Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba

Habari zenu wapendwa... naombeni msaada wa dawa ya kwikwi kwa mtoto mchanga wa wiki tatu.wiki ya pili sasa anateseka na kwikwi yaan ni kila siku mpaka analegea mwili. naombeni mnisaidie ameenda hospital lakini tatizo bado linaendelea.. hata dawa ya asili pia naomben mnielekeze jamani. AHSANTENI
 
Chukua uzi mdogo wa nguo aliyovaa weka mdomon ukiloa muwekee juu ya paji la uso
 
Shida ya kwikwi inatokana kumpa maziwa yaliokwisha kuwa ya baridi sana au ni yamoto kwa unywaji wa mtoto..jaribu kumpa maziwa ya uvuguvugu kabla ya kumpa jaribu kudondosha kwenye ngozi ya mkono wako kutest usijaribu kwa kushika chupa..jaribu kuepuka kumpa maziwa ya baridi au ya moto.na wala usije ukampa dawa yoyote ile mtoto kwa kipindi hiki.kisha uje unipe majibu kuanzia leo.
 
Mkuu kipozi anafanyiwa hvo lkn haisaidii...

Mkuu @jamii001 mtoti ajaanza kunywa maziwa ya kopo, ana wiki ya tatu tangu azaliwe.. na hyo kwikwi imeanza akiwa na wiki mbili toka kuzaliwa kwake.. yaan ni kila siku hadi inaogopesha.
 
Shida ya kwikwi inatokana kumpa maziwa yaliokwisha kuwa ya baridi sana au ni yamoto kwa unywaji wa mtoto..jaribu kumpa maziwa ya uvuguvugu kabla ya kumpa jaribu kudondosha kwenye ngozi ya mkono wako kutest usijaribu kwa kushika chupa..jaribu kuepuka kumpa maziwa ya baridi au ya moto.na wala usije ukampa dawa yoyote ile mtoto kwa kipindi hiki.kisha uje unipe majibu kuanzia leo.

maziwa ya moto? kwani si ananyonya kwa mama yake?
 
Kwanza maana ya kwikwi, ni kujaa kwa hewa tumboni ni hewa tu ipo tumboni hakuna dawa ya asili wala kisayansi jibbu ni kwamba ananyonya hewa ni si maziwa ndo maana inajaa, swali una maziwa ya kutosha? itakua maziwa yako si ya kutosha ndo maana anameza hewa.... jitahidi kwenye maziwa, na usimpe mtoto kile kinyonyo cha plastic kwani kinamuongezea hewa tumboni
 
Wakati wakunyonyesha, mama ahakikishe chuchu inajaa mdomoni kwa mtoto bila kuacha nafasi ili hewa isipite.

Mtoto akimaliza kunyonya abebwe kwa kulazwa begani na kupigwapigwa (sio kwanguvu) mgongoni hadi abeue,. Hili tukio lifanyike hata kwa nusu saa bila kuchoka.
 
Pia mama anapomnyonyesha mtoto ahakikishe amemweka position sawasawa, isije ikawa mtoto chuchu haikai vizuri hewa unaingia mdomoni mwa mtoto. Mama awe very attentive chuchu na mdomo wa mtoto vinavyokuwa positioned.
 
Basi akimaliza kunyonya ameweke begani kwake kwa dkt 5 akiwa anamgonga mgongoni kusaidia maziwa kushika tumboni asikimbilie kumlaza au kumbemba kwa namna yoyote nyingine ile kisha uje unipe majibu..mtoto wangu alikuwa anashida kama hizo pia so nakwambia kwa uzoefu wangu mdongo
 
ok. thank you
 
Na ushauri niliopata ni kumuekea kauzi kwenye paji la uso .

Eenye uzoefu Tafadhari na masuala haya.
 
ni Leo tu baada ya chakula cha usiku

Amemeza hewa nyingi wakati wa kula/kunyonya au ameshiba kupitiliza(mmemshindilia chakula kupita uwezo wa tumbo lake) cha kufanya mlambishe sukari nusu kijiko cha chai au msimamishe kichwa chini miguu juu kwa dk 1 au mtekenye ssna mpk acheke au mlaze alalie upande wa kushoto ukibonyeza taratibu sehemu ya chembe ya moyo. Mojawapo litatoa majibu. Gnight nitaomba mrejesho pse
 
asante mkuu cc Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom