Lakisihela village

STABLE GIRL

Member
Feb 7, 2011
19
2
Kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Wakati wengine wakifa njaa wengine wanaona laki si hela. Hapo chanika kuna kijiji kinaitwa lakisihela kwa maana kwamba mtu anayeishi hapo kutoa rushwa ya laki moja kwa afisa wa polisi au mheshimiwa fulani si tatizo.
Kijiji hicho kimejificha sana kiko ndani ya hifadhi moja ya msitu wa asili karibu na mahandaki ya jeshi yaliyochimbwa kwa tahadhari ya vita. Watu wake wanajishughulisha na uvunaji wa miti na uchomaji wa mkaa kinyume cha sheria, pia wanachimba mchanga, wanawinda kwa kutumia silaha wanazopewa na askari wanaolinda handaki hilo au wanaoziuza kwa laki au pungufu, pia wanavuna mbolea ya popo inayopatikana katika handaki hilo. Kazi yao ambayo inawapa au kuwaletea migogoro wanakijiji hao ni biashara ya pombe haramu ya gongo.
Waungwana tunakwenda wapi?
 
Back
Top Bottom