Lake Ngozi (Ziwa Ngozi) na simulizi za ajabu

Sasa kama hautakiwi kuongea Kinyaki so ni lugha gani ya kutumia ya wenyeji KISAFWA au English?
Mkuu Caldera ni shimo litokanalo na milipuko ya kivolcano.
Geothermal ni chem chem za maji ya moto ardhini ambazo hutokana na volcanic activities bila shaka ni goegraphy ya form 3 on Vulcanicity.
Mambo ya jiografia ya form three.
 
yah ni kweli kabisa mazee na lina dhahabu ndani yake na kuna samaki wana manyoya kuna wazungu wengi tu wanakufa wanajaribu kwenda chini kuchukua mali zile ila inashindikana wanakufa we njoo mb utapata full story na liliama baada ya kuchoma moja jiwe kwa week 4 likawa jekundu kama nyanya ndo kesho lake likaaama mazee

Mmmmhh!!!
 
Hilo ziwa nshawahi kulisikia, eti wazungu walienda kufanya uchunguzi wakazama. Wakaenda kundi jingine wakajifunga minyororo ya chuma kwenye miti kisha wakaingia ziwani, minyororo ikakatika, wakazama.

I heard that stories, nimesoma somewhere in mbeya several kilometers from that ziwa. My fellow students by then walienda kuvisit. Many wonders happen from there nasikia...
 
Lilihama toka mbali sana mkuu, nadhani ni kama toka Ubungo(Dar) mpaka Chalinze hivi, nasikia lilikuwa na maajabu zamani lakini siku hizi lipo tu na halina maajabu. Nimewahi kwenda kutembelea na nimeoga kabisa ila maji ni mazito sana na kwa asilimia kubwa chini ni matope. Nikitulia na nikiwa kwenye pc ntaweka na picha kabisa maana zipo nyingi tu.

hapa lazima yawepo maelezo yakutosha kushawishi,wanasayansi wa mambo ya ardhi watueleze vp hii?
 
Wakuu,kuna rafiki yangu mrombo aliwai nihadithia huko kwao kuna ziwa challa,aliniambia maji yake ni ya kijani,je ni kweli?je ziwa hilo lipo?
 
mimi nilishafika kabisa kwenye hili ziwa Ngozi, Sio la ajabu sana kama watu ambao hawajafika wanavyolisimuria kweli lipo katikati ya milima na kuna pori kubwa sana na kuna baridi na mawingu au ukungu. Tulipokuwa njiani kuelekea kwenye hilo ziwa dogo tuliambiwa na wenyeji tuwe makini sana kuna wakati ukungu huwa unazidi na kufanya giza kubwa. Kwa wanao ifahamu Mbeya vizuri kuna njia rahisi ya kwenda ziwa ngozi kwa kupitia Uyole.
 
yaa kuna kakitabu kahistoria ya wanyaki kalikuwa kanasimulia hili, kuhusu kuhama inasemekana lilikuwa linawazingua na maajabu yake hivyo wakachoma jiwe kubwa lilipokuwa lekundu wakalitumbukiza kwa ziwa basi maji yakakauka kuelekea huko milimani
 
Mimi nimesoma Iwalanje High school nami ni Mnyakyusa mbona niliogelea na kunywa Maji yake lakin suala la Kuongea kinyakyusa sina experience......
 
Wakuu,kuna rafiki yangu mrombo aliwai nihadithia huko kwao kuna ziwa challa,aliniambia maji yake ni ya kijani,je ni kweli?je ziwa hilo lipo?

Ni kweli ziwa Chala lipo na linafanana na hilo la Ngozi isipokuwa ziwa Ngozi maji yake yapo mbali san kuliko ya Chala ambayo unaweza kuyafikia kwa kutembea kwa dk kama 20 kupitia kingo zake hadi kule chini. Watu wanaogelea na kuvua samaki.Maji yake ni yakawaida na rangi anyodai ya kijani ni 'mwangwi' wa miti na majani yanayozunguka ziwa hilo.inasemekana robo tatu ya ziwa Chala ipo Tanzania na sehemu iliyobakia ipo Kenya.
 
Ngoja tuweke picha... deo 164.JPG deo 164.JPG
 
Kama ni cadela lake unaweza peleka maloli ata millioni ya mchanga ukashangaa bado haujaweza lifukia.
Kuna potential ya kulitumia kwa ajili ya geothermal power!

Wazo la kisomi kama hili wengine hawalifikirii haraka haraka!
Ndo kitu kinachoenda kufanyika ndani ya muda mfupi ujao
 
Hilo ziwa nshawahi kulisikia, eti wazungu walienda kufanya uchunguzi wakazama. Wakaenda kundi jingine wakajifunga minyororo ya chuma kwenye miti kisha wakaingia ziwani, minyororo ikakatika, wakazama.

Mkuu naona kama umechanganya kidogo hiyo habari ya wazungu ni sehemu nyingine 7bu hizo sehemu mbili zote nimefika what I see lake ngozi is just a huge crater Coz hata huwezi ona maji yanapo ingilia wala kutokea, na huko kwa wazungu ni sehemu kama mto unaoingiza maji sehemu ambayo maji hayaeleweki yanapo elekea
 
Mara nyingi maziwa kama haya huwa ni volcanic lakes,inlates and outlates zinakuwa chini.
Niliwahi kusikia kuwa Lipo ziwa linaitwa DULUTI huko Arusha maeneo ya Tengeru kuwa linaendana tabia na hili ngozi.
Hilo ziwa (Duluti) halitoi maji wala hakuna mto unaoingiza maji lakini iwe masika iwe kiangazi maji hayaongezeki wala kupungua, pia kina chake hakijulikani.
Sijui kitaalam hii ikoje.
 
Back
Top Bottom