwa sababu ya kukufikiria mabaya tu

Hata kama yako mapungufu zamani kiongozi si mkishasahameana huwa vinaisha na kupita, unajua kama ulikosea ukaomba msamaha vikaisha alafu kila mara unakumbushwa kuna hatari ukawa sugu na ukaanza kuvirudia
 
inaelekea wewe mwenyewe hujiamini pia wewe mwenyewe ni mlalamishi.jiamini kwanza na maisha yako kuwa proud na confidence na unayoyafanya then utapata appreciation
 
Ndo maana wenye matatizo ya moyo ni wengi siku hizi,ndo maana mimi nimejivua gamba!
 
Hata kama yako mapungufu zamani kiongozi si mkishasahameana huwa vinaisha na kupita, unajua kama ulikosea ukaomba msamaha vikaisha alafu kila mara unakumbushwa kuna hatari ukawa sugu na ukaanza kuvirudia
mmmmhhh, this is too much! alifanya hivo?
 
Back
Top Bottom