Kweli Waafrika Ndivyo Tulivyo - We Aint 'Capitalist Niggers'!

Wakuu, hizi thread zinazohusu 'sisi tulivyo' huwa ngumu sana kuzisoma bila kufedheheka kinamna moja au nyingine.

Mimi ilinitumia zaidi ya mwaka kuweza kupata jibu fupi la "je, waafrika ndivyo tulivyo?"

Jibu nililokuja nalo niliamua kuliweka kama signature yangu:

Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi.

Kutoka thread mbalimbali zilizowahi kuzungumzia hili swala niliahidi kujibu siku moja kwa kirefu maono yangu. Lakini kwa vile ni mvivu wa kuandika marefu, ilinibidi nijipinde na ku-compress kila kitu na kupata hayo juu. Ndiyo maana mara kwa mara nimeshajaribu kutumia hiyo sentensi kama jibu langu la hoja mbalimbali ziibuliwazo hapa JF.

Ahadi zangu za kuandika kirefu niliifanya: HAPA na HAPA na HAPA na HAPA na HAPA na HAPA na HAPA na HAPA

.... ni nyiiiiingi. Nami ndivyo nilivyo!

By the way, hapo juu kwenye hitimisho langu suala la binadamu na mazingira (taming the environment) linaonekana kutokugusiwa. Nimefanya hivyo makusudi kwasababu argument katika hili jambo iko neutral, na mara nyingi ni self defeating.

Ahsanteni.

SteveD.
 
Well tumeachana navyo kwa sababu tu wajinga! Kama kuna kipindi tulikuwa tunatengeneza hayo Manyumbu (nadhani yalikuwa malori) enzi hizo sasa hivi usikute wangekuwa wamesha transition ktk kutengeneza passenger cars kama sedan na SUV...

Na kwa kuongezea... Hili linawezekana kam kuna nia ya kweli...Wahindi mbona wameweza kuwa na gari yao from TATA lorries hadi PSV tena ya bei poa.Huenda kama unavyosema hadi sasa tungekuwa mbali sasa.
 
Steve knowing ni is a necessary but sufficient condition for a society not stagnating/Kujua ni muhimu lakini hakutoshi kuifanya jamii isidumae

Nyani kwa hiyo kabla hatujaachana na kutengeneza bidhaa zetu wenye, yaani wakati tunatengeneza nyumbu n.k., tulikuwa hatukuwa kama tulivyo sasa - wajinga - na je hiyo sio hoja tosha ya kuonesha kuwa ujinga sio asili yetu?
 
Je, unamaanisha kuwa unaweza kujua kitu (cha kukudumaza) lakini usiwe na jitihada za kukukwamua/kukuondoa wewe kutoka kwenye huo mdumao?
 
Je, unamaanisha kuwa unaweza kujua kitu (cha kukudumaza) lakini usiwe na jitihada za kukukwamua/kukuondoa wewe kutoka kwenye huo mdumao?

Namaanisha unaweza ukajua na ukafanya jitihada na bado ukabaki umedumaa - kwani waafrika bado hatujui vinavyotudumaza? Tulipokuwa tunapigana na maadui wakuu watatu wa maendeleo: umaskini, ujinga na maradhi (Mwalimu aliongeza adui mkuu wa nne - rushwa) ina maana tulikuwa hatujui kinachodumaza? Sasa inakuwaje bado tuna umaskini, ujinga, maradhi na rushwa iliyokithiri mpaka sasa tunaiita ufisadi?
 
Kwa nini tu wajinga? Je ni asili yetu kuwa wajinga? Ndivyo tulivyo - wajinga?

Hapana mkuu. Sisi Waafrika sio wajinga. Hatuli mchanga wala hatujipaki kinyesi. Tatizo letu ni uzubafu. Tumezubaa. Au ni vilaza. Tunazinduka wakati watu wote wengine wameshatuacha nyuma sana.

Ndo hilo tu tatizo letu.
 
Namaanisha unaweza ukajua na ukafanya jitihada na bado ukabaki umedumaa - kwani waafrika bado hatujui vinavyotudumaza? Tulipokuwa tunapigana na maadui wakuu watatu wa maendeleo: umaskini, ujinga na maradhi (Mwalimu aliongeza adui mkuu wa nne - rushwa) ina maana tulikuwa hatujui kinachodumaza? Sasa inakuwaje bado tuna umaskini, ujinga, maradhi na rushwa iliyokithiri mpaka sasa tunaiita ufisadi?

Mkuu tuko pamoja na ahsante kwa jibu lako. Basi, na ndipo hapo nami nilipoamua kuchukua maneno manne ambayo yote yanaelezea jinsi gani mafanikio (ya matendo) hupatikana katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga, maradhi na hata rushwa.

Uki-balance namna ya kuitumia dharau, ubinafsi, chuki na ustaarabu katika hayo manne uliyoyaelezea utafanikisha malengo yako. Usipokuwa na uwiano ulio thabiti utateteleka na kudumaa!

SteveD.
 
Nyani kwa hiyo kabla hatujaachana na kutengeneza bidhaa zetu wenye, yaani wakati tunatengeneza nyumbu n.k., tulikuwa hatukuwa kama tulivyo sasa - wajinga - na je hiyo sio hoja tosha ya kuonesha kuwa ujinga sio asili yetu?

No, we were just going through the motions and that's why we reverted back to being who we were (are) by stoping doing those things. You can't go against nature for long.
 
Naomba kuuliza swali la kizushi.

Kwanini wakati tunapata uhuru, Waafrika hatukuamua kuachana na mambo yote ya kigeni na kurudia maisha/utamaduni wetu tuliokua tunaishi kabla ya utumwa?

Kwanini hatukuvua mashati, suruali, blouse, sketi, gauni, kanzu, soksi, chupi na kuvaa manyanga, majani kisha kuondoka mijini na kurudi maeneo yetu ya asilia?
 
Jibu la swali lako linahusiana na tafsiri uliyonayo mtu kuhusiana na utamaduni, maendeleo na kupata uhuru. Wamaasai wengi mbona bado wanajali sana utamaduni wao na kuendelea kuthaminiwa?
 
No, we were just going through the motions and that's why we reverted back to being who we were (are) by stoping doing those things. You can't go against nature for long.

Actually Nyumbu ni project ya jeshi inayojihusisha na automotive and engineering works. Bado wanadunda. Just this week walikuwepo viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maonyesho ya Public Service wamedisplay electric brick-making machine among other things.
 
Jibu la swali lako linahusiana na tafsiri uliyonayo mtu kuhusiana na utamaduni, maendeleo na kupata uhuru.

Wewe unavitafsiri vipi hivi vitu?

Wamaasai wengi mbona bado wanajali sana utamaduni wao na kuendelea kuthaminiwa?

Safi sana. Kwanini Wamasai wote hawaishi maeneo yao asilia, hawavai mavazi yao asilia na kuongea kimasai? Kwanini hawakufanya hivi wakati wa uhuru? Kwanini Waafrika wote wa makabila yote hawakufanya hivi wakati wa uhuru?
 
Wewe unavitafsiri vipi hivi vitu?

Safi sana. Kwanini Wamasai wote hawaishi maeneo yao asilia, hawavai mavazi yao asilia na kuongea kimasai? Kwanini hawakufanya hivi wakati wa uhuru? Kwanini Waafrika wote wa makabila yote hawakufanya hivi wakati wa uhuru?

Tafsiri yetu ya maendeleo na uhuru ikiwa tofauti na jamii kama zile za Wachina, Wahindi, Waarab, Wasomali, Native Americans na Wazungu wa aina yote, then nasi ingelibidi turudie manyanga na kuvaa majani. Otherwise, if same then kupata uhuru hakubadilishi matamanio ya binadamu licha ya kuwa na tamaduni zao.
 
I love this prediction! Any timelines?

Signs of the times are everywhere.
And there's a brand new feeling in the air.
Keep your eyes upon the eastern sky.
Lift up your head, redemption draweth nigh.

Law separating business and politics coming, says PM Pinda

By Bilal Abdul-aziz

19th June 2009

PindaBungeni.jpg

Prime Minister Mizengo Pinda

Prime Minister Mizengo Pinda yesterday informed the National Assembly that new legislation on separating business and politics, as directed by President Jakaya Kikwete will be ready before the next general elections.

Fielding direct questions from Members of Parliament here, the premier said the process towards drafting the law was in an advanced stage and he was certain
that a Bill for the same would be tabled in the House and new legislation enacted before going to the polls next year.

"The process has reached final stages; I cannot tell you that the Bill will be brought to Parliament in the next parliament meeting, but I am certain that it will be ready before general elections," said Pinda.

The PM, who was responding to a question from Victor Mwambalaswa (Lupa, CCM), cautioned however, that legislation was not the only effective way to fight dishonesty among leaders.

"We must fight temptations within ourselves," insisted the premier. In his question, Mwambalaswa suggested for the immediate adoption of a new law to implement the head of state's order and thereby curb dishonesty among political leaders.

Meanwhile, Prime Minister Pinda appealed for patience from lawmakers and the general public as the government finalised preparations for implementation of the National Identity Cards project.

Responding to Beatrice Shelukindo (Kilindi, CCM) he said: "It's true that the project has taken long and is yet to be completed, but it has gone very far. It is now at the level of cabinet for final decision."

The lawmaker had demanded explanation from the government over failure to complete the project after about 22 years.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
Ive lost hope Mkuu!
When u hear a law on this or that.. I dont think it will bring any more hope to the hopeless.
To me its more of rhetorics...
Can u reflect as to what it will entail to lift the wagon back on track and let it move? It will require massive overhaul of almost the entire system.It will mean purgings that you can never phantom!
Anyway..miracles do happen.
 
Waafrika wamekulia katika natural abundance, kwa hiyo hawakuwa na uchoyo naturally. Central theme ya Capitalism ni uchoyo, everybody for himself, Waafrika baba mmoja akisoma na kuwa wa kwanza kufika Chuo Kikuu ukoo mzima utahamia kwake, na hawezi kuwafukuza, hatimaye kila kitu kinakuwa bogged down, tunaendekeza welfare system, etc.

Wenzetu wameanza kufukuzana na wanyama wakali kwenye mapango ya Ulaya huko, huku wakipigana na baridi kali, wakajua principle ya "everybody for himself" zamani sana, wakaanza mashindano zamani sana, mashindano haya ndiyo yaliyo waletea maendeleo.

Kwa hiyo kwa mtazamo wa utu, waafrika tumewazidi watu wa west, kwa mtazamo wa kiuchumi wa west wametushinda waafrika.

Kwa sababu ya choyo, sisi hatuna choyo wao wana choyo.

Hata baba akija kumtembelea mwanae (kama baba hajawekwa nursing home) anaonekana nuisance na swali la kwanza ni "Unakaa siku ngapi?".Swali hili kiafrika ni tusi!

Watu wanapimiana kila kitu, kuanzia vyakula mpaka dakika anazooga mtu bafuni, sisi afrika tulikuwa tunaangua maembe mtini tu na kuoga mtoni.

Kwa hiyo kinachotutofautisha ni choyo, na choyo kimekujaje? Kutokana na mazingira.

BluRay:

Nilitaka ku-comment hii last night lakini maboksi yalinipeleka kitandani haraka sana.

Nina classmates wangu wazungu. Nilisoma nao Europe na wote tulihamua kuzamia maboksi Marekani.

Toka wamefika hapa hawana mpango wa kurudi kwao na hawaoni kuwa wana-miss sana kuachana na ndugu zao. Na pesa wanazotengeneza hapa ni kwa ajiri ya matumizi yao.

Nikirudi kwa upande wangu bado nani attachment ya Tanzania na ndugu zangu. Na kuna risk nyingi za investments siwezi kuzifanya kwa sababu nikianguka kuna watu nao wataanguka.

Kikwete alipokuja hapa kwa mara ya kwanza kama rais. Wosia wake kama rais akatuambia tukumbuke kujenga nyumbani. Na watu wakampigia makofi. Na sababu kubwa ni kuwa ukifariki watu wakirudisha maiti wasikute vibanda.
 
SteveD,
Bila shaka vitu vyote hivi vinategemea na utamaduni gani unaozungumzia. tanzania tulikuwa na makabila 120 na watemi wasiopungua 50 wa makabila makubwa..Sasa sielewi ni utamaduni upi ungetumika tofauti na wenzetu Wachina, Mazungu na wengineo ambao baada ya kudai uhuru wao walirudi ktk tamaduni zao kirahisi..
Nadhni ndicho walichokiona waasisi wa Uhuru wetu kwamba Muungano wa makabila haya ulikuwa muhimu kwanza kabla ya kutafuta utamaduni upi utaweza kuendana na mazingira yetu ndipo mwalimu kwa fikra zake akaja na huo Ujamaa wa Kiafrika ambao pia haukuwa kitu kigeni..
Mimi naamini kabisa kwamba mategemeo ya watu wengi hasa viongozi wetu ilikuwa wao kuchukua nafasi ya mkoloni yaani wao kuwa watawala wafalme wasiotokana na ukoo ila kwa kutumia siasa. Na wananchi tulifikiria ubora wa kuwa huru.. tukazisoma ahadi za mwalimu kuwa binadamu wote sawa, hakuna Unyonyaji, ubwanyeye, ukabaila na kadhalika tukasema YES huu ndio Uhuru bila kuelewa kwamba mambo haya hayawezi kupatikana kirahisi ikiwa hatukuwahi kuwa na utamaduni huo.

Na ukitazama Royal family wa kiafrika leo hii karibu zote hazitokani na asili bali utawala baada ya Uhuru..na asikudanganye mtu hakuna royal family hata moja isiyokuwa na fedha (utajiri).ndio maana unaona kina Mwinyi, Karume na wengine wote wanajilimbikiza mali kujibu hoja ya Royal family.
Kwa nini hatukurudi ktk asili yetu hata mavazi, mkuu nadhani pia imetokana na utata uleule wa nini asili na utamaduni wa Mtanzania..Kati ya makabila 120 ni vazi lipi utasema ni la Mtanzania! tena tushukuru sana bahati tumebakia na lugha ya kiswahili laa sivyo tungepoteza hata Lugha zetu kama jamaa zetu wa Angola na hata Sudan walokuwa Arabanised..Utakuta katika nchi zote hizi zile kabila walioamua kurudi ktk asili yao ndio tunawaita washenzi wasiokuwa na maendeleo kwa sababu maendeleo kwetu ni kuwa na shati, viatu, suruali bila kusahau tai shingoni hata kama jua kali kiasi gani..Mwalimu alijaribu sana kutubadilisha hata mavazi kama kiongozi wa India na Punjab suit zao lakini tofauti inakuja kwamba hatukuwa na asili tena. hatukuweza kufuata nguo za Mchina sijui ChoNlai lakini tumekuwa rahisi sana kufuata nguo za Kizaire (Pedejee) na Kighana hasa kwa kina mama..Yaani bora kinachonipendeza ndio vazi la Mdanganyika. Hatukuitwa Wadanganyika bure mkuu wangu ni kwa sababu hatuna tena utamaduni ambao tunaweza kuuweka mezani mtu akasema bila shaka huu ndio Utanzania labda kiswahili pekee..nacho kinapigwa vita utafikiri ni part of Ujamaa wa mwalimu..
Hizi lugha za asili zinaanza kupotea, kizazi kinachokuja sidhani kama wataweza kuongea lugha yoyote ya makabila yetu bila kuunganisha na kiingereza au lugha nyingine... In the coming 40 yrs, bila shaka lugha za asili pia zitapotea..Kiswahili chetu kitakuwa kibovu kuliko hata Kenya ambao sasa hivi wamekichukua kama lugha yao..
Ni rahisi sana kuona tunakokwenda lakini mara zote hatutaki kutazama nyuma kwani tunaogopa kugeuka mawe!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom