LAT nipe Msaada please

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Miaka kama miwili nilifika Singida kwa shughuli maalumu,niliweza kujifunza mambo kadhaa mazuri hasa kule Mtinko/Ilongelo. Nikawa na hamu ya kufika Tabora,akina Elinino/Sikonge walinipa ABC za huko. Mwaka huu nilimtuma mjumbe wangu Singida aende Wanda, Wanda kuna vitunguu sana,ila mwaka huu Wanda wamepata hasara sana.

Kuna kipande cha kutoka Itigi kupitia Chunya mpaka Mby. Kipande hiki kina uchumi sana na kimesahaulika sana, naomba uniambie miundombinu ya barabara,maji kwa kipande hicho ikoje. Na je siku za usoni kuna mipango gani. Nataka kuwekeza huko. Sikwenda Tabora kwa sababu ya majukumu mengi,ila na-plan kwenda huko Tabora na nikitoka huko nipitie Itigi kwenda Mby.

Hii haina maana ni LAT tu ndio anisaidie kupata data, ye yote anaweza kunipa. Nawasilisha.
 
mkuu malila

kwa bahati mbaya sijapata fursa ya uenyeji wa maeneo hayo nimewahi kuwa natambelea maeneo ya Mlali ya morogoro na maeneo ya Mlembule na Chamkoroma huko ni Dodoma karibu na mpwapwa , huko kote vitunguu vinastawi sana, nilifurahi kuona vitunguu vinastawishwa kwa ajili ya kutoa mbegu, hii si shughuli yangu lakini napenda kilimo

nilishangaa juzi juma nne huko Tarakea boda ya kenya na Tz nilipoona malori Fuso tatu zimejaa vitunguu zikienda kenya

nimepanga kufuatilia soko hilo

tupo pamoja
 
Kuna eneo linaitwa Mafene (linapakana na Kilosa) lipo jimbo la Kibakwe nalo linazalisha sana vitunguu...ila barabara ndio mbovu kuliko maelezo
 
Asante sana,
Lakini umetoa fursa moja tu ya kilimo cha Vitunguu, kama unaweza kunipa fursa zilizopo hupo nitafurahi zaidi,kwa sababu hii ya vitunguu naifahamu kwa kiasi fulani.
 
Kibakwe nilishatia timu siku nyingi,barabara toka Mpwapwa mpaka Kibakwe ni mbaya sana,halafu wakati wa kiangazi inapotea inakuwa kama njia ya ng`ombe hivi. Ukiwa mgeni unaweza kupotelea jangwani !!!!!!. Kibakwe ni maarufu kwa Kitunguu, kule milimani kuna maharage pia, Kibakwe kuna mbuzi wazuri sana.
 
  • Thanks
Reactions: LAT

Kule Wotta? Ambako kuna wahehe wengi sana?
 
Kibakwe nilishatia timu siku nyingi,barabara toka Mpwapwa mpaka Kibakwe ni mbaya sana,halafu wakati wa kiangazi inapotea inakuwa kama njia ya ng`ombe hivi. Ukiwa mgeni unaweza kupotelea jangwani !!!!!!. Kibakwe ni maarufu kwa Kitunguu, kule milimani kuna maharage pia, Kibakwe kuna mbuzi wazuri sana.

mkuu maharage na njegere niviona kule mlimani kijiji cha Mtega jimbo la kilosa sasa limehamishiwa Gairo ambako ukiambaa ambaa na milima unatokea Kibakwe

kibakwe pia kuna copper (shaba) nyingi sana
 
Mkuu maharage yanalipa kwa sababu unaweza ukayakausha na kusafiirisha kiangazi,njegere mbichi ni ugonjwa wa moyo. Halafu hiyo shaba naiogopa kama ukoma. Mimi nacheza na vitu vya kawaida sana,havina BP wala nini. Ni nguvu zako tu. Kibakwe imekosa barabara,kuna utajiri ile mbaya.

Turudi ktk hoja, kule nilikosema mwanzo,siwezi kufuga mbuzi? Tamaa yangu nifuge mbuzi kule Itigi/Chunya na nyuki kwa wingi na nilime alizeti. Ukanda ule bado fresh au unasemaje mkuu?
 
Asante sana,
Lakini umetoa fursa moja tu ya kilimo cha Vitunguu, kama unaweza kunipa fursa zilizopo hupo nitafurahi zaidi,kwa sababu hii ya vitunguu naifahamu kwa kiasi fulani.

Kwa kweli kilimo cha vitunguu ni kizuri coz soko ukiliotea ni kuwa biashara hii inakutoa, Maeneo ya Simanjiro Manyara karibu na mpaka wa manyara na Kilimanaro kuna eneo linaitwa Ngage Kilometer kama 60 kutoka Moshi Mjini kuna kilimo cha umwagiliaji na zao kuu hapo kwa sasa ni vitunguu na kwa kweli watu wanatoka sana na biashara hiyo. Mimi nimejaribu Heka tatu ahaaa Mungu anasaidia kwa kweli siatakosa japo M 15 (kwa hali ilivyo sasa) na hao wakenya ndo customer wakubwa wananunua mzigo shambani.

Karibuni huku!!!
 
shida yangu ni kupata eneo kubwa linaloweza kuwa na miradi mingi kwa pamoja na liwe na maji ya kutosha. Eneo chini ya eka hamsini halitoshi. Ukanda wa kilimanjaro/Arusha umejaa sana na bei ziko juu ndio maana ninatafuta Singida,Chunya. Huko bei angalau si mbaya kwa eka na ninaweza kupata pakubwa.
 
mkuu maharage na njegere niviona kule mlimani kijiji cha Mtega jimbo la kilosa sasa limehamishiwa Gairo ambako ukiambaa ambaa na milima unatokea Kibakwe

kibakwe pia kuna copper (shaba) nyingi sana
shaba hiyo inachimbwa na akina nani?wachimbaji wadogo au kuna kampuni zimeshaingia?any idea ni copper % ngapi inapatikana.je kuna reli inapita karibu na maeneo hayo ya shaba
 
Maeneo ya Mpwapwa kuna wachimbaji wadogo wadogo na Wathai fulani kama wanunuzi wa kati, Reli imepita mbali sana, si ya Tazara wala ya Kati. Kuna zaidi ya copper kule na hayo madini mengine ya vito ndio yaliyopelekea hao Wathai kufika kule.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kwa kweli kilimo cha vitunguu ni kizuri coz soko ukiliotea ni kuwa biashara hii inakutoa, Maeneo ya Simanjiro Manyara karibu na mpaka wa manyara na Kilimanaro kuna eneo linaitwa Ngage Kilometer kama 60 kutoka Moshi Mjini kuna kilimo cha umwagiliaji na zao kuu hapo kwa sasa ni vitunguu na kwa kweli watu wanatoka sana na biashara hiyo. Mimi nimejaribu Heka tatu ahaaa Mungu anasaidia kwa kweli siatakosa japo M 15 (kwa hali ilivyo sasa) na hao wakenya ndo customer wakubwa wananunua mzigo shambani.Karibuni huku!!!
katika hiyo m15 unayoitagemea utakuwa umeinvest kiasi gani?
 
Mkuu maharage yanalipa kwa sababu unaweza ukayakausha na kusafiirisha kiangazi,njegere mbichi ni ugonjwa wa moyo. Halafu hiyo shaba naiogopa kama ukoma. Mimi nacheza na vitu vya kawaida sana,havina BP wala nini. Ni nguvu zako tu. Kibakwe imekosa barabara,kuna utajiri ile mbaya. Turudi ktk hoja, kule nilikosema mwanzo,siwezi kufuga mbuzi? Tamaa yangu nifuge mbuzi kule Itigi/Chunya na nyuki kwa wingi na nilime alizeti. Ukanda ule bado fresh au unasemaje mkuu?

Malila

Kikubwa hapa ni ubora wa mbuzi, ninavyoona mimi na kwa vile nimeshafanya na kufanikiwa ni kuweza kupata eneo kubwa karibu na Dar hata kama ni kibaha kwa ajili ya mradi wa kuboresha mbuzi, soko la mbuzi ni kubwa sana Dar, kinachotakiwa ni kuleta mbuzi kutoka Singida, Shiyanga na Tabora halafu ukawaweka katika intermediary ranch/farm, hapo wakifika una wapa na kuwapiga sindano za dawa ya minyoo (deworms), unawaogesha na deep, una wapa multi vitamins pamoja na kuwapa antibiotics (OTC) kwa magonjwa mbali mbali, zaidi unajitahidi kuwapa grains (pollards, pumba za mahindi) na health value ingridients kama mashudu ya pamba na alizeti na majani kama luceni

mkuu.... baada ya mwezi mmoja utaona product hiyo ya mbuzi itakuwa na kiwango kikubwa sana, kwanza wataongeza uzito, pili watakuwa katika hali ya usafi, tatu watakuwa na uwezo mzuri wa kuzaliana

kikubwa ni kujaribu kuchagua mbuzi wengi wa kike tena wenye mimba pale unapokua unanunua hawa mbuzi mnadani au kwenye maboma ya watu, jitahidi kuwa castrate madume na ubakize machache, kuna kifaa maalum cha kufanya hiyo kazi kinaitwa badizzo kiko kama mkasi hivi

tengeneza banda la mabanzi ambalo ni suspended na flooryake iwe ni ta mabanzi ambayo inatengenezwa in treli like (kama chaga za kitanga, yaani inakuwa na gaps kila baada ya banzi na banzi) ili kuruhusu vinyesi kupita,

