Ladies kama wewe utachukua hatua gani?

sasa na yule kaka aliyejitambulisha na akasema atamuoa huyo binti wa kazi, ameishia wapi?
Preta baada ya hili sakata kuwa wazi ..huyu jamaa hajaonekana mpaka leo ..na mbaya zaidi huyu mama hakumfatilia hata kujua anakaa wapi
Ingawa jamaa alikuwa anajitahidi kuja hapo nyumbani kabebelea ,nguo pesa na matumizi mengine ya mama na mtoto.
 
Huyo mama wala asijihangaishe kumfuatilia huyo mkaka, manake inaonekana baba na h'gal walimtengeneza ili kuficha ukweli...hata hizo nguo na pesa za matumizi yaezekana pia alikuwa anapewa na baba mwenye nyumba... Kuna wanaume wabaya ndugu yangu, mara mia ukutane na simba kuliko kukutana na mwanaume dizaini ya huyo mbaba, unakula nao na wabaya ni hao, hao! Shame on him!
 
Chauro hiki kisa kimenisikitisha sana kila nikiwaza sipati majibu ,hivi unakaa na adui ndani ..mnakula sahani moja bila kujijua mpaka mtu anazaa na mmewe bila kutambua.
Inauma aisee!...unamlea h'gal kwa upendo wote kisa mjamzito kumbe mimba ni ya mumeo!.. Daaah! Sipati picha maumivu ya huyo mama yakoje!
 
Preta baada ya hili sakata kuwa wazi ..huyu jamaa hajaonekana mpaka leo ..na mbaya zaidi huyu mama hakumfatilia hata kujua anakaa wapi
Ingawa jamaa alikuwa anajitahidi kuja hapo nyumbani kabebelea ,nguo pesa na matumizi mengine ya mama na mtoto.
Halafu nimeshtuka sasa, dizani kama kuna dili lilikuwa limechezwa na hao watu watatu ukimtoa wife wa jamaa maana jamaa anatokomea tu ghafla mhhh!!!
 
Mpe pole huyo dada mmmmh!sipati picha hayo maumivu yake,maumivu ya kuuibiwa yalivyomakali itakuwaje hayo ya hg kuwa mke mwenza!kwanza namshauri aombe kwenda kupumzika hata kwao ili apate muda wa kufikiria vizuri juu ya maisha hayo mapya ya kuishi uke wenza ndipo afanye maamuzi japo ndoa yao ni yakufa na kuzikana ila hapo aangalie kile moyo wake unataka,kwan ni lzm atakuwa ameshawachukia hao wanafiki wote na sijui wataishi vp nyumba moja!mmmmh kweli wanawake yanatukuta mengi jaman,mungu tu amsaidie uvumilivu ktk hilo liliompata!
 
Sidhani kama ataendelea kumuamini tena huyo mumewe, kuliko kuishi kwa wasiwasi ni bora kujiengua tu!! I doubt, huo mkwala wa kusema kuwa wameanzia kijijini ni kupunguza soo tu, no wonder ukifungua moyo wa huyo baba utakuta anaombea wife aondoke ili wajinafasi na h'gal!
 
sasa na yule kaka aliyejitambulisha na akasema atamuoa huyo binti wa kazi, ameishia wapi?
Swadakta sis P, I was just trying to figure out why did she bring that poor boy to introduce himself as a father? and where is he now? Huyo binti (beki tatu) na father house wanatakiwa watoe ufafanuzi zaidi.
 
Nakuunga mkono kuwa yule mkaka alikuwa ni wa kupikwa tu. Naomba kuamini kuwa kila kitu alichokuwa analeta alikuwa amepewa na huyo mbaba. So ilikuwa ni deal kabisa iliyochezwa na watu hao watatu. Inawezekana huko nyuma hapakuwa na uhusiano kati ya watu hao lakini baada ya kuoa kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi, huyo mbaba akaanza mahusiano na huyo house girl. Kwa misingi hiyo, huyo mama anatakiwa kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi yoyote. Nafahamu kabisa hili jambo linauma sana lakini linahitaji hekima na maarifa ya ziada juu ya nini kinatakiwa kufanywa na huyu mama. Namshauri apate mapumziko maalum akiwa mbali na watu hawa wawili ili aifanye akili yake itafakari mara mbili tatu juu ya hili tukio.

Huyo mama wala asijihangaishe kumfuatilia huyo mkaka, manake inaonekana baba na h'gal walimtengeneza ili kuficha ukweli...hata hizo nguo na pesa za matumizi yaezekana pia alikuwa anapewa na baba mwenye nyumba... Kuna wanaume wabaya ndugu yangu, mara mia ukutane na simba kuliko kukutana na mwanaume dizaini ya huyo mbaba, unakula nao na wabaya ni hao, hao! Shame on him!
 
sasa na yule kaka aliyejitambulisha na akasema atamuoa huyo binti wa kazi, ameishia wapi?
Hiyo ilikuwa deal tu nadhani ni rafiki wa karibu sana wa jamaa ambaye anafahamu issue nzima. Hahahhaha labda anajiandaa kuwa mshenga au bestman siku ya harusi. Inasikitisha sana kama mtu anaweza kumwumiza mwenzake kiasi hiki. Msichana wa kazi hajamtendea haki mwanamke mwenzake hata kama ni kuficha siri hii imezidi. Mimi ningemshauri huyo mama aondoke tu hapo huyo mwanaume hana mapenzi naye akiendelea kukaa atajutia maisha. Naamini ataweza kujitunza yeye na watoto(baba atoe matunzo kwa watoto) ataweza kumpata mume mwingine ambaye atampenda kwa dhati. Maisha popote.
 
Sidhani kama ataendelea kumuamini tena huyo mumewe, kuliko kuishi kwa wasiwasi ni bora kujiengua tu!! I doubt, huo mkwala wa kusema kuwa wameanzia kijijini ni kupunguza soo tu, no wonder ukifungua moyo wa huyo baba utakuta anaombea wife aondoke ili wajinafasi na h'gal!

na kwanini huyo baba hakumuoa huyo h/girl pale mwanzo.....
kwa sababu alimjua h/girl kabla ya huyo mke wake.......wanaume bana.....
 
Dah huyo kaka alikuwa na lengo gani yarabi? nini kilikuwa nyuma ya pazia? Kwa sababu kama walianzana tangu kijijini inawezekana wazazi wa pande zote mbili walijua na hata alivyochukuliwa kuja kufanyishwa kati mjini si ajabu wazazi wake walijua kuwa kaja kuolewa mwe! Ningewezakusema mengi lakini naona kuna info zinamiss
1. Kama wazazi wake bwana kaka huyu waliafiki ndoa ya jamaa (ndoa ya kwanza)na kumtambua mke kama mke halali wa jamaa
2. Uhusiano wa wazazi wa jamaa na binti wa kazi toka kijinini, familia zao huko kijijini na uhusiano wa jamaa na wazazi wa binti.
3. Mahusiano currently ya huyu bwana kaka na mkewe kabla hajatoa tamko

My take. Inawezekana ilikuwa ni makubaliano ya wazazi (kushurtisha jamaa amuoe binti wa kijijini) bila ridhaa ya kijana na ikabidi kijana akubali kuwaridhisha wazazi but akawa na lake moyoni. Akamgeuza msichana wa kazi ambapo hakuwa na mpango wa kumwoa lakini kwa kuwa ndo hivyo tena ikabidi awe ana'jifaidia' pale anaposhikwa na njaa ..ile ya somba akizidiwa hula hata nyasi. Na bahati mbaya akanogewa akachovya mpaka akatengeneza mtoto akiwa ndoani.....atasema nini zaidi ya kutafuta story na mtu wa kumcover?
Baada ya kuoa mke alomkusudia, akamzalisha na pengine mke akaanza vinyodo au kamchoka tu na akitazama kwa binti wa kijijini adabu na heshima bado imelala plus malezi, hewa ya mjini ah binti kapendeza anafaa kuwa mampsap wake ............kaamua kutoboa siri.

But all in all huyo binti ni msiri aisee.
Aisee kama ni mimi hata sijui nitafanyaje...........
 
Nyodo?? Walitafuta suluhu wapi mambo yakashindikana? Ivi is it possible mwanamke kumfanyia mumewe nyodo alafu ampende h'gal kiasi hicho na kumuachia uhuru wote huo??(may b)! Mwisho wa siku mi nasema ni bora kujiengua. Huyo mwanamke hapendwi, believe me u...! Yaani mwanaume anafikia hatua ya kujilipua kisa h'gal?! Huyo anakuwa ameshajua kabisa reaction itakuwa ni negative na hivo ameshaamua vyovyote na iwe hata uamue kuondoka kwake poa tu! Hata kama mwanamke alianza nyodo h'gal akiwa ameshazaa, mie bado nashawishika kusema hilo lilikuwa limepangwa tu, we unadhani hiyo siri ingetunzwa mpaka lini?? Au kwa nini asingemhamisha huyo h'gal kimya kimya ili awe anaenda kupata faraja kwa uhuru? Jamani akufukuzae hakwambii tokaa...............!
 
na kwanini huyo baba hakumuoa huyo h/girl pale mwanzo.....
kwa sababu alimjua h/girl kabla ya huyo mke wake.......wanaume bana.....

Na ndo maana bado nadoubt huo uhusiano wa h'gal na mume kuwa yawezekana haukuanzia kijijini!! Au labda mwanaume alimtamani huyo house gal huku akiwa keshamchumbia mke hivo hata huko kijijini walikuwa wanafanya kwa wizi na sasa wameamua kujitanua!! Mianaume mingine bana????
 
hapa faida ya kufuata zile kanuni inaonekana......mke angeheshimiwa..lol
 
eeh Mungu wangu,maumivu aliyonayo huyo mke hayaelezeki, Mpe pole sana huyo mke aliyeumizwa kiasi hicho. Cc binadamu tumeumbiwa kila aina ya matatizo, ikitokea haujakutana nalo Basi mshukuru sn Mungu. Huyo mwanaume ni katili na msiri sn, mke awe makini sn kwenye uamuzi wowote atakaouchukua. pole sana Mama Mungu akutie nguvu ktk wakat mgumu huu ktk ndoa yako.
 
duuu,huyo bwana amemfanyia dharau ya mwisho mke wake.na watu wanajua kuwa wasiri,kweli utaendelea kuishi na mume wa aina hiyo?kila siku utaishi kwa wasiwasi.watu watamwambia vumilia,na ndoa iendelee.kwa kweli inauma,mimi nisingeweza
 
Ndio maana huwa sipendi kumuamini mtu kirahisi rahisi hivi, lazima uwe mchunguzi sio unabweteka tu
 
Back
Top Bottom