Lake Ngozi (Ziwa Ngozi) na simulizi za ajabu

Fika Mbeya mjini au Uyole. Panda gari ziendazo Tukuyu au Kyela. Shuka kituo kiitwacho number one.Eneo hili ndipo waliungua na mafuta ya petroli watu wengi miaka ya nyuma baada ya kuanza kukinga mafuta toka lori lililopinduka!. Hapa tafuta wazee wenye busara na wenyeji wakuelekeze taratibu za kwenda ziwani. Usiwe curious na kwenda peke yako kwa kutumia GPS,Google maps nk. Waliojaribu u kisasa hawakurudi!


Nashukuru sana
 
ngozi-crater-lake.jpg
 
siyo mambo ya chemchem za moto ndio imesababisha kuchoma mawe yakawa mekundu hivyo na kuhama sio mambo ya movement za plates za chini ya ardhi? lilihama kutoka wapi kwenda wapi
maanna loliondo kunamchanga unaohama ndivyo wanavyoita ila ni upepo ukielekea huko basi ule mchanga unajikusanya taratibutaratibu na kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine tena si hatua nyingi. ila kama ziwa liliama kutoka posta hivi hadi kimara pana jambo.
mkuu naona una apply map late tectonics
 
ziwa hilo lina ingiza tuu maji na hali toi maji kwa sababu liko katikati ya milima alafu halina ufukwe kwani ukiwa ukingini kabisa uka jalibu kupima kuna ni parefu na haijulikani ni mita ngapi kwenda chini kwa hivyo huwezi kuogelea kwenye ziwa hilo lililoko maeneo ya upoloto ukiwa una toka mbeya una shuka kituo kina itwa nymbe one alafu una tembea kilomita 12 ili kufika ziwani
mbona sisi tulienda pindi nipo o level tuliogelea sana tukapiga picha bila tukio lolote lile kutokea
 
Mbona kuna barabara inafika huko na unatembea kidogo wakati unapanda kilima then unashuka kidogo unafika ziwani.Mimi nimefika mwaka 2011,maji yake yamatumika na kuna watu wanaishi jirani.Pia kuna ziwa jingine dogo lipo jirani na hilo.

Hakuna mtu anaeishi karibu na Lake Ngosi(ngozi)..
 
Hilo ziwa nshawahi kulisikia, eti wazungu walienda kufanya uchunguzi wakazama. Wakaenda kundi jingine wakajifunga minyororo ya chuma kwenye miti kisha wakaingia ziwani, minyororo ikakatika, wakazama.

Hapana..

Ambako wazungu walipotea ni MTO WA MUNGU.. upo mbozi
 
ziwa hilo lina ingiza tuu maji na hali toi maji kwa sababu liko katikati ya milima alafu halina ufukwe kwani ukiwa ukingini kabisa uka jalibu kupima kuna ni parefu na haijulikani ni mita ngapi kwenda chini kwa hivyo huwezi kuogelea kwenye ziwa hilo lililoko maeneo ya upoloto ukiwa una toka Mbeya una shuka kituo kina itwa nymbe one alafu una tembea kilomita 12 ili kufika ziwani

Sio upoloto ni Uporoto,kwa wenyeji wa mbeya tunapaita MPOROTO
 
Sasa kama hautakiwi kuongea Kinyaki so ni lugha gani ya kutumia ya wenyeji KISAFWA au English?
Mkuu Caldera ni shimo litokanalo na milipuko ya kivolcano.
Geothermal ni chem chem za maji ya moto ardhini ambazo hutokana na volcanic activities bila shaka ni goegraphy ya form 3 on Vulcanicity.

Caldera kama imepita porous rock au Aquifer panatokea ziwa. Pia geothermal inaweza kuwa taped kutokana mvuke wa magma. Any form (maji,mvuke,magma) of energy comes from rock/geo panaweza tengenezwa thermal plant to generate energy.
 
Nilishawahi sikia zamani sana kwa Geologist mmoja kuwa Lake Duluti, Lake Ngozi na maziwa mengine mengi yana connections ambazo zipo chini ya ardhi. Ni kama mito inayoflow chini ya ardhi ambayo huenda kumwaga maji yake mostly in the Oceans. Ngoja nitafute more dataz, nitarudi baadaye

Mkuu, Volkano inapolipuka inapita kwenye layars za miamba tofauti,sasa ikilipuka na kuipitia Porous rock/Aquifer inatengeneza crater lake au caldera.
 
Mimi nimesoma maeneo ya huko nlivyokuwa form 3 tulienda huko maana ya kuona crater lakes zilivyo. Kitaalam lile ziwa huwezi sema lilihama, maana ule mlima udongo wake ni majivu kabisa (lava). Na kusema kweli hadi kufikia kingo za maji yaani ni steep slop ambayo sehemu zingine inakulazimu kushika mizizi ya miti ndipo upate kushuka nayo, sijui labda kama kuna njia nyingine ila kwa njia tulopita sisi ni hatari sana. Na ukifika kwenye kingo zake huoni hata chini yaani anaesema aliogelea ni uongo maana kina chake kinatisha sana na sisi tulipewa condition kuwa tukifika tusiguse maji yake. Ziwa liko mbali na makazi ya watu hivyo halitumiwi kwa matumizi yoyote nyumbani wala shamba. Nakuhakikishia lile ziwa huwezi kuogelea kwa maana linatisha kweli. Yayo ndo niliyoyaona na kuyajua kuhusu lake ngozi (Ziwa ngozi)

atleast wewe umeongea ukweli kiasi chake
 
2Q==
Z

Lake ngozi lipo "crater lake" ambalo lipo Isongole karibu na mji wa Tukuyu katika wilaya ya Rungwe, ni ziwa la pili kwa ukubwa kwa maziwa ambayo ni "crater lakes" ktk bara la Africa. Lina ukubwa wa 2.5 km x 1.5 km (3.75 sq KM)
 
Back
Top Bottom