ku control stock tumia ear tags zenye namba au alama fulani na kila unapouza una itoa na ku stock out kwenye kitabu chako cha stock .......mbuzi hawa watazaliana kwa wingi kila mara na pia utakuwa ukiendelea kununua stock mpya kila baada unavyo uza stock yako,

amini mkuu.... soko la mbuzi ni kubwa na lilinishinda, nilifanya kama hobby au part time lakini sikutegemea inaweza kuwa project per se katika kashamba kangu bagamoyo ..... watu wengi hupenda kununua mbuzi ambao wanafugwa kwa style ya livestock farming (goat meat farming) na siyo mbuzi wa machungani kama wa masai na wasukuma

nilijaribu mbuzi wa maziwa ambao stock yeke ilitoka Uingereza walioletwa kwa mradi wa kusaidi waathirika kibaha .... du nilichemsha ... yaani wapo delicate vibaya sana

Malila ... wazo lako la project ya mbuzi wa nyama ni zuri sana
 
Mkuu LAT asante,

Asante kwa sababu umenisaidia kujua ukubwa wa soko la mbuzi na ni aina gani nifanye na kwa jinsi gani, kwamba ninenepeshe kwa kuchukua mikoani kwa kufanya mini livestock farming.

Mkuu, tayari nina shamba la ukubwa wa eka kumi lenye kijito ktkt kisichokauka na kabonde kazuri, nina mbuzi wa majaribio 30 tayari, ktk hao kuna mmoja tu wa maziwa. Nimechanganya mbuzi, hybrid na local wanaozaa pacha. Banda langu ni juu kama ulivyosema na lina vigezo vyote. Nimekosa kifaa cha kuhasia vidume na madawa. Kazi niliyobaki nayo ni kujifunza namna ya kuwatibu na kuwarutubisha basi. Ndoto ya kuwa na ranch kubwa ya mbuzi iko pale pale na lazima itimie.
 
Malila sorry kama swali langu litasound personal kwani sio nia yangu hiyo. Hilo shamba liko wapi? Sisi wengine tunapata hamasa ya ajabu tunaposoma vitu kama hivi so mkiwa specific zaidi inspiration tunayoipata kutoka hapo lazima Mungu atawabariki.

LAT nikushukuru pia hapa kwa msaada mkubwa unaoutoa siku zote, ni kitu kizuri kutokuwa mchonyo na knowledge kwani kadri unaovyoshare ndivyo unavyozid kuwa deep kwenye eneo husika.
 
Malila sorry kama swali langu litasound personal kwani sio nia yangu hiyo. Hilo shamba liko wapi? Sisi wengine tunapata hamasa ya ajabu tunaposoma vitu kama hivi so mkiwa specific zaidi inspiration tunayoipata kutoka hapo lazima Mungu atawabariki. LAT nikushukuru pia hapa kwa msaada mkubwa unaoutoa siku zote, ni kitu kizuri kutokuwa mchonyo na knowledge kwani kadri unaovyoshare ndivyo unavyozid kuwa deep kwenye eneo husika.

Hili shamba liko Mkuranga, Mkuranga ni ya ajabu, wengi wana amini kuwa Mkuranga hakuna mito midogo ya kudumu, lakini kuna mito mitatu upande wa mashariki ya Mkuranga wilayani, mto Mduzi, mto Galawani na Mto Kogamimba, yote hii huingia ktk bonde zuri na kufanya mto Mbezi. Kutoka Mbagala mpaka galawani kuna daladala za moja kwa moja na nauli ni Tsh 2500/ mpaka Shungubweni. Ni km 60 toka Tazara Dsm mpaka hapo shambani.

Au kama unataka maeneo kama hayo, yapo Marogoro Mkuranga, Nauli toka Mbagala kwa daladala ni Tsh 1500/ huko kuna mto Koga mimba. Kwa ufupi ni sehemu nzuri, kuna jf members watano ambao tumeanza pale Galawani mwaka jana. Ni km 43 hivi toka Tazara mpaka Marogoro. Hapo Marogoro ndio wanapotarajia kujenga uwanja mpya wa ndege wa kimataifa.
 
Kwa kweli kilimo cha vitunguu ni kizuri coz soko ukiliotea ni kuwa biashara hii inakutoa, Maeneo ya Simanjiro Manyara karibu na mpaka wa manyara na Kilimanaro kuna eneo linaitwa Ngage Kilometer kama 60 kutoka Moshi Mjini kuna kilimo cha umwagiliaji na zao kuu hapo kwa sasa ni vitunguu na kwa kweli watu wanatoka sana na biashara hiyo. Mimi nimejaribu Heka tatu ahaaa Mungu anasaidia kwa kweli siatakosa japo M 15 (kwa hali ilivyo sasa) na hao wakenya ndo customer wakubwa wananunua mzigo shambani.Karibuni huku!!!
Mkuu mil 15 kwa hekta are u serious?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom