valid statement
JF-Expert Member
- Sep 18, 2011
- 2,851
- 868
Kila siku wanaume kwa wanawake wanatoka nje ya mahusiano yao bila kujua au hata kujali sana kitakachotokea ikiwa watafumaniwa/gunduliwa na wenzi wao. Kama baadhi yetu tunavyoimba kila siku kwamba "Cheating is BAD" ndivyo nao wanavyoimba kwamba "Cheating is NECESSARY/INEVITABLE". Wanatoka nje ya mahusiano yao bila kufikiria wala kujali matokeo yake kwao binafsi, watoto kama wanao na wenzi wao kwa visingizio vya "nature haikubali niwe na mwanamke mmoja, mume/mke wangu haniridhishi/ mwenzangu hanijali/umbali ndio chanzo n.k"
Matokeo mabaya ya kucheat ni pamoja na kumuumiza mwenzi, kupeleka magonjwa (ya moyo/kiakili na kimwili kwa ujumla) kwa aliyetulia nyumbani, kuzaa mtoto ambae anaweza asikubaliwe na mwenzi hata kuishia kunyanyaswa, kuwakosesha watoto malezi wanayostahili, mahusiano/ndoa kuvunjika na kubwa zaidi ambalo sidhani kama watu hua wanalifikiria sana. . . nalo ni kuuwawa au hata kuumizwa sana pale atakapokamatwa.
Hizi kesi ambazo mtuhumiwa anakua amefanya kosa (laweza kuwa ni la kuua, kubaka au kumpiga hata kumuumiza mwenzake) kutokana na hisia kali sana za mapenzi au hasira baada ya kufumania huitwa Crimes of passion. Je na wewe uko tayari kuwa victim wa hili baada ya kumfanya mwenzio victim wa kudanganywa?
Mwaka jana tu tulisikia hapa kwetu mwanaume alichomwa kisu na mwanamke wake wa nje baada ya kugundua kwamba hakua mwenyewe, kuna mama wa kiMarekani (Clara Harris ukipenda kumgoogle) yeye alimgonga mume wake kwa gari mara kadhaa baada ya kumkuta hotelini na mwanamke mwingine, Zimbabwe kuna mwanaume alimchoma mke kisu. . akachinja mtoto mwenye umri wa siku mbili ambae alikua wa mwanaume mwingine kabla nae hajajitundika.
Haya ni madhara makubwa zaidi tofauti ya yale tuliyozea/wahusika wanayotegemea kwasababu yanahusu kuondoa maisha ya mtu au hata watu. Je wewe unadhani hicho unachopata huko nje ya ndoa/mahusiano yako kina thamani sawa na maisha yako wewe au ya mtu mwingine yeyote yule? Kama kina thamani kiasi hicho kwanini usiachane na maisha uliyonayo ukaenda kuanza upya huko unakopata hicho/hayo yaliyo muhimu zaidi?
Binafsi napinga sana kitendo cha mtu kutoka nje ya mahusiano yake kwa sababu yoyote ile. . tena baada ya kushuhudia mtu ambae alijitahidi kuwa mke mtulivu akiletewa UKIMWI nyumbani kwake, ugonjwa ambao unaweza ukafupisha maisha yake nashindwa kabisa kuelewa ni vipi mtu anaweza akawa mbinafsi hata kupitiliza. Jioneeni huruma, waoneeni wake/waume/wapenzi/watoto na ndugu zenu huruma. Ukiona mambo yamekufika shingoni, nyumbani hakukaliki jiweke huru. Maana kwa kutaka kuendelea kuwepo huko na bado uwepo kule kunaweza kukakufanya wewe usiwe tofauti na mtu muuaji.
Cheating is a very selfish act. . . JALI, CHUKUA HATUA!
Lizzy
Umeongea vizuri