Language

Side buggati

JF-Expert Member
Feb 8, 2015
219
175
Shida yangu kubwa ni neno "was" ukitaka kulitumia na verb unatumia verb gan Kat ya irregular verb, past au partipaticiple mfano juz boss aliniambia I was not seen you in an office hpo ilo neno seen ni past participle ya verb je ni sawa hpo naomben ufafanuzi wa kina
 
Ulimsikia vizuri? Kuna uwezekano alisema ' I was not seeing you in the office' Au boss angesema ' I have not seen you in the office'
 
I didn't saw you in the office if it's past...
DID imetokana na mnyumbuliko wa DO. maumbile mengine ya kitenzi saidizi hiki ni (DO, DOES, DID) ukishaanza na moja ya viambishi hivi kitenzi kinachofuata kimesaidiwa kubeba dhana hivyo hakibadiliki
 
Shida yangu kubwa ni neno "was" ukitaka kulitumia na verb unatumia verb gan Kat ya irregular verb, past au partipaticiple mfano juz boss aliniambia I was not seen you in an office hpo ilo neno seen ni past participle ya verb je ni sawa hpo naomben ufafanuzi wa kina

Japo kwa uchache na kwa kuchanganya lugha (si vizuri kujifunza lugha kwa kuchanganya)

WAS/WERE inatokana na kitenzi TO BE
PRESENT (Wakati wa Sasa/uliopo)
I am
You are
He/she/it is
We are
They are

PAST (Wakati Uliopita)
I was
You were
He/She/It was
We were
They were

I was at the office yesterday (Nilikuwa ofisini jana)
They were playing with the children last weekend (walikuwa wanacheza na watoto wikiendi iliyopita)

Hivyo am/is/are na was/were hutumika kama kitenzi kikuu (main verb) --angali sentensi ya kwanza-- au kitenzi kishirikishi (helping verb)--angalia sentensi ya pili.

Japo kuna wakati 'I' huendana na 'were'; ukitumia Conditional Clauses/If Clauses
Kwa mfano: If I were you, I would not go outside ( Ningekuwa wewe, nisingeenda nje)

HAVE/HAS hutumika kuonyesha wakati mtimilifu au utimilifu wa tendo; aidha kwa wakati uliopo au wakati uliopita

I have done my work (Nimefanya kazi yangu)
She has gone to the shop (Ameenda dukani)
Have they stayed long? (Wamekaa muda mrefu?)

The car had left early (Gari lilishaondoka mapema)
We had already eaten at the hotel (Tulishakula hotelini)
Had you gone swimming at that beach? (Ulishaogelea katika ufukwe huo?)
 
I didn't saw you in the office. Alikosea ila kwa kibongobongo tunaelewana mn lugha ni ngumu kwa tuliopitia kayumba ss.
Isitoshe lugha hii ilikuja kwa msaada wa meli. hivyo hata kizigua,kimasai, kikurya, kihangaza, kinyiramba n.k ni lugha kamili kabisa bora zikamilishe malengo ya watumiaji
 
Back
Top Bottom