Laiti Kama Wazanzibari Wangeukataa Muswada wa Kuunda Tume ya Katiba Mpya!

LordJustice1

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
2,263
530
Wazanzibari wanaogopwa sana na Viongozi wetu wa Serikali ya Muungano! Laiti kama wangeuchana tena Muswada wa kuunda Tume ya kukusanya maoni kuhusu Katiba mpya JK asingethubutu kusaini Muswada husika! Hali inavyoelekea JK atausaini Muswada huo bila kujali kelele za aina yoyote toka Bara! Hata hivyo JK ana-create matatizo makubwa sana kwa Tanzania ijayo! Kelele kuhusu "Katiba mpya nyingine" hazitaisha na umoja na mshikamano wetu utaendelea kumomonyoka siku hadi siku! Serikali kwa kutokuwashirikisha wananchi katika mchakato huu wa Katiba mpya inafanya kosa lile lile lililofanywa tangu Uhuru zilipoundwa Katiba nyinginezo!
 
hiyo hata mimi nime note, wazanzibari wakidindisha tu-ccm na serikali yake wanainama! hata bungeni ukiangalia utaona wabunge wazanzibari wanatoa kauli kali tena za kudhalilisha kwa watanganyika lakini utaona spika hasemi lolote na wabunge wa ccm
wote kimyaaa! yaani wanapelekeshwa kinoma-kuna kitu!
 
Kuna kitu kinaitwa kuogopa nchi au muungano kumfia JK hilo analiogopa sana sana maana historia haitamsahau kamwe!!
 
Hilo la serikali kuwaogopa Wazanzibar ni kweli kabisa. Nashindwa kuelewa hawa Wapemba wamewalisha nn viongozi wa CCM
 
yah ni kweli, Zanzibar ni mshirika muhimu wa huu muungano, bila Zanzibar hatuna Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, itabaki Jamhuri ya Tanganyika.
Nahisi ni vizuri chama kikuu cha upinzani (CDM) kiwatumie WaZanzibari ili tuweze kupata Katiba iliyo nzuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom