Kweli watanzania wamepoteza maadili na utu?

Global Publisher nadhani mnastahili kusoma hii kwa umakini.

Tabia yenu ya kuchapisha picha za watu waiopatwa na umauti katika ajali mbalimbali inachefua na inaondosha kabisa misingi ya Utu.

Umeongea vema ndugu yangu. Hawa jamaa wa global publishers siku zote huwa wananiboa sana kwa mipicha yao ya hovyohovyo. Mara wapige picha za uchi na mara hizo za waliokutana na mauti tena wanaweka kwenye kurasa za mbele. Hawa jamaa ni waandishi wa kusomea au ni makanjanja fulani?
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Watu wanapopata ajali na kuumia au kuangamia katika ajali hizo sisi tulio hai na tunaofanikiwa kufika kwanza katika eneo la ajali tuna jukumu la pekee la kuwaokoa walionusurika na kuhakikisha wako salama na kuwaepusha na majanga zaidi. Lakini zaidi sana tunalo jukumu la kimaadili la kuwahifadhi na kuwasitiri ubinadamu na utu wao wale ambao wamefariki katika ajali hizo badala ya kuanza kuwapiga picha katika saa ya mauti yao na kuzisambaza kama vile ni udaku.

Kinyume na hili kwa muda sasa jamii yetu imekubali na kuanza kuvumilia vitendo vya kukufuru miili ya marehemu kwa kupiga picha miili iliyopondwa na kuvunjika katika ajali kwa ajili ya aina fulani ya burudani na udadisi wa macho. Makala hii ni nzito* na ina lengo la kugusa dhamira; kuendelea kuisoma kunaweza kukuumiza hisia, kukupa mashaka na kukuondolea hamu ya chakula na kukupa wasiwasi. Tafadhali soma kwa tahadhari. (Wahariri wanaruhusiwa kuitumia jinsi ilivyo bila kubadilisha jina la mtunzi na kuhakikisha barua pepe mwishoni mwa makala inatokea).

* Natamani ninayoandika kwenye makala hii yangesemwa kwa namna fulani na viongozi wetu wa juu wa serikali au dini. Ni mzigo mkubwa kwangu.

mwanakijiji asante sana, kuna siku huwa natafakari na kuumia sana hasa nikiwa pale mwenge karibu na jirani yangu shigongo na kujiuliza maswali kama vile
hivi angekua mamake mza angemuacha tumuone na chupi tu au sehemu za marehemu za setiri?
je tungeweza kumuona mkewe akiwa katika hali ya kuvunjika mgongo na kiuno na damu imetapakaa?
angekua babake mzazi, tungeweza kuona chupi yake na kitovu chake?

its a high time tukumbuke usetiri wa binadamu hauishii kwenye uhai na ndio maana kuna majeneza, kuosha maiti na kupamba maiti pia

ninamuomba mungu atufundishe kwa vitendo haya tunayoyashuhudia na ningependa sana siku moja huyo mpiga picha au eric mwenyewe ashuhudie inavyotutesa na kutukumbusha madili
 
wana JF nao hawako nyuma kwa kuweka picha za marehemu.....humu ndani kulikua na picha za marehemu wa ajali ya Kibamba zimezagaa.
 
Inasikitisha lakini ndio maana halisi ya habari na Teknolojia. Huwezi kusema Kwenye TV watangaze kama Radio au magazeti yapige picha za black and white kwa kuwa tu picha zinatisha. That is news we need to see and feel it.

Wala tusingekuwa tujadili hii mada na hata za ajali yenyewe kwa hisia za kuguswa kama tusinegeona yaliyotokea.
 
kwa hiyo kama ndugu yako amepata ajali usingependa asitiriwe utu wake ila watu waende kumpiga picha uili uweze kuona ili hatimaye uweze kuguswa na hiyo ajali?
 
Unaona sasa....hapo ndipo unapokosea....huyo uliyemtaja atatufundishaje?

sorry NN, maybe nimetumia lugha kali au mbaya... maana yangu ni kwamba huyo mpiga picha na huyo anayeziruhusu kwenda gazetini siku akija kukuta ni ***** au mkewe au mumewe au mwanawe yuko front page akiwa ameharibika kwa ajali, nina imani atatuelewa zaidi kwani atakua amejifunza kwa vitendo
 
Viongozi wetu wako kama actors, wanaachia maadili (ethics) za kikazi ziwe abused, maana hata Marehemu Salome Mbatia walitoa picha lkn hakuna aliyekemea, sijui baraza la habari lafanya shughuri gani?napata kigugumizi
 
hapa kuna na suala jengine la mtu kushtaki kwa kosa la kubakwa, na akabandikwa picha zake kwenye blog.
au mtu anapiga tu picha ya mtoto wako akiwa katika hali mbaya ya ugonjwa bila ya ridhaa yako.

