Lawama hazijengi bali zinabomoa tu!

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mwanakijiji lawama hazijengi bali zinabomoa tu

ADELADIUS MAKWEGA
Iringa

WATU wa pwani wana msemo kuwa kila kifo kina sababu yake, huo ni msemo miongoni mwa misemo mingi katika jamii yetu ya waswahili ambapo kila jambo linalotokea basi msemo, nahau na methali zinaweza kuibuka katika kusudio la kuelezea jambo hilo.

Februari 11 mwaka huu nilisoma gazeti la Tanzania daima katika kurasa yake ile ya 10 upande wa kulia wa gazeti hilo ambayo ilipambwa na na makala ya siasa ambayo ni hoja ya Mwanakijiji yenye kubeba kichwa chake kisemacho

“Tuseme Ukweli, Bunge letu lina matatizo.”

Kama kawaida niliisoma hoja ya mzalendo huyo mwenye jina laM.M Mwanakijiji na kuangalia je makala yake ina kitu gani juu ya Bunge letu lililoharishwa hivi karibuni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa hotuba ilyohitimisha kwa kikao hicho Mkaoni Dodoma.

Ndani ya hoja za Mwanakijiji zilikuwa zimebebwa na mikasa sita ambayo iliwafika wabunge wa Bunge letu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi mbalimbali tangu kuanza kwa Bunge letu chini ya Spika Samwel Sitta mwaka 2006.


Lakini kwa hakika hoja za M.M.Mwanakijiji zilibebwa na hisia zisizo na ukweli wowote ule ambapo kwa ujumla zilikuwa na mtazamo wa kumtafuta mchawi katika misiba na matukio ambayo kwa hakika ni sehemu ya maisha ya binadam ambayo lazima atayapitia tu.

Kwa hakika suala la kutafuta mchawi kwa kila tukio hasa ya misiba inayowakuta ndugu zetu waliofariki dunia ni tabia mbaya ambayo kwa hakika inatokana na watu ambao kwa hakika si Watanzania wa leo bali ninaamini ni tabia mbaya ambayo wengi wetu inatutia simanzi na uchungu mwingi kwenye lindi la ukungu mkubwa wa kukumbuka mambo yalikwisha pita na misiba ya kupoteza ndugu zetu ambao wengine tulikuwa tukiwapenda, tukifanya nao kazi au kuwajua kwa mema yao mengi.

Hivi kweli anapokufa kabwela mbona hatuwezi kusema mkono wa fulani?. Lakini kwanini kila anapofariki kiongozi na mtu maarufu basi litasema hili na lile.

Kwani ninaamini hii ni dhana potofu ambayo sisi wana wa Tanzania ni vema kutokupenda kukuza na kuendeleza tabia hizi ambazo kwa hakika ni propaganda ambazo ndani yake kuna uongo mkubwa ambao si kitu chema kuukuza.

Watanzania mpaka sasa tumeshuhudia matukio mangapi yakishugulikiwa vema na jeshi letu la Polisi kwa kina na kuweka hadharani na hatua kadhaa zimekuwa zikichukuliwa bila ya kujali vyeo vya wahusika hao?

Adolf Hitler aliyewahi kuwa kiongozi wa Ujerumani mwaka aliwahi kusema “ kama unataka propaganda iweze kuenea na kuonekana kuwa ni kweli katika vichwa vya wananchi ni vema kuisema kila mara . Basi watu waliowengi wataamini kuwa ni kweli.”

Kwa hiyo hoja ya kudai hili na lile na lawama tele kwa Bunge letu ni propaganda tu ambazo si vema kuziendeleza tuwaache wabunge wetu wachape kazi kwani maneno matupo hayafunni mfupa Mwanakijiji.

Nikianzia na hoja ya M.M Mwanakijiji ya sita ambayo kwa hakika mimi binafsi ninaamini ndiyo iliyomsukuma kuandika makala yake ya tukio la Dokta Wilbroad Slaa na Daktari mwenzake Taarabu Ally juu ya kukutwa kwa vinasa sauti ndani ya vyumba vyao.

Mimi binafsi ninaamini ni matukio ambayo ni miongoni mwa matukio kazaa ambayo yanatokea na si suala la kuanza kulaumu polisi au serikali kwani kwa hakika adui hauwezi kujau anakuja lini kukufanyia tukio hilo baya.

Ni vigumu kusema kuwa Bunge kuwawekea utaratibu wa walinzi wabunge wote katika vyumba vyao wanavyoishi kwani kila mbunge anajua ni wapi atakapoishi wakati wa kikao vya bunge vinapoanza. Inakuwa ni vigumu kwa Jeshi la Polisi kuweza kufanya kazi ya kulinda wabunge hao katika kila makazi wanayoishi labda basi Jeshi hilo kuacha kabisa kazi zingine na kujiingiza kwenye majukumu ya kumlinda kila mbunge.

Kitendo hicho ni kigumu kufanyika kwani nchi yetu ni kubwa na ninaamini ni ubinafsi ambao si kitu chema kwa taifa letu. Suala la kulaumu Jeshi la Polisi kuwa ni wanaboronga si la kiungwana kwani mangapi mema vijana wa jeshi hili wanawafanyia Watanzania hadi kudai kuwa Jeshi ili linaboronga.Kwa Hakika Mwanakijiji hapo utakuwa umekwenda kombo mno kwa kutoa hoja ambayo kwa hakika haikufanyiwa uchunguzi wa kutosha juu jambo hili na hakika hapo sichelei kusema umekwenda kombo mno.

Ni jambo baya na la kushangaza kutoa lawama pale ambapo unachokifikilia kuwa sahihi pale unapokiona hakiwi kama unavyotaka kwani hiyo ni tabia

mbaya ambayo si ya kizalendo kwa mtu yeyote anayetakia mema taifa letu la Tanzania.Hivi tulitaka hao polisi wawe kama watwana wetu kwa kitu

Labda mazuri yote ynayofanywa na Bunge, serikali na vyombo vingine ya umma si kitu kwetu au tungekuwa sisi ni miongoni mwa watekelezaji tungefanya zaidi ya hayo?

Binafsi ninaamini kuwa Jeshi la Polisi la Mkoani Dodoma chini ya Kamanda Omari Mganga wanafanya vema kazi zao ili kuhakikisha raia wa taifa hili bila kujali itikadi wanaishi kwa amani na utulivi bila uonevu.

Labda wenzetu mmekuwa hamkumbuki enzi zile za kamata kamata ya polisi mitaani na kuwapa watu kesi ya kubambikia, hivi sasa imekuwa ni hadithi ya kale kwani polisi wanajitahidi kufanya kazi kwa kujali utu na utaratibu wa haki ni vema tukawapongeza sana.

Uchapakazi huo ndio maana unahakikisha wabunge wetu kwa sehemu kubwa wamekuwa wakihudhuria vikao vya bunge bila shaka yoyote na kurudi kwenye majimbo yao kwa amani kubwa na utulivu.

Mwakijiji kama hilo halitoshi pia ameshutumu sana suala la Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kuitisha uchaguzi pale linapotukia tukio lolote kulingana na katiba jimbo linapokuwa wazi . Hiki si kitu chema kwani si maamuzi ya serikali bali ni katiba ya nchi hii ndivyo inavyoelekeza.

Hivi kwani ata ingeingia madarakani serikali ya kikundi gani uchaguzi usifanyike labda serikali hiyo iwekuwa ya dikteta. Kwa hakika si mbunge tu bali kila raia wa nchi hii wanalindwa ndani ya nchi na katika mipaka ya taifa letu bila shaka lolote chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania na na Jeshi la Polisi .

Kwa kifo cha Mhe Chacha Wangwe ni jambo la ajali kama ambavyo jeshi letu la polisi lilivyotoa taarifa na uchunguzi wa Daktari ulivyodokeza hivi Mwanajijiji embu tujiulize kama kungekuwa na lakini hivi ndugu wa marehemu wangeweza kukaa kimya juu ya kifo cha ndugu yao?

Si kwa Wangwe tu bali ata kwa Bi Salome Mbatia na Juma akukweti ni ajali tu ,ambazo kwa hakika ni sehemu ya maisha ya binadamu yeyote yule ambayo inaweza kumkuta katika maisha yake. Hivi tunaweza kujiuliza ni ajali ngapi zinazoweza kutokea katika taifa ili zote zina mkono wa mtu? Binafsi ninaamini imani haba ambazo kwa hakika ni vema kuwekwa kando katika maisha yetu.

Kwa hakika embu tujiulize ni Watanzania wangapi ambao wanafariki kwa magonjwa mbalimbali, Je akifariki mbunge au waziri ni lazima iwe mkono wa mtu katika taifa letu? Hilo ni swali ambalo kila mtu ni vema kujiuliza na kupata jibu kuwa wabunge, mawaziri au kiongozi yeyote wa taifa hili ni binadamu ambao wamezaliwa ,wamekua na ni wajibu wao kama binadamu yeyote yule kuonja huo umauti ambao mimi, wewe lazima utatufika tu.

Kweli watanzania mpaka leo hii bado tunaamini kuwa kila kifo cha mtu maarufu ni mkono wa mtu. Hii ni imani haba ambayo kwa hakika inanikumbusha mchezo wa kuigiza wa Edwini Semzaba ambao ulikuwa ukionyesha watu waliokuwa matatizo miaka ile 1970 ambayo imani haba ziliwafanya kutokwenda kupata ata huduma muhimu za afya, kushiriki sensa na mambo kadha muhimu kwa taifa lao.

Kwa hakika Mwanakijiji kama Mtanzania mzalendo ni vema kwa kila kiachoandikiwa ni vema kuwa na mtazamo chanya wa kuiletea maendekleo taifa letu. Ata kama ungepewa nafasi ya kufanyia majukumu ya mbalmbali ya Tanzania nawe naamini usingeweza kukamilisha kila kitu.

Kuendesha taifa si lele mama bali kila jambo linafanywa kwa wakati ni vigumu kuweza kufanikisha kila jambo kwa wakati mmoja kama Mungu alivyowalisha mana wana wa Israeli kule jangwani wakati wa kuwapeleka wana hao kwenye nchi ya ahadi.

Hivi kweli Watanzania tuna mambo mangapi yakuyashughulikia mpaka kufikia hatua ya kulaumiana kila kukicha na kuyaacha mambo ya msingi. Kwa hakika jukumu letu ni kufanyakazi hili kuleta maendeleo na si vinginevyo.

Huu uandishi wa kila kukicha wa kulaumu, kwa hakika unakuwa haujengi bali ni kitu kibaya kwa hakika unabomoa taifa letu na hata taaalumu hii ya uandishi wa habari ni vema kukawa na mtazamo wa kina kwa kila kinachoweza kuandikwa kwenye magazeti au vyombo vyetu vya habari.


MWISHO
 
Last edited by a moderator:
Hongera shy kwa makala ndefu sana.
Kweli kama utunzi wa habari wewe umefuzu.
 
Acheni watu waandike. Wewe urefaree alikupa nani? Wasomaji tuna uwezo wa kuchambua wenyewe.
 
Itatoka tanzania daima kwa sababu ndio imesambazwa leo asubuhi

mwambie mwandishi aimprove arguments zake, vinginevyo kwa kweli nitaona masikitiko sana nikimjibu. Naweza kumpa ushauri kidogo wa jinsi ya kuvunja hoja yangu ya msingi.

Kitu ambacho ameshindwa kufanya ni kunukuu kauli zangu kwenye makala yake kuonesha ni wapi nimekosea.
 
Nimesha confirm itatoka jumanne ya wiki ijayo tanzania daima , changamoto , kulikoni pamoja na gazeti jipya la tanga yetu ambalo limeanza kutolewa leo
 
mwambie mwandishi aimprove arguments zake, vinginevyo kwa kweli nitaona masikitiko sana nikimjibu. Naweza kumpa ushauri kidogo wa jinsi ya kuvunja hoja yangu ya msingi.

