La katiba nawapa credit tuongozeni tena kudai Tanganyika...

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Ni ukweli usiopingika Chadema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye suala la katiba, ingawa mchakato bado uko kwenye hatua za mwanzo lakini jitihada zao zimeonekana hakuna mtu atabisha kuwa bila wao tusingekuwa hapa leo, hii imezidisha imani ya watu kwao na kukomaa kwao katika masuala ya kitaifa kabla hawajawakabidhi nchi.

Kwa hiyo basi, kwa nguvu ile ile na mapenzi yale yale waliyotumia kufanikisha hilo naomba waanze kupiga kelele tena kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika Insallah watafanikiwa. Msiogope sera yenu kutekwa na wapinzani wenu kama walivyoteka sera ya katiba kwa vile mwisho wa siku watakaofaidika ni wananchi wote wa Tanzania kama tukavyofaidika na kuanzishwa kwa katiba mpya.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom