Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

muwa aina hii unapatikana wapi jamani? mie kwikwi ni tatizo langu la muda mrefu...



Muwa Mweusi Black Sugarcane Mkuu King'asti


stock-photo-black-sugarcane-isolated-on-white-54141133.jpg

Black Sugarcane
naona Unesi utakushinda lol
 
bibi yangu alikuwa akinichanganyia kijiko kimoja cha jivu na maji ya uvuguvugu glass moja kisha ananipa nakunywa safi kabisa
wakati mwingine kifua kikinibana na kwikwi alikuwa akinichanganyia magadi kwenye glass ya maji ya uvuguvugu na kuninywesha
 
wakati wa kula, hasa vyakula vikavu, kwa hiyo siku zote naepuka vyakula vikavu vikavu, hata wali lazima uwe na mchuzi wa kutosha ndo nile....
Mkuu, vyakula karibu vyote haviwezi kumeng'enywa mwilini bila maji, unapokaribia kula chakula kigumu mfano viazi au mkate hivi, mwili hutambuwa kuna kumeng'enya chakula hicho kutahitaji maji mengi zaidi na unajuwa sisi hatunywi maji mpaka tusikie kiu. Dawa yake ni kuchukuwa tu glasi ya maji ya kawaida (siyo ya kwenye friji) na kunywa, mhimu kumbuka kila nusu saa kabla ya kula chakula unakunywa maji glasi 2 (ml 500). Ni hivyo tu. Mwili unakuwa unakuambia kuwa ili chakula hicho unachoenda kula kitumike vizuri na mwili, unahitaji kutanguliza maji. Basi.
 
Na dawa nyingine ni hii chukua kijiko kimoja cha sukari weka chini ya ulimi na kwa kitendo hicho kitafanya maji maji mengi mdomoni wewe meza hayo maji mpaka sukari itakapoyeyuka yote kwikwi itakuwa imekwisha
 
Nimetumia dawa ya mua mweusi na asali mbichi, niliyoshauriwa na Mzizimkavu kwa kweli ni dawa maridadi
Jamani tumtumie Doctor huyu kwa ushauri na mapendekezo ya dawa anayotoa..Asante Dr. I real appreciate!!!
:israel:
Mkuu daniel don Asante kwa kutoa Feedback ninakutakia afya njema na uzima na kila kheri inshallah.Ni Watu wachache sana kama wewe wanaotoa Feedback nimefurahi kwa feedback yako asante.Ubarikiwe mbinguni.
 
kuhusu hili suala la kwikwi, nakushauri uende hospitali upewe dawa. Ikumbukwe kwamba zipo kwikwi za presha. Kwikwi hizi huchukua siku nzima bila kuisha, hivyo ni vema uende hospitali ukapime presha na wakupe dawa ya kukata hiyo kwikwi. Hili tatizo lilimpata mzazi wangu, alikuwa ana presha na aliandikiwa dawa. Baada ya kumeza hizo dawa kwikwi iliisha, na haikumpata tena mpaka leo hii.
 
jamani naomba kufahamishwa tatizo la kwikwi kwa mtu mzima linatokana na nini? Nini athari zake? je kuna matibabu ya kwikwi?
 
Back
Top Bottom