Kweli wanaume wengine kazi ipo ......

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Baba X aliondoka nyumbani kwake miaka 7 iliyopita na kuambatana na nyumba ndogo yake,na kumwacha mkewe akiwa mjamzito miezi tisa na watoto wakubwa wawili, ,bila hata huruma,na hakuwa na mawasiliano yoyote kujua wife na wanawe wanaendeleaje,
,mama wa watu alijifungua mtoto wake salama maisha yakiwa magumu na kuwalea wanae kwa taabu akifanya biashara ya kuuza mboga mboga , mungu si athumani kasomesha mwanae mkubwa sasa yuko form five ,mwingine form two,Na yule alokuwa tumboni sasa yuko la kwanza ,
Juzi mama wa watu akiwa anaandaa chakula mara mmewe huyo after seven years aliyowatelekeza..
Mama kwanza alidhani kaona mzuka na kuanguka chini huku fahamu zikimpotea ,,
Baada ya kuzinduka anakuta jamaa analia huku anaomba kusamehewa.....
eti shetani ndo alimpotosha ,anatubu dhambi zake na sasa anaomba wasameheane waanze upya..:hatari:

Kama wewe ndo mwanamama ulokumbwa na dhahama hili ungefanya maamuzi gani???:A S-coffee:
 
Unaongelea miaka saba tu? Watu waliachwa 14 years, na baba akiwa na mihela hiha akawa anajiita Mkapa.
Baada ya kufulia njemba ikarudi home kinyemela na wakaipokea.
thats life, real life.
Cha muhimu mama aitoe u-home kwa afya zaidi.
Wamwache tu aishi hapo sasa ataenda wapi na umri huo?
 
Kwakweli ingekua mie ningesema basi sababu hakua na mapenzi ya kweli na mimi,Ulie okota nae kuni ndio unaota nae moto sasa huyu ajipange kivyake tena kaja mifuko imetoboka aende tena hata nyuma asiangalie loh ......
 
Acheni hizo, maisha yako hivyo. Mungu huwa ana mipango yake kwa kila jambo linalotokea. Ningepanda kama mkisoma kitabu kinachoitwa "the power of now" na "power of letting go" Ni vizuri vinaelezea namna ambavo tunatakiwa kuishi kwa kupractise letting go. Hata kama huyo mwanaume asingeomba msamaha na kuamua kuishi kivyake lazima kuna hisia atazipata mamaa. Kumbukeni wamezaa nae watoto 3! Halafu kwa wanawake mnatakiwa kujua kuwa mumeo naye ni mwanao eeeh! Ukimsamehe ni kama umesamehe mwanao!
Ningekua mimi ningemsamehe na kuanza kuishi kwa tahadhari.
 
Kumsamehe ndio jambo muhimu kabisa ili asije akajiumiza kihisia, lakini baada ya hapo kila mtu awe na maisha yake, kama alimudu kuishi peke yake na kulea wanae kwa miaka 7, ni dhahiri hahitaji msaada wake tena.................... aachane naye na asonge mbele na maisha............
 
Unaongelea miaka saba tu? Watu waliachwa 14 years, na baba akiwa na mihela hiha akawa anajiita Mkapa.
Baada ya kufulia njemba ikarudi home kinyemela na wakaipokea.
thats life, real life.
Cha muhimu mama aitoe u-home kwa afya zaidi.
Wamwache tu aishi hapo sasa ataenda wapi na umri huo?
:poaaseeee!!!:poa
 
...ebo? anaomba kusamehewa kitu gani?...
kwani alichukuliwa msukule?...
9100590-cartoon-zombie-isolated-on-white-his-brains-are-sticking-out-of-his-head.jpg
 
jee kwa upande wa m.me mngesamehe?kama hayo aliyoyafanya ni m.ke?kila mtu na moyo wake,kwa upande wangu nitamsamehe maana kuwekeyana vinyongo sio vizuri.ila kwa upande wa ndoa haitokuwepo tena.maana nitakuwa nimeshayazoea maisha yangu mwenyewe bila yeye.miaka 7 ni mingi.hee kwani nimeambiwa yupo?wapo.nita focus na wanangu tu na sio yeye tena
 
Mhhhhh!!! yahitaji Mungu kumsamehe mtu kama huyu. Nafikiri kwa msaada wa Mungu naweza kumsamehe, ila nafikiri sitaweza tena kuishi naye kama mume na mke. Ni ngumu sana.................
 
Mimi namkaribisha tu,Ila ndoa hamna.

Sasa mpendwa, ukimkaribisha mwanaume 'aliyekuwa mumeo" miaka saba iliyopita, unadhani atakuacha wewe uendelee na maisha yako? Lazima atalazimisha ndoa na baada ya muda hata jamii yako itakushangaa kwanini unambania "mumeo". Ukimkaribisha ukubali vyote.Kama hutaki ndoa usimkaribishe ndani mwako maana utakuwa unakaribisha kifo!Wanawake na wanaume tumeumbwa tofauti sana.
 
Back
Top Bottom