hiyo ya kupigwa picha maiti kwenye ajali imeshazoweleka sana kiasi cha kwamba wengine wataona ajabu kuambiwa wasipige
 
Tangu nimeona zile picha naogopa kusafiri sana....na ninaogopa picha za aina yeyote ile zenye wekundu yaani kuashiria damu. Hata hapa JF kuna AVATAR 2 nikiziona nashtuka sana na relate na ile picha. Moja mtu ananyofolewa tumbo lake na nyingine mtu yuko ****** akapasuka kichwa kweli nimeathirika sana na sio utani.
 
Hata mimi huwa inanishangaza sana hii.Kuna siku nilikuwa ninasafiri na mheshimiwa fulani tukakuta ajali njiani kilichonishangaza tulipofika tu eneo la tukio mheshimiwa huyu alianza kupiga picha na kutoa maelekezo kwa wengine kwamba washughulikie miili ya wahanga,yeye akiwa bize kupiga picha.Kilichofuata alizituma picha zile kwa waandishi wa habari ili watoe stori kesho yake.Nilishangaa sana,picha kwanza msaada baadaye.
 
Kwa kweli MM inasikitisha sana huu ukosefu wa maadil. Hata TV zetu zinaonyesha picha za maiti hadharani bila kujali kuwa hata watoto wanaangalia. Mfano ajali iliyotokea brbr Mogoro juzi na kuua watu wote kwenye mini bus, picha zilirushwa hewani kama za wanyama.

Wakati mwingine nafikiri kuwa utu umetutoka na tumeelekea kweunyama zaidi. Kama mtu anasagura majeruhi hela yake wakati anapambana na uhai au anasachi maiti kama vile yeye hajui kufa unafikiri nii hali ya kawaida?
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Watu wanapopata ajali na kuumia au kuangamia katika ajali hizo sisi tulio hai na tunaofanikiwa kufika kwanza katika eneo la ajali tuna jukumu la pekee la kuwaokoa walionusurika na kuhakikisha wako salama na kuwaepusha na majanga zaidi. Lakini zaidi sana tunalo jukumu la kimaadili la kuwahifadhi na kuwasitiri ubinadamu na utu wao wale ambao wamefariki katika ajali hizo badala ya kuanza kuwapiga picha katika saa ya mauti yao na kuzisambaza kama vile ni udaku.

Kinyume na hili kwa muda sasa jamii yetu imekubali na kuanza kuvumilia vitendo vya kukufuru miili ya marehemu kwa kupiga picha miili iliyopondwa na kuvunjika katika ajali kwa ajili ya aina fulani ya burudani na udadisi wa macho. Makala hii ni nzito* na ina lengo la kugusa dhamira; kuendelea kuisoma kunaweza kukuumiza hisia, kukupa mashaka na kukuondolea hamu ya chakula na kukupa wasiwasi. Tafadhali soma kwa tahadhari. (Wahariri wanaruhusiwa kuitumia jinsi ilivyo bila kubadilisha jina la mtunzi na kuhakikisha barua pepe mwishoni mwa makala inatokea).

* Natamani ninayoandika kwenye makala hii yangesemwa kwa namna fulani na viongozi wetu wa juu wa serikali au dini. Ni mzigo mkubwa kwangu.

Najua kuna watu wameguswa leo na matukio ya usambazaji wa picha za marehemu; nimeona nilirudie hili kusaidia hasa viongozi na watu wazima kutafakari kidogo.
 
Hata mimi huwa inanishangaza sana hii.Kuna siku nilikuwa ninasafiri na mheshimiwa fulani tukakuta ajali njiani kilichonishangaza tulipofika tu eneo la tukio mheshimiwa huyu alianza kupiga picha na kutoa maelekezo kwa wengine kwamba washughulikie miili ya wahanga,yeye akiwa bize kupiga picha.Kilichofuata alizituma picha zile kwa waandishi wa habari ili watoe stori kesho yake.Nilishangaa sana,picha kwanza msaada baadaye.

Duh maneno haya; maneno haya yanatusuta leo! RIP Regia
 
Najua kuna watu wameguswa leo na matukio ya usambazaji wa picha za marehemu; nimeona nilirudie hili kusaidia hasa viongozi na watu wazima kutafakari kidogo.
Safari yetu ya kuelekea kwenye mmomonyoko kimaadili ilianza zamani kidogo... I think kuna haha ya a few people kushughulikiwa na kuwa mfano
 
Back
Top Bottom