Kweli waTanzania wamechoka. Nchi imemwagiwa petroli. (MWANZA)

Siku 9 za kishindo zatangazwa
headline_bullet.jpg
Polisi wa Mwanza wafagiliwa

Main(65).jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akiwahutubia maelfu ya wananchi walioshiriki maandamano ya chama hicho ya kupinga mfumuko wa bei na malipo ya Dowans yaliyofanyika jijini Mwanza jana.



Maelfu ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walifanya maandamano ya amani yaliyoongozwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ambayo yalikuwa na msisimko mkubwa bila ya vurugu yoyote.
Maandamano hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kutoilipa Kampuni ya Dowans, kupanda kwa bei ya umeme na kutokubali uchaguzi uliomweka madarakani meya wa Jiji la Arusha. Maandamano hayo yaliyoongozwa na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilibrod Slaa na wabunge karibu wote wa chama hicho kutoka karibu majimbo yote Tanzania, yalianzia katika viwanja vya shule ya msingi Bugarika na kumalizikia katika viwanja vya Furahisha jijini hapa ikiwa ni karibu ya kilometa 10, ambapo viongozi hao wote walishiriki mwanzo hadi mwisho pamoja na maelfu ya wananchi wa Jiji la Mwanza, Baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo mkubwa kwenye viwanja vya Furahisha, Dk. Slaa alisema kuwa Chadema inamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua kali wale wote walioliingiza taifa katika matatizo ya kampuni ya Dowans.
Alisema kuwa anaamini kuwa kabla ya kumaliza maandamano hayo ya siku tisa katika mikoa tofauti, Kikwete atatangaza kuwachukulia watu hao waliosababisha taifa kutaka kuilipa Dowans wakati kampuni hiyo ni haramu kutokana na Kamati ya Bunge kutamka kuwa mkataba wa Kampuni ya Richmond uliorithiwa na Dowans haukuwa halali.
"Tunajua kabla hatumaliza maandamano yetu ya siku tisa tuna imani kubwa kuwa (Rais) Kikwete atangaza kuwachukulia hatua waliohusika la sivyo wananchi watatumia nguvu ya umma kama nchi za Kaskazini ya Afrika ambako kuna wimbi la nguvu ya umma ambalo linawatoa madarakani viongozi," alisema Slaa.
Pia aliwaomba wananchi kuwazomea wabunge wote wa CCM watakapokuwa majukwaani kama walivyofanya wakati ule wa EPA, ambapo walikuwa wakiwazomea wabunge kila walipokuwa wakihutubia.
Naye Mbowe pamoja na mambo mengine ya kuishinikiza serikali kupunguza bei ya umeme na kutoilipa Dowans, aliwataka askari wote kuielewa Chadema na kulinda maslahi ya umma badala ya kuwalinda mafisadi wachache wanaoimaliza nchi kila uchao.
"Askari mgome kuwapiga watu, kama Misri askari waligoma kabisa kuwapiga watu, lakini Arusha askari walikubali kuwapiga ndugu zao risasi wakati hawakuwa na hatia," alisema Mbowe.
Mbowe alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, kwa kukubali maandamano hayo na kutowapiga mabomu watu wa Mwanza tofauti na Arusha ambako polisi wa huko kila mara wamekuwa wakiwapiga mabomu wananchi wa huko.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godobless Lema, naye alikuwepo katika maandamano hayo alilaani polisi wa Arusha kuwapiga wananchi kila uchao, ambapo alisisitiza kuwa wananchi wa Arusha sasa hawaogopi mabomu ya machozi na wanayaona kama manukato tu.
 
Tunaoijua mza tumekaa kimya wewe kuku wa maziwa ndo unajiongelesha kwamba hiyo sio chochote. Viva chadema ViVa wana mwanza walizoea kusema wasukuma wamelala sasa wanahaha baadaa ya kuona kumbe harati za ukombozi mpya wa TZ zimezaliwa mwanza.
Jana wanachadema tumezindua AZIMIO LA MWANZA na tunapinga MALIPO YA DOWANS, UPANDAJI WA GHARAMA ZA MAISHA,NA KATIBA MBOVU

yes, mapinduzi ya kweli yataanzia Mwanza
 
nyingi huanza na mbili. Ninavyofahamu population ya jiji la Mwanza hawa walioandamana si lolote si chochote, hao ni majobles tu, maduka mangapi yalifungwa wenyewe wakaenda kuandamana, masoko yalifungwa??wangapi waliondoka makazini?? vyuo/shule ngapi zilifungwa ?? Si chochote si lolote, msiige tembo kunya...nguvu ya wanachi haitatokea TZ, Watanzania wana akili bwana...CCM Oyeee!!!!
Sikio la kufa.....
 
nyingi huanza na mbili. Ninavyofahamu population ya jiji la Mwanza hawa walioandamana si lolote si chochote(chochote ni hayo ****** yako?), hao ni majobles tu, maduka mangapi yalifungwa wenyewe wakaenda kuandamana, masoko yalifungwa??wangapi waliondoka makazini?? vyuo/shule ngapi zilifungwa ?? Si chochote si lolote, msiige tembo kunya(tuige huo utumbo wako? MTHENGE wewe)...nguvu ya wanachi haitatokea TZ(Itatokea huko kwenye kengele zako), Watanzania wana akili bwana(mfn makamba,wewe,riz,RA,JK n.k,Kweli wewe ni zezeta)...CCM Oyeee!!!!(kamwambie kunduyo)./QUOTE]
Punguza hasira atakuwa kaelewa!
 
Hata wao wenyewe CHADEMA walishangazwa na idadi ndogo ya watu waliojitokeza. Amini usiamini, watu walidhani Mwanza pangechimbika na biashara kufungwa.....hakuna lolote magari yalipita kama kawaida, watu waliendelea na biashara na kazi kama kawaida. Maoni ya wengi waliona ni kupoteza muda tu, mtu aache kutafuta riziki yake na watoto aandamane akapigwe jua!
Wengine walisema mbona hao viongozi wa CHADEMA hatujawasikia wakitoa posho au mishahara yao kwa wananchi kama kweli wana uchungu huo? Mbona hawajakataa ile mikopo ya millioni 200, na milioni 90 za magari? Lema anaongea tu, mbona mkopo kavuta?
Watu wamekuwa wajanja, wameona wanatolewa kama chambo, viongozi wakitoka hapo wanakutana Tilapia au TAI FIVE WANAGONGANISHA GLASI ZA MVINYO,,, WALALAHOI WANARUDI MILIMANI AMBAPO HATA UMEME HAKUNA!
Acheni kuwapotezea muda watanzania. Amani iliyopo tuilinde wote.
 
Nchi yeyote ile haiwezi kuendelea kwa kuwa na kiongozi kilaza asiyejua wajibu na majukumu yake
kwanza huyo kiongozi atolewe, then wananchi watafanya kazi kwa nguvu safi tu maana watakuwa na viongozi watakao waongoza
Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.
 
Badala ya kupoteza KODI zetu kwenye mambo yasiyo ya msingi kama maandamano, ni bora muhamasishe watanzania wafanye kazi kwa bidii.

Maendeleo yanaletwa na kazi na siyo maandamano.

Hiyo ndio line peke yake unayoiongelea humu ndani, wakati huo watu wapo mtaani wanaandamana. Tayari sukari imeshushwa bei. Na bado wananchi wanaanza kuhamasishwa taratibu.

Huna raha kabisa mkuu kulikoni? Unakumbuka ya Misri na Tunisia eh? Hiyo ndo count down to mapinduzi ya kweli!!!
 
Mkuu, hapo juu palipokolezwa ulimaanisha hayo maneno au ulipitiwa tuu..siamini kama Watanzania tumefikia hatua hii ya ubaguzi wa kitabaka. Unataka kutugawa kati ya walionacho na wasio na kitu..kwamba Tanzania ndipo ilipo kwa sasa. Jamani tutambue kwamba Mtanzania ni Mtanzania, na wala si Mkenya, Mmarekani, Mwarabu au Mmyama..kila taifa lina namna yake ya kuwatambua na kuwaheshimu raia wake.

Umetafsiri vibaya mkuu wangu, tufanye kazi badala ya kupoteza muda kwa maandamano yasiyo na tija!!!
 
Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.

Hivi hawa bado nipopo na Zemarcopolo ni kina nani naomba watalamu wetu muwatafiti manake mi nashindwa kuamini kama tz k una watu disgn hii natoa rai wachunguzwe, hawa naweza kusema ni empty brain minded people au kina Ridhiwan na January sio bure, sababu mtz mwenye akili timamu awe fukara au tajiri hawezi kutoa commet za hivi. Na wana jf naomba mjue watu kama hawa hawatufai hata kidogo, naomba hawa jamaa wafutwe kabisa yaani wanakera
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom