Kweli watanzania sasa tuko njia panda,kondomu mpaka makanisani na misikitini?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Sikuamini kwamba nilichokuwa nakiona na kukisikia ni kweli.Sheikh kukubali matumizi ya kondomu kwa waumini wake na Maaskofu nao kuzikaribisha makanisani huku wakijua wazi kwamba ni kinyume kabisa cha maagizo ya Mungu.Hii ni kali ya millenia.Kwa mtu mwenye akili timamu,akili ambazo hazija haribiwa na mazingira ya kileo ya kifirauni,hakuna mjadala kwamba matumizi ya kondomu ni kinyume kabisa na hisia,maumbile na hata maagizo ya Mungu,na kwamba hatma yake ni kuzidisha uzinzi na uasherati na wala sio kupunguza.

Tukumbuke kwamba kitendo cha uzinzi au uasherati ndicho cha msingi na ambacho hakikubaliki,kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha maagizo ya Muumba wetu.Aliye geuza kibao na kutuambia kwamba ukimwi ndio kitu cha kujali zaidi kuliko Muumba wetu,anatutakia laana kabisa na anapashwa kukataliwa kwa nguvu zetu zote.Swala la kupata mimba au ukimwi ni la ziada tu na wala sio jambo la msingi sana.Ni wale tu wenye tamaa za mwili za kupindukia, tamaa zinazotawaliwa na mashetani,ndio tu wanaoweza kushabikia matumizi ya kondomu. Mwanadamu wa kawaida ana kiasi,sasa huyu mwanadamu wa leo ametoka wapi?

Lakini upuuzi huu ambao sasa hata wale tuliowategemea watuongoze kiroho wametekwa nao umetoka wapi?Ni kwamba, kwa siri mawakala wa mashetani wamepenyeza mawazo yao potofu,na sisi kwa ujinga tulio nao tumeupokea bila kuhoji.Athari zake ni nyingi katika jamii lakini directly or indirectly ni pamoja na ngono kuzidi katika jamii,ndoa nyingi kuvunjika,mimba mashuleni kuzidi,ukimwi kuongezeka n.k.n.k..Mwenye akili anaelewa kwamba wanapo onyesha mbele ya kiganja wana maanisha nyuma ya kiganja!

Angalizo langu ni kwamba tusiposimama imara na kukataa mafundisho yaliyo kinyume na ubinadamu wetu, laana ya Mungu iko juu yetu.Ni vema basi tukaogopa kuangukia kwenye laana na hasira ya Mungu,inatisha sana.

OLE WAO VIONGOZI WA DINI AMBAO SASA WAMEAMUA KWA MAKUSUDI KABISA KUPOTOSHA UKWELI,HUKUMU YAO ITAKUWA KUBWA ZAIDI!
[/COLOR][/COLOR]
 
Nyekundu ndio msisitizzo..!??
ilibidi ukemee pale pale kwani nahisi we ulikuwepo mahali hapo. unapoileta iyo mada hapa intuelimisha lakini vizuri zaidi ungewakemea hao viongozi palepale walipokuwa wakizinadisha hizo kondomu.
 
Kuna viongozi wa dini zingine hawaruhusiwi kuo hivyo wameshauriwa kutumia kondom kwavile wapenzi wanaokutana nao wana wenzao.Jamani waruhusini hao viongozi wawe na wake kwani hali inatisha sana!
 
Katika mika hii makanisani kuona kondom sio issue ukumbuke wezentu wanakwenda na wakati hilo sio kubwa sasa ukiwa unashabgazwa na mambo ya kondom hili la kuwepo maprist gays na kuambiwa kuwa ugay ni wake lakini akiwa kanisani anamtumikia mungu , ukija kwa mashekhe nikweli itakuwa ni mshangao kwani hakuna mtu wa kubadilisha au kurelax mambo yaliyoandikwa ndani ya quran na wao wanaelewa kufanya hivyo ni kupiga kauli za Mmungu.
 
Sikuamini kwamba nilichokuwa nakiona na kukisikia ni kweli.Sheikh kukubali matumizi ya kondomu kwa waumini wake na Maaskofu nao kuzikaribisha makanisani ..
Wapi huko na lini? Mbona ipo nusu nusu? Ikamilishe basi tusijeanza kujadili yasiyokuwapo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom