Mkuu LAT asante,
Asante kwa sababu umenisaidia kujua ukubwa wa soko la mbuzi na ni aina gani nifanye na kwa jinsi gani, kwamba ninenepeshe kwa kuchukua mikoani kwa kufanya mini livestock farming.
Mkuu, tayari nina shamba la ukubwa wa eka kumi lenye kijito ktkt kisichokauka na kabonde kazuri, nina mbuzi wa majaribio 30 tayari, ktk hao kuna mmoja tu wa maziwa. Nimechanganya mbuzi, hybrid na local wanaozaa pacha. Banda langu ni juu kama ulivyosema na lina vigezo vyote. Nimekosa kifaa cha kuhasia vidume na madawa. Kazi niliyobaki nayo ni kujifunza namna ya kuwatibu na kuwarutubisha basi. Ndoto ya kuwa na ranch kubwa ya mbuzi iko pale pale na lazima itimie.
mkuu ..... hichi kifaa kinaitwa Badizzo mimi nilinunua TFA Arusha by the time kiligharimu Tsh 40,000/= nadhani pia unaweza kukipata kwenye Vet iliyopo pale ubungo
ningekushauri uweke na Kondoo ..... kondoo ni wazuri sana na hata nyama yao ni tamu tena ni laini sana ...... advantage ya kondoo ni kwamba mzao wao ni mara tatu kwa mwaka pia wana ability kubwa sana ya ku sustain magonjwa ..... kiimani pia kondoo ni mifugo inayosadikika kuleta baraka katika maisha .... haa haaaaa haaaa naomba msini quote hapa
kuna majani yanaitwa luceni na aina fulani ya miti midogo ambayo ni fodders nzuri sana za kuboresha mbuzi ..... nikirudi dar nitakupa mbegu ya miti hii lakini luceni ni mpaka Arusha au labda shirika la elimu kibaha
mkuu .... tafuta vet mmoja akuonyeshe jinsi ya kutibu mbuzi wako rather search kwenye internet utajua, dawa ya minyoo zipo aina mbili, moja wanachoma kwenye misuli (intermascular) especially sehemu ya paja na ni 10mls kwa mbuzi ambaye yupo about 10-20kg under 10kg unachoma 5mls, nyingine inachomwa katikati ya ngozi na myama especialy kwenye shingo dawa hii inauzwa Tsh 4000/= , ipo nyingine ya minyoo ya kunywesha mdomoni..... na antibiotics ni Tsha 4500/= antibiotics huchomwa kwenye misuli tu