Kitu ambacho ameshindwa kufanya ni kunukuu kauli zangu kwenye makala yake kuonesha ni wapi nimekosea.

angalia email yako ya mwanakijiji@jamiiforums.com kuna kopy yake iliyotumwa leo asubuhi yeye yuko katika jukwaa moja la bidii afrika mashariki nakumbuka na wewe ni member kule luli za nzela sijui
 
Hiyo makala orijino ya MMM iko hapa wakuu au mpaka TZ daima?
 
Naamini hii "chemistry" ya mawazo siku moja itazaa "tunda" bora, kwani nchi haijengwi kwa kuwa na rasilimali nyingi bali kwa kuwa na watu ambao si wavivu kutumia akili zao.
 
Makala anayoizungumzia huyu ndugu yetu ni hii:


M. M. Mwanakijiji

NILIKUWA najaribu kutafuta jinsi ya kuanza makala hii ya leo.

Mifano mbalimbali ambayo ningeweza kuanza nayo naona yote haifai isipokuwa niseme tu moja kwa moja bila utata, kujiuma uma au kubania maneno.

Ndugu zangu Watanzania, tuna tatizo bungeni, tuna tatizo na wabunge, tuna tatizo na mfumo mzima wa bunge hususan linapokuja suala la usalama wa wawakilishi wetu bungeni.

Tunaweza kutafuta maneno ya kupindisha au hoja za kuzungushana lakini kama inavyosemwa katika mithali kuwa ‘msema kweli ni mpenzi wa Mungu’, nimejitolea kusema ukweli ambao kila mtu mwenye fikra huru anajua ndivyo ulivyo. Hadi hivi sasa hatujafanya juhudi za kina na za wazi kuhakikisha kuwa wabunge wetu wapo salama na hivyo tumekuwa tukizembeazembea na mara kadhaa tumeshalipa gharama kubwa mno na tumelipa hadi ile gharama kuu ya uhai.

Cha kuudhi hata hivyo si kwamba hatujui tatizo bali tatizo lenyewe hata tukilijua hatuna muda mrefu wa kulifikiria na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Hata tukitaka kutafuta ufumbuzi wa kudumu kumbukumbu zetu ni fupi mno kiasi kwamba kabla hatujafika mahali pa kutafuta ufumbuzi tunakuwa tumeshasahu tatizo lenyewe!

Kifo cha Amina Chifupa

Mojawapo ya mambo ambayo tumekwepa kuyafikiria ni mazingira ya kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano, Amina Chifupa.

Mara baada ya siku ile ambapo Amina alizungumza na vyombo vya habari na kuahidi kuwa atasema ukweli wote juu ya wabaya wake, ni wazi kuwa alikuwa amejiweka katika mazingira magumu.

Je, kulikuwa na uwezekano wowote wa Amina kuzungumza tena hadharani? Jibu langu wakati ule lilikuwa ni “hapana”.

Tuliposikia kuwa familia imeamua kuwa Amina hatozungumza tena, kengele za tahadhari zililia kwenye kichwa changu na nilikuwa mtu wa kwanza kutaka Amina aachwe aseme alichotaka kusema bila kujali gharama yoyote ile. Kilichonishtua zaidi ni kuwa Amina alionekana amefichwa kwa muda mrefu na hakuna mtu aliyejitokeza kumtetea!!

Mbunge wa Jamhuri ya Muungano ameshikiliwa bila ya mawasiliano na mtu mwingine (incommunicado) na hakuna mtu aliyeshtuka. Si DPP, si DCI, si Spika, si Ikulu, si nani. Ati ni suala la familia, kana kwamba Amina alikuwa ni mtoto mdogo.

Baadaye wanatutangazia kuwa amefariki na pamoja tunatakiwa kukubali ‘mapenzi ya Mungu’! Niliandika kwa ukali wakati ule kukemea dhamira zetu zilizopigwa ganzi. Tukanung’unika pembeni, tukasema pembeni. Tukasahau. Tukasubiri tukio jingine.

Kifo cha Mhe. Juma Akukweti


Fikiria kifo cha Mhe. Juma Akukweti kufuatia majeraha yaliyotokana na tukio la ajali ya ndege pale Mbeya.

