Kwenye swala la mapenzi wanaume hawana mzaha...!

Last edited by a moderator:
Mtambuzi issue siyo uhaba bali ni kile unachokipata kutoka kwa huyo mwanamke (mambo fulani)
kinachouma zaidi ni pale unapokumbuka anavyokudenda na kukulalamikia kwa maneno matamu ya mahaba...unafikiri ndivyo alivyo fanya hata kwa mgoni wako..dah lazime mtu ashikishwe adabu.

Lakini pia hii kitu ni cultural orientation ndani ya jamii hasa jamii za kiafrika (Sijui za wenzetu)...Mwanamke/wanawake ni wa Mwanaume (mmoja), Mwanaume ni wa mwanamke/wanawake!

hii ya kujitoa roho pengine ni kwa wale watu ambao self esteem (Nafsi tukuka) zao ziko low sana!


"..Hivi kumekuwa na uhaba wa wanawake kiasi cha kupelekea baadhi ya wanaume kuhatarisha maisha yao au kupoteza maisha kutokana na kumgombea huyu kiumbe mwanamke au kuna kitu kingine kinachotafutwa hapo?"
 

Ni aghalabu sana kusikia mwanamke kamuua mume baada ya kumfumania au kumuua mgoni wake tofauti na wanaume. Kama ukipima jambo hilo kitakwimu basi utapata idadi ya wanaume ya kutosha ukilinganisha na ile ya wanawake. Kimsingi wanaume wamewageuza wanawake kama mali zao wanazozimiliki na hiyo ndio sababu inapotokea kumfumania mkewe au mchumba wake akiwa na mwanaume mwingine mambo mawili yanaweza kutokea, kwanza atamuadhibu mgoni wake au hata kumuua kisha mke naye atasulubiwa au hata kuuawa.

Lakini, pale anapofumaniwa mwanaume mambo huwa ni tofauti sana. Kuna uwezekano mkubwa wa mke huyo kusulubiwa kwa sababu amemfumania mume na wakati mwingine hata huyo mgoni anaweza kushirikiana na mume huyu kumuadhibu huyo mwanamke aliyefumania.Nadhani kuna haja ya wanaume kujikagua upya na kubadili mwenendo wao mzima juu ya matendo yao ili kuepuka kupoteza maisha kwa jambo ambalo wangeweza kuliepuka.

Ni kweli Mtambuzi unayosema ila hapo nilipo-bold nadhani ulikuwa unamaanisha Nadra ambayo maana yake ni mara chache na aghalabu ni kinyume chake yaani mara nyingi. Nadhani kiswahili changu cha huku kijijini Maligisu nitakuwa sijakosea!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli Mtambuzi unayosema ila hapo nilipo-bold nadhani ulikuwa unamaanisha Nadra ambayo maana yake ni mara chache na aghalabu ni kinyume chake yaani mara nyingi. Nadhani kiswahili changu cha huku kijijini Maligisu nitakuwa sijakosea!

Hebu ngoja nipekue kamusi yangu kwanza, nitakuja na jibu....
 
Yeah uko sahihi, nilitakiwa niseme 'Si aghalabu"

Ni kweli huwa inachanganya sana kwa watu wengi japokuwa watu huelewa bila kujua kama umekosea (kwenye kithungu huwa kuna common mistake in english na lugha yetu ya kimatumbi huwa kuna vitu kama hivi ambavyo mara nyingi huwa tunavizoea kutokana na waliotutangulia ktumia hivyo na mwisho wa siku tunazoea). Asante kwa kuchukua muda wa kuperuzi kamusi
 
Back
Top Bottom