Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
Yeah hii mara kibao inatokea mkazoeana na dada wewe ukajua pengine anataka penzi kumbe sivyo wazo lake yeye anahitaji kampani tu alafu mnaweza mkalala hata chumba kimoja na usimfanye kitu ukaishia kutoa udenda mdomoni.
ha ha haaaaaaaa, Fidel80 hapa umenikumbusha siku moja kuna rafiki yangu alikuja kunitembelea. si unajua kampasi mambo ya chumba kimoja tu? tukapiga story, mara mvua kubwa sana ikaanza. ilinyesha mpaka usiku sana, ikabidi yule kaka alale pale. sikuwa na wasi sababu tulikuwa so close, tukapiga story mpaka nikapitiwa na usingizi. mwenye nyumba nimepiga usingizi mpaka asubuhi, kumbe jamaa hajalala. kuamka asubuhi nashangaa mgeni kachoka, nikamwuliza kulikoni mbona upo hoi? au kitanda kidogo sana umeshindwa kulala? akaniambia hakuweza kupata usingizi. Nikamshangaa sana