Akukweti alikwenda pale kuangalia tukio la kuungua kwa Soko la Mwanjelwa na alipokuwa akirudi Dar ndipo alipanda ndege ndogo ambayo ilishindwa kuruka, kuanguka na kuungua.

Mazingira ya kifo hicho na safari hiyo ya ndege yanatufanya tuhoji kama yote yalifanyika kuhakikisha usalama wa mbunge huyo na abiria wengine waliofuatana naye na ambao wengine pia walifariki?

Safari ya kutoka Mbeya hadi Dar ni safari ya masaa machache tu na ni ndani ya siku moja. Kwanini kulikuwa na haraka ya kurudi Dar kiasi cha kuamua kupanda ndege hii ambayo taarifa za awali zilisema ilikuwa imebeba mizigo mingi kuliko uwezo wake?

Rais Kikwete alipomtembelea Mhe. Akukweti pale hospitali alizungumza na kusema: “Nimesikitishwa sana na ajali hii, na yote yaliyotokea pamoja na kupotea kwa maisha ya watu wawili, lakini haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”

Sasa sina mashaka katika yeye kusikitishwa, lakini kweli tunaweza kusema ni mapenzi ya Mungu? Tukanung’unika pembeni, tukasemea pembeni. Tukasahau. Tukasubiri tukio jingine.

Kifo cha Mhe. Salome Mbatia

Mbunge mwingine aliyefariki dunia katika mazingira ya ajabu na yenye kuhoji uwezo wetu wa kulinda viongozi wetu ni Mhe. Salome Mbatia ambaye hadi kufa kwake alikuwa ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Kifo chake kilitokea baada ya gari lake kugongana na lori huko Iringa.

Mojawapo ya vitu ambavyo niliandika wakati ule ni kuwa kwanini mbunge ambaye haendeshi gari mwenyewe (abiria) anakaa kiti cha mbele cha abiria badala ya nyuma kama wanavyofanya majaji au viongozi wengine?

Jibu tuliloambiwa wakati ule na bado sijalielewa-marehemu Mbatia alikuwa na dereva mwingine (si dereva wake wa kawaida) na alikuwa anaendesha gari yake mwenyewe.

Kwa maneno mengine, hakuna utaratibu unaoeleweka wa wabunge kusafiri.

Tukaona picha za ajali, tukasikitika. Tukanung’unika pembeni, tukasema pembeni. Tukasahau. Tukasubiri tukio jingine.

Hadi leo hatujajiuliza yule dereva wa lori alipotelea wapi?

Si bungeni, si vyombo vya habari, si nini! Tumekubali!

Ajali za Wah. Mudhihir Mudhihir, Juma Kapuya na Zainab Vulu.


Wakati tukiwa hatujapoa vizuri au kutulia wabunge wengine wakawa katika ajali zilizotishia maisha yao.

Ile ya Mudhihir Mudhihir ilisababisha apoteza mkono wake mmoja, ya Kapuya kusababisha majeraha makubwa na ya Vulu vivyo hivyo. Tunamshukuru Mungu na jitihada za madaktari kuokoa maisha yao vinginevyo orodha ya wabunge waliotutoka ndani ya miaka hii mitatu katika ajali ingetufanya tuhoji kama yawezekana ubunge ni kazi ya mkosi zaidi!

Tukakubali kuwa ni “ajali na mapenzi ya Mungu” bila kupima kama yumkini tungeweza kuepusha ajali hizo.

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe

Kama vile katika ajali ya Mbatia, Mhe. Wangwe naye akapanda gari na dereva sijui kutoka wapi na hata sijui alikuwa na sifa gani za kuweza kumwendesha mbunge.

Yaani katika Tanzania mtu yeyote anaweza kumpatia usafiri mbunge na kwenda naye popote bila kujali mtu huyo ni nani!

Ajali ikatokea katika mazingira ya ajabu kabisa na sasa kesi iko mahakamani lakini tunajiuliza, hivi kweli yote yalifanyika kuhakikisha wabunge wetu wako salama? Kweli kama gari lilikuwa bovu au lina matatizo wabunge wanaweza kupeleka magari yao mahali popote pale?

Tuliohoji na tulihoji tena kwa hoja. Lakini, kwa ujumla wetu kama taifa tukakubali yakaisha!

Tukio la ‘unga unga’ bungeni

Tukiwa tunajaribu kutuliza mawazo likaja tukio la ‘ndumba’ bungeni ambapo hadi leo hii nina uhakika wananchi tumeuziwa mbuzi kwenye gunia.

Mara tuliambiwa kuna video zimerekodiwa kuonyesha kilichotokea, mara wachunguzi wakaja baada ya masaa kadhaa na baada ya Bunge kutumika wakachukua “vumbi” kwenda kulichunguza huko Dar. Majibu yakaja na kutuambia hakukuwa na kitu!

Tukaambiwa watu wamepagawa tu na ni washirikina.

Waandishi wakaonywa kutokuandika mambo ya kishirikina sana kwani tutatishia wawekezaji! Tukakubali.

Nina uhakika kama wangekufa wabunge kumi wiki ile wananchi tungelia, tungepigwa na hamaki, na kama watu waliolishwa dawa fulani tungeanza kuimba “mapenzi ya Mungu!”

Tukio la Dk. Slaa na Dk. Tarab

Sasa kilele cha jinsi tunavyowalinda wabunge wetu kimetokea wiki iliyopita.

Hivi ile Ijumaa kama Watanzania wangeamka na kusikia Dk. Slaa amepatwa na janga hata mauti ni nani angejua juu ya hivyo vifaa?

Vipi kama wote wawili vyumba vyao vingeungua wenyewe wakiwa ndani na baadaye tukaambiwa kulitokea “shoti ya umeme” na tukaimbiwa hadi kwa machozi kuwa yalikuwa ni mapenzi ya Mungu, kweli tungejua juu ya chupa ya mvinyo na vidubwasha vya kielektroniki vilivyokutwa kwenye vitanda vyao?

Sasa kwa vile wanatufikiria sisi hamnazo, kuna watu wanataka tuamini ati wabunge hawa walijiwekea vifaa hivyo wao wenyewe ili kutafuta sifa au kujipa ujiko. Na kuna mtu mwingine amekuja na nadharia kuwa ati wake zao kutokana na wivu walienda kutafuta vifaa hivi na kuviweka kwenye hivyo vyumba! Siwezi kushangaa kuna watu wanaamini porojo hizo!

Cha kushangaza wale wale Polisi walioboronga uchunguzi wa ‘unga unga’ ndio wale wale ambao leo wanatakiwa kuchunguza vifaa hivi ambavyo wanajaribu kutuambia ati “vinapatikana kiurahisi”. Lengo ni kutaka tuchukulie kuwa mtu yeyote anaweza kuvipata lakini hakuna anayeuliza kuna usalama gani katika maeneo ambapo wabunge wanalala?

Na hapa sijazungumzia ajali nyingine na matukio mengine ambayo msomaji unaweza kuyafikiria.

Ningeweza kusema mengi, lakini nakataa kusema ninachofikiria zaidi. Nakuomba wewe ufikirie kuwa serikali ya CCM iko tayari kurudia uchaguzi kwa mabilioni ya hela kuliko kuhakikisha ulinzi wa wabunge wetu.

Wamerudia uchaguzi wa Tunduru na Tarime na gharama nyingine nyingi kwa kiasi ambacho naamini kingeweza kabisa kulipia maafisa wa polisi, kampuni za ulinzi au hata madereva wa kudumu wa wabunge hawa!

Na kwa mtindo huu wa kurudia uchaguzi mdogo ni gharama kubwa sana kwa taifa endapo siku moja itatokea kundi kubwa la wabunge wafariki dunia au kwa namna moja washindwe kuendelea na ubunge wao. Hatuwezi kuwalinda wabunge wetu, hatuwezi kulinda Benki Kuu, hatuwezi kulinda maliasili zetu, hatuwezi kulinda watoto wetu, sisi tupotupo tu!

Nina mawazo ya mapendekezo lakini kwenye taifa la wasahaulifu na wasiojali majanga kama la kwetu tuseme nini? Tupendekeze nini bila kuonekana “wajuaji”?

Tutoe ushauri gani kabla hawajatushikia bango na kusema si mrudi nyumbani?

Ninachosema ni kuwa huu ndiyo mwaka mpya, na kama matukio yetu ya usahaulifu huko nyuma ni ishara ya kile kilichoko mbele yetu, basi tujiandae mwaka huu kwa mambo mengine ambayo wengine watasema ni uchuro!

Majanga yatakayotokea mwaka huu ni majanga yanayojulikana na yanaweza kuepukika.

Lakini kwa vile kujiandaa inahitaji kumbukumbu na sisi hatuna kumbukumbu nzuri basi tujiandae kwa machozi!! Tuendelee kusubiri tu hadi yatukute mengine.


Hata hivyo nitatoa pendekezo langu la nini kifanyike. Wiki ijayo, nikikumbuka.
 
Hata hivyo nitatoa pendekezo langu la nini kifanyike. Wiki ijayo, nikikumbuka.

Kwa maelezo yako hapa unataka kusema WABUNGE ni miungu watu na hawatakiwi kufa? Miaka mitano ni mingi sana kwa jamii ya watu zaidi ya 250 wakaao pamoja. vifo visipotokea kwa muda huo ni miujiza. Suala la mjadala wa jinsi gani wamekufa, hilo nadhani unalichochea tu. Mbona Watanzania wanakufa kama panzi kila sehemu na sioni hoja hapo.
Unles unataka kuandika na kusoma mwenyewe, wakati mwingine makala zingine huwa ni michosho sana!.
 
Kwa maelezo yako hapa unataka kusema WABUNGE ni miungu watu na hawatakiwi kufa? Miaka mitano ni mingi sana kwa jamii ya watu zaidi ya 250 wakaao pamoja. vifo visipotokea kwa muda huo ni miujiza. Suala la mjadala wa jinsi gani wamekufa, hilo nadhani unalichochea tu. Mbona Watanzania wanakufa kama panzi kila sehemu na sioni hoja hapo.
Unles unataka kuandika na kusoma mwenyewe, wakati mwingine makala zingine huwa ni michosho sana!.

jinsi unavyoreason inaonesha uwezo wako wa kufikiria hoja. Nikikubali hoja yako hapo juu najikuta naelekea huku:-

a. Kwa vile binadamu wote hufa hivyo hakuna haja ya kujilinda na kifo.

b. Kwa vile binadamu wote si miungu basi hakuna ulazima wa kuwa na hospitali kwani mahospitali yanajaribu kuepusha watu kufa, na kifo ni kitu cha kila mtu.

c. Kwa vile ajali zinatokea kwa Watanzania wengi na dunia nzima basi alama za usalama barabarani na vitu vya tahadhari visiwekwe kwani kwa kufanya hivyo ni kuingilia the inevitable.

d. Kwamba, kwa vile wabunge nao ni wanadamu tu, hakuna sababu ya kuhakikisha kuwa wanakuwa salama licha ya gharama kubwa ambayo Taifa linaingia kuwachagua.

e. Kwamba, kwa vile uchaguzi unarudiwa kila baada ya miaka mitano basi tusiwe na wasiwasi wa nani anakufa na jinsi gani mtu anakufa. HIvyo kesho ikitokea wabunge 20 wamepigwa risasi wakiwa baa au kujirusha tusiulize maswala ya ulinzi wao, kwani ni binadamu tu kama sisi!

f. Kwa vile hawa wote ni binadamu tu kama vile alivyo Rais basi tuondoe ulinzi wa Rais, Waziri Mkuu na wengine kama kufa wote watakufa!

This is what I call flawed reasoning!
 
Mwanakijiji ukiendelea kujibizana nao, nitashindwa kukuelewa. Achana nao please!

Hapa ndipo utakapogundua jinsi elimu yetu ilivyokosa ubora na jinsi isivyoandaa watu wetu. Baadhi yao ni viongozi hawa. Masikini Tanzania!
 
Back
Top Bottom