Kwenu kina dada: Mavazi yepi mwapenda wenzenu wavae

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,320
17,822
Wakuu,,

Tukiendelea na hili libeneke la mahusiano ma mapenzi, kuna kitu kimenijia akilini, nacho ni:

Linapokuja suala la mavazi na muonekano wa mpenzi/mume wako, ungependa avaeje/aonekaneje mtokapo au hata muwapo nyumbani?

Tukiacha suala la mazingira na hali ya hewa pembeni, kuna wengine kwa mfano wangependa mtu anayepigilia viwalo vya kisasa, wengine wangependa mitindo ya zamani kama nywele za afro, visuruali vya 'chinjio' au wengine 'mabagi',

ukija kwen viatu, labda wengine wanapenda vya kileo, vilivyopo kwenye fasheni na vyenye majina (mf. kama raba za puma, nike, adidas -original sio hizi za 'kwa mtogole)

Kuna wengine wanapenda wapenzi wao wawe na vidani..kama cheni, kidani cha mkononi, au hata hereni kabisa,,

Sasa sijui kwa ujumla mnapenda mmwenzi wako aonekaneje..ukitilia maanani jamii na pia your own satisfaction.

hata sijui kama nimeeleweka lakini hivyo hivyo.
 
1. Awe smart asizidishe sana.
2. Sipendi anayevaa macheni cheni au wenyewe mwaita mabling bling!
3. Awe na nywele fupi za wastani- sipendi kama ananywele anyoe kipara kile kinachong'aa hapana.
4. Avae mavazi yanayoendana na umri wake si ukuta mbaba wa miaka 45 anavaa masuruali yenye mamifuko makubwa au t-shirts zenye macharter makubwa.
5. Kifupi avae kulingana na umri wake.
6. Hata gari asiwe anafungulia mziki mkubwa hadi wa nje wanasikia mh!
 
Hiyo ya kwanza imeniacha hoi MJ1,, kuzidisha inakuwaje tena....lol

hapo kwenye muziki wa kwenye gari.....najua wengi hampendelei sauti kubwa lakini kama gari yenyewe mziki ni mkubwa jamani.....:rolleyes:
 
Akishindwa kufungua mziki kwa sauti ndogo basi akiweka sauti kubwa afunge vioo kuusikiliza mwenyewe humo ndani ya gari kuliko kupita barabarani na makelele.

@ Uvaaji
Wanaume uvaaji wao haupo complicated kama wanawake, kwahiyo ni rahisi hata mwanaume kujipangia vizuri kuvaa na akawa amelipuka...Uvaaji uendane na mazingira kama kazini,sherehe weekend au sports nk.
Mfano: Siyo t-shirt ya voda unavaa kwenye harusi.
 
Ah Kaizer kaka yangu si unajua mwingine aweza vaa yaani akawa havutii tena. Utakuta kavaa msuti wakati anatembea barabarani na jua kaaali jasho lamtiririka huyo ni msmart but amezidisha. Au perfume amepulizia ni kali kuliko ya binti hapana bwana.

Kuna wale wanatembea na vitana mifukoni- hawa ni smart but kukitoa na kuchana barabarani ni kuzidisha kaka yangu. Mi spendi!

Gari sawa mziki mkubwa but mh sikiza mwenyewe basi. Au angalau uwe na rika lile la ki hip hop (ningesema ki yo yooo man msijesema namsema rafiki yangu Yo Yo bure). Sasa utakuta baba na mvi kibao mziki huo afu bora sasa ungekuwa wa rika lake hapanaaaa kina wanaume TMK au wale wanao sijui ni kuimba au kufoka ah!
 
Wow..karibu tena Belly!

Hapo nimekusoma, naona umeegemea zaidi kwenye mazingira,, mi niulize mfano wakati wa weekend.....unapenda atokeje (kama hakuna harusi of which tshirt ya voda ni marufuku)
 
Hapo umenikumbusha mwalimu wangu wa zamani (RIP)! LOL

Kuna wale wanatembea na vitana mifukoni- hawa ni smart but kukitoa na kuchana barabarani ni kuzidisha kaka yangu. Mi spendi!

hapa nakubaliana na wewe imezidi hii!

Gari sawa mziki mkubwa but mh sikiza mwenyewe basi. Au angalau uwe na rika lile la ki hip hop (ningesema ki yo yooo man msijesema namsema rafiki yangu Yo Yo bure). Sasa utakuta baba na mvi kibao mziki huo afu bora sasa ungekuwa wa rika lake hapanaaaa kina wanaume TMK au wale wanao sijui ni kuimba au kufoka ah!

LOL..sasa hapa kasheshe...kuna wazee wa 'kimjini mjini' hapo huwatoi,, na sijui kwa wenzetu wengine wana maconvertible hali ya hewa ikiruhusu tu unamkuta mzee na mvi zake (labda vijana hali ya uchumi inakuwa ngumu kuwa na mgarai ya ki hivyo) lakini kuna wazee wanahusudu sana mambo ya kileo,, nadhani wa hivo kwako atakuwa amegonga mwamba!
 
Wow..karibu tena Belly!

Hapo nimekusoma, naona umeegemea zaidi kwenye mazingira,, mi niulize mfano wakati wa weekend.....unapenda atokeje (kama hakuna harusi of which tshirt ya voda ni marufuku)

Asante Kaizer, nimerudi tena!..

Wakati wa weekend anaweza akavaa bukta/suruali na t-shirt (casual) pia viatu vya wazi miguu ipate hewa maana kila siku kazini viatu vya kufunika..
Unless weekend anaenda kazini basi avae kikazini(inategemea na ofisi mmaana wengine weekend wanavaa t-shirt) au akihudhuria nyumba ya ibada iwe ijumaa/jmosi/j2 basi avae kulingana na mazingira ya eneo..
 
Then najiita mwenye bahati wangu huwa anapenda nimchagulie mie cha kuvaaa kila siku kuanzia office ,casual mpaka sports wear, but kunogesha mambo huwa namuomba awe huru kusema anachojiskia ,unajua kuna siku mtu unakuwa umeikumbuka nguo flani na una hamu nayo basi huwa ananambia na mie namridhia,mapenzi kusikilizwa na kusikiliza wajameeni.
 
hapo mummy tuko pamojaaaaaaaaaa...... plus its ma hobby kumfanyia shopping here en there!!
 
Then najiita mwenye bahati wangu huwa anapenda nimchagulie mie cha kuvaaa kila siku kuanzia office ,casual mpaka sports wear, but kunogesha mambo huwa namuomba awe huru kusema anachojiskia ,unajua kuna siku mtu unakuwa umeikumbuka nguo flani na una hamu nayo basi huwa ananambia na mie namridhia,mapenzi kusikilizwa na kusikiliza wajameeni.

hii nimeipenda,,vipi kuhusu vikolombwezo vingine?
 
Napenda avae mavazi anayopenda avae
Akivaa na kutopendeza sintokuwa naye
Kumwambia cha kuvaa ni utumi shume
Hata hilo kujadili ni mfumo dume
Ikibidi nimwambie wazi hajafundwa
Na mie sitaki ambaye hajakungwa
 
Ah Kaizer kaka yangu si unajua mwingine aweza vaa yaani akawa havutii tena. Utakuta kavaa msuti wakati anatembea barabarani na jua kaaali jasho lamtiririka huyo ni msmart but amezidisha. Au perfume amepulizia ni kali kuliko ya binti hapana bwana.

Kuna wale wanatembea na vitana mifukoni- hawa ni smart but kukitoa na kuchana barabarani ni kuzidisha kaka yangu. Mi spendi!

Gari sawa mziki mkubwa but mh sikiza mwenyewe basi. Au angalau uwe na rika lile la ki hip hop (ningesema ki yo yooo man msijesema namsema rafiki yangu Yo Yo bure). Sasa utakuta baba na mvi kibao mziki huo afu bora sasa ungekuwa wa rika lake hapanaaaa kina wanaume TMK au wale wanao sijui ni kuimba au kufoka ah!

Poa nimekupata Mkuu. Huwa nachania washrooms. Mwanaume ni Kuchana nywele na kupiga kiwi kiatu kung'aa kwa kwenda mbele.
 
babalynn
Kacheni kamoja ka kawaida akikavaa kistaarabu sawa- sio yale makuuubwa ka mnyororo wa mbwa.

mami umenifurahisha hapo....napenda aonekane smart! pete ni moja tu aliyoyonayo ya ndoa, cheni ya kawaida tu! jmoc na jpili baada ya kanisa anaweza kuvaa jeans,tshit, na viatu vya wazi, kaptula pia, yaani aonekane cmple but sure.
 
Then najiita mwenye bahati wangu huwa anapenda nimchagulie mie cha kuvaaa kila siku kuanzia office ,casual mpaka sports wear, but kunogesha mambo huwa namuomba awe huru kusema anachojiskia ,unajua kuna siku mtu unakuwa umeikumbuka nguo flani na una hamu nayo basi huwa ananambia na mie namridhia,mapenzi kusikilizwa na kusikiliza wajameeni.

mnh, wenye wake na mashori kumbe mwafaidi namna hii?, duh
naungana na yo yo, GOAL 2010: KUSAKA SHORI
 
Back
Top Bottom