Lameck Airo Vs. John Mashaka..Rorya 2015

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Lameck aligusa nyoyo za watu na hata kumshinda mpinzani wake mkubwa Prof. Monyo. Lameck alitoa kituko cha mwaka, kwa kusema kwamba, Darasa la saba mpo??? basi umati mkubwa ukaitika tupo... Basi hiyo ndio ikawa signature yake kwenye kampeni.......Darasa la saba ukawa ndio wimbo wake. ....
 
We ndio huyo John?! Mbona hatujui CV yako na uhanarakati wako!! lete CV tupitie basi.
 
Amini msiamini, naona mchuano mkali kati ya Lameck Airo na Bwna mdogo John MAshaka 2015. Lameck aligusa nyoyo za watu na hata kumshinda mpinzani wake mkubwa Prof. Monyo. Lameck alitoa kituko cha mwaka, kwa kusema kwamba, Darasa la saba mpo??? basi umati mkubwa ukaitika tupo... Basi hiyo ndio ikawa signature yake kwenye kampeni.......Darasa la saba ukawa ndio wimbo wake. .... Ila kwenye uchaguzi wa 2015, kuna tetesi za uhakika kwamba atapambana na mwanaharakati John Mashaka ambaye anaheshimika na kukubalika siyo kawaida kwenye jimbo la Rorya. Vile vile kuna tetesi kwamba mashaka ambaye amekulia Ukonga, anaweza kugombea Segerea. Tunasubiri tuone ni wapi, ila Lameck atakuwa na wakati mgumu sana 2015

Huo ni umbea, kwanza wabunge ndiyo wameaanza kipindi chao cha 5yrs, anything can happen in btn , kwa hiyo huyo unayomuita mashaka huwezi sema ataleata upinzani mgumu miaka minne ijayo.
 
Wako kama watano tayari na wenye elimu na fedha za uhakika kugharimia walau kampeni za kawaida. Bwana mdogo naona umechelewa. Baadhi yao walitaka kugombea 2010 wakawapisha Mashishanga na Mpendazoe.
 
Hakuna Mbunge wa hovyo kama Lameck Airo. Aliwahonga wakurya na wajaluo gongo akaingia Bungeni akidhani atatumia mali zake kuleta maendeleo Rorya lakini hadi sasa ameshindwa kabisa kuleta maendeleo na wala hana changamoto yotote Bungeni.

Hata sijui kama huwa anahudhuria. Kuna vijiji huko Rorya vina miundombinu ya maji kwa maana ya ntandao wa mabomba lakini havipati maji toka ziwani eti kwa sababu mashine ya kusukuma maji imeharibika.

Airo anashindwa hata kupigania hilo tu acha matatizo lukuki ya Rorya. Airo ni afadhali angekimbia mapema na kuwaaachia wanarorya jimbo lao.
 
John Mashaka ni nani? Atagombea Rorya kwa tiketi ya Cham gani? Anaifahamu Rorya au anaisikia tu kwenye vyombo vya habari? Rorya ni zaidi ya unavyoifahamu...!!
 
John Mashaka ni nani? Atagombea Rorya kwa tiketi ya Chama gani? Anaifahamu Rorya au anaisikia tu kwenye vyombo vya habari? Rorya ni zaidi ya unavyoifahamu...!!
 
Who is John Mashaka? Hajulikani Rorya. Acha uongo. Kama unamjua ni wewe, jirani zake na kijiji chake anakotoka. Ukimwangalia hana hata haiba ya kuwa mbunge wa Rorya. Pili ni mtu wa CCM. Si mwanaharakati kama unavodai bali mtafutaji tu kupitia pesa za wafadhili.
Ni kweli Rorya 2015 Airo hawezi tena kuwa mbunge lakini mashaka na ccm hawawezi tena kupata nafasi ya ubunge. Mashaka, Maina Owino na ccm orphans wengine wahesabu tu maumivu hakuna chao Rorya.
 
Hakuna Mbunge wa hovyo kama Lameck Airo. Aliwahonga wakurya na wajaluo gongo akaingia Bungeni akidhani atatumia mali zake kuleta maendeleo Rorya lakini hadi sasa ameshindwa kabisa kuleta maendeleo na wala hana changamoto yotote Bungeni. Hata sijui kama huwa anahudhuria. Kuna vijiji huko Rorya vina miundombinu ya maji kwa maana ya ntandao wa mabomba lakini havipati maji toka ziwani eti kwa sababu mashine ya kusukuma maji imeharibika. Airo anashindwa hata kupigania hilo tu acha matatizo lukuki ya Rorya. Airo ni afadhali angekimbia mapema na kuwaaachia wanarorya jimbo lao.

Unakumbuka lile sakata la yeye (lameck Airo) kulalamikia viongozi wa chama chake kumwekea kauzibe asilete maendeleo jimboni nao wakaufyata? Rorya ni zaidi ya unavyoifahamu...usije shangaa 2015 anarudi bungeni...wewe na mimi hatufahamu
 
Mkuu platozoom ni kwamba Airo hagombei ten huko Rorya na wala hawezi kupata tena Ubunge. Ofcourse alishasema hagombei kama unatka kwenda wewe piga tu jalamba.
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa alikuwa anatafuta ubunge ili mambo yake ya kibiashara yaenda kirahisi.
 
Ukweli ni kwamba Lameick Airo ameshatangaza kwamba hatagombea tena ubunge Rorya. kwasababu pamoja eti na kuwaletea maendeleo kwa kutumia pesa yake (barabara, madawati, visima vya maji) Lakini wanarorya wanamtukana eti hakusoma darasa la saba (ambayo BTW ndiyo ilikuwa slogan yake wakati wa kampeini 2010).

Sasa hivi CCM wanamuandaa Waziri wa Vijana na Ajira Mh. Gaundesia Kabaka. Sijui CDM wanamundaa nani? Ninakumbuka Mabere Nyaucho Marando aliwahi kulichukia hilo jimbo 1995 alipokuwa NCCR Mageuzi.
 
Mkuu niko karibu na Lameck na has no interest na ubunge anymore, hivyo ondoa shaka mkuu songa mbele, amekwisha hata watangazia.
 
Ukweli ni kwamba Lameick Airo ameshatangaza kwamba hatagombea tena ubunge Rorya. kwasababu pamoja eti na kuwaletea maendeleo kwa kutumia pesa yake (barabara, madawati, visima vya maji) Lakini wanarorya wanamtukana eti hakusoma darasa la saba (ambayo BTW ndiyo ilikuwa slogan yake wakati wa kampeini 2010).

Sasa hivi CCM wanamuandaa Waziri wa Vijana na Ajira Mh. Gaundesia Kabaka. Sijui CDM wanamundaa nani? Ninakumbuka Mabere Nyaucho Marando aliwahi kulichukia hilo jimbo 1995 alipokuwa NCCR Mageuzi.
Mkuu Bobuk naona huijui Rorya wewe. Gaudencia Kabaka anataka kugombea Tarime siyo Rorya. Pia ufahamu kwamba Rorya kuna ukabila wa kufa mtu. Lile jimbo ni la wajaluo hivyo hakuna mkurya ama kabila lingine abayeweza kupata ubunge pale hasa kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Mbunge wa hovyo kama Lameck Airo. Aliwahonga wakurya na wajaluo gongo akaingia Bungeni akidhani atatumia mali zake kuleta maendeleo Rorya lakini hadi sasa ameshindwa kabisa kuleta maendeleo na wala hana changamoto yotote Bungeni.

Hata sijui kama huwa anahudhuria. Kuna vijiji huko Rorya vina miundombinu ya maji kwa maana ya ntandao wa mabomba lakini havipati maji toka ziwani eti kwa sababu mashine ya kusukuma maji imeharibika.

Airo anashindwa hata kupigania hilo tu acha matatizo lukuki ya Rorya. Airo ni afadhali angekimbia mapema na kuwaaachia wanarorya jimbo lao.
Kimbunga kwa unafiki
 
Last edited by a moderator:
Lameck Okambo Airo alibaka ubunge na ukweli ni hawezi ubunge kwani hata ukimuuliza maana na kazi ya mbunge hatokupa jibu kamwe! Yule alitumwa na Lowassa ili kumsaidia Lowassa kutimiza ndoto zake 2015! Hutaki unaacha na ukweli ndo huo....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom