Ladies kama wewe utachukua hatua gani?

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Salam MMU membaz miss u big T.
Naanza na mkasa unaonishangaza !
Huyu jamaa ,Kabla hajaoa alienda kijijini kwao na kuleta binti mrembo akiwa ni mfanyakazi wake wa ndani
Amekaa nae muda mrefu huku binti akishuhudia pilika za jamaa wakati akileta girlfriends zake Na kufanya utambulisho mzuri tu kuwa ni msichana wake wa kazi na vile vile anamchukulia kama ndugu yake.
Muda wa kuoa ulifika jamaa kaoa na kuleta mke ndani ya nyumba wamekuwa na mahusiano mazuri tu kati ya mke/ mme na binti wa kazi.
Mama mwenye nyumba mungu amemjaalia watoto wawili.
Mara binti wa kazi nae alibeba mimba kisha alimleta jamaa na kumtambulisha kwa dada na shemeji kama ndo baba mwenye ujauzito
walimpokea vyema na kumuuliza nini hatma yao ,jamaa alisema atamuoa mambo yakikaa vizuri
Alienda kwao kujifungua na kukaa miezi sita kisha kurudi kuendelea na ajira yake kama kawaida.
Alifanya vema sana ktk kazi zake za ndani na kumuheshimu sana mke wa jamaa
Mama alimpenda sana na kumchukulia kama ndugu wa mmewe na wake pia,pia baba wa mtoto alikuwa anakuja mara kwa mara kumuona mwanae.
Jamaa baada ya mtoto wa H/G kutimiza miaka 3 Ndipo kaamua kuvunja ukimya kwa kuita ndugu na jamaa kuwatambulisha kwa binti wa kazi
bila kusita alisema huyo binti ana uhusiano nae toka kijijini na hata kabla hamjamuoa wife na mtoto ni wake na ameamua kumuoa kama mke wa pili
Na pia ameshamjengea nyumba anataka kumwamisha………………………
Haya kina mama wenzangumlio kwenye ndoa na mnaotarajia kuingia kama wewe ungechukua maamuzi gani?
Hekima inahitajika hapa …maana mama mwenzetu amechanganyikiwa.
Na nyie baadhi ya akina baba kwa nn mnafanya hivi lakini?
Mbona mnatuumiza sana !
Based on true.
 
Daaah! Kama dini inaruhusu amuoe tu, manake kama wameshapata hadi na mtoto? Ila huo uhusiano wao haujaanzia kijijini. Wameuanza baada ya kuoa.
 
Ni kumsikitikia tu huyo mwanamama. Kuna mrembo aliambia all men are animals..mwanzoni sikumuelewa but with time nimejagundua alichokuwa anasema kina ukweli flani
 
kwanza kabisa huyo mama lazima akubali part of the blame...nasema hivyo kwa sababu she did not do her homework....kabla hujaolewa lazima uhakikishe kuwa kweli huyo jamaa unaifahamu historia yake.

sasa chakufanya ni hivi...kwanza akubaliane na hali aliyojikuta nayo. pili hapa ndoa tena hakuna...mana hakuna trust tena
hivyo basi nivyema atafute divorce.....hii hadithi yakusema oh lakini watoto waototo itakuwaje ni ulimbukeni...sepa becoz ukibaki utaendelea kuwa iserable na hii itaenda hadi kwa watoto.....time to back the bags and leave!!!!!
 
miaka yote hiyo mama hata hakuhisi chochote.................inaumiza sana ufa aliojenga kwenye ndoa yake ni mkubwa hata mke akiamua kuendelea kubaki kwenye hiyo ndoa trust me things will never be the same again!!!!!!!!!
Usijali sitokufanyia hivyo katu hata siku moja
 
Aiseeeeeeee!!
Maskini dada wa watu..mpe pole sana.

Binafsi ningekua kwenye viatu vyake kungekua hamna kuangalia nyuma ila inawezekana yeye akawa tofauti kwahiyo nashauri :Kwanza akajipumzishe mbali na mumewe na huyo mke mwenza mtarajiwa kwa muda afikirie anataka nini.
Baada ya muda atajua kama yuko tayari kusamehe yaliyopita/kuvumilia alichofanyiwa na kuishi maisha ya wake wawili.Na kama ndivyo arudi kwake maisha yasonge.

Kama hatoweza ajiweke vizuri...mazingira ya yeye na wanawe kuishi maisha ya kuridhisha kisha aombe talaka amwachie dada wa kazi nyumba.
 
Mmmh! inauma sanaaaa hasa ukizingatia amemchukua huyu bint kama mdogo wa mumewake kinacho umazaidi nikufanywa mjinga na watu wawili unao waheshimu nakuwathamini,mwambie avute subra najua sio rahisi lakini ajikaze akiwakama mwanamke anatakiwa kua na ustahamilivu,kama dini yao inakubali kuoa mke wapili na yeye yuko tayari na hata kama hayuko tayari kuishi na huyo bwana asiamue kwa sasa.....
 
Daaah! Kama dini inaruhusu amuoe tu, manake kama wameshapata hadi na mtoto? Ila huo uhusiano wao haujaanzia kijijini. Wameuanza baada ya kuoa.

Sweetlady hawa watu ni wakristo ..swala la huu uhusiano hata mie nakosa majibu...
 
miaka yote hiyo mama hata hakuhisi chochote.................inaumiza sana ufa aliojenga kwenye ndoa yake ni mkubwa hata mke akiamua kuendelea kubaki kwenye hiyo ndoa trust me things will never be the same again!!!!!!!!!
Chauro hiki kisa kimenisikitisha sana kila nikiwaza sipati majibu ,hivi unakaa na adui ndani ..mnakula sahani moja bila kujijua mpaka mtu anazaa na mmewe bila kutambua.
 
Back
Top Bottom