Kwetu ni pazuri, karibuni

Barraza

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
481
270
Huu wimbo ni mzuri sana kuusikiliza, kuna mtu aliniambia kuwa asilimia kubwa ya waimbaji wa huu wimbo walifariki kwenye ajali, eti ni kweli?



"Nyumbani kwetu hakuna Masaburi, wala hakuna maleria wala hakuna vyandarua"

Nawatakia week end njema ndugu zangu.
 
Last edited by a moderator:
kwa wanaoujua huu wimbo... Kwa waloona hapo!
Wote mtakubali umetulia huu wimbo. Ni mtamu. Hata bar unapigwagwa achilia kwenye basi.
 
Yani ndio nipo nausikiza hapa!! nadhani ni watatu tu ndio waliokufa kwenye ajali.
 
hapana waliokufa ni watatu tu wanyarwanda wawili na mtanzania mmoja raia wa kigoma anaitwa amos tafuta cd yao ya nne utawaona
 
Huu wimbo unafariji sana. Kwaya zetu zingekuwa zina utaratibu wa uimbaji huu watu wengi wangeokolewa.Waimbaji wengi wa muziki wa injili Tz. wamegeuza muziki wa injili ni biashara kelele, mavazi ya ovyo, uchezaji kama wapo baa ni ghasia tupu. Ambassadors for Christ mmbarikiwe sana.
 
pia watakuwa mwanza mwakani kwenye makambi ya kanisa l wasabato kirumba
 
Huu wimbo ni mzuri sana kuusikiliza, kuna mtu aliniambia kuwa asilimia kubwa ya waimbaji wa huu wimbo walifariki kwenye ajali, eti ni kweli?



"Nyumbani kwetu hakuna Masaburi, wala hakuna maleria wala hakuna vyandarua"

Nawatakia week end njema ndugu zangu.


dah! masaburi hayapo vp kuhusiana na mambo ya cameron!
 
Last edited by a moderator:
kwa kweli nyimbo zao nazipenda sana. Kuna mwingine unaitwa Ambassador of Christ tunashukuru nao mzuri.
 
Ni kweli wimbo mtamu sana. Ukitaka zingine unaweza kupata kwenye; YOUTUBE- AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR; RUMERA SDA CHOIR.
 
asee hawa jamaa hua nawapenda sana.... yani kariakoo siku hizi kila kona unausikia huu wimbo na hua nikiusikia bado ninakua na furaha ile ile yani
 
Back
Top Bottom