Kweli ukitaka kuua biashara ya mtu kwa waafrika tumia njia hii!

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,305
13,265
Yaani nimeamini kama una ugomvi wa kibiashara na mfanyabiashara mwenzako ,mbinu ambayo itakurahisishia mkakati huo ni kusema kuwa bidhaa hiyo ina punguza nguvu za kiume! na watu wakaamini hivyo utakuwa umemumaliza mshindani wako.

Hili suala kipindi cha nyuma lilishawahi kutokea kwenye ile juice ya super dip kwa wale wanayoikumbuka paketi moja unachanganya na maji ndoo moja. Ilitokea kupendwa sana miaka hiyo, pale waliposema kuwa inapunguza nguvu za kiume tu ndio ikawa mwisho wake!

Mfano mwingine ni hivi vyandarua vinavyogawiwa na serikali, watu wanavichukua na kuviweka ndani tu, na wengine wanatumia kuvulia samaki! kisa vinapunguza nguvu za kiume, na hata watoto wa kiume wameshakatazwa na wazazi wao kuvitumia.

Kuna sehemu moja nimekwenda wameshahamia kwenye hizi AZAM COLA, wanasema nazo zinapunguza nguvu za kiume! eti kutokana na gesi iliyomo, kwani soda gani kila uifunguapo gesi haiishi! Mpaka wiki bado inafuka gesi!

KWELI WA AFRIKA TUNAJARI SANA ILE "KAZAENI MUONGEZEKE".NA KIBAYA ZAIDI WATU WAKISHA JAZWA FIKRA HIYO KUWA BADILISHA TENA UFANYE KAZI TENA YA ZIADA
 
ajabu habari hizi zitaua biashara fast
mimi niliambiwa juice za sayona zinapunguza nguvu za kiume
ingawa najua ni uwongo,sijanunua tena lol
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! mweeeeeeeeeeeeeeeeeee! ngoja nikalale tu sasa maana kadiri muda unvyoenda na vituko ndo vinazidi, mweeeeeeeeeeeeeeee! ila poa ngija nipunguze machungu ya haya matokeo ya igunga, hii misukuma nayo sijui vp!!!
 
mimi nimekumbuka zile sumaku za kwenye mikanda eti nayenyewe ilidaiwa inaua nguvu za kiume
 
sasa kama nauza matairi ya gari, nitauaje biashara ya mpinzani wangu mwafrica? Au niseme matairi ya duka lile ukinunua unapoteza nguvu za kiume?
 
mtoa mada anamaanisha vyakula ndugu yangu kaeleweka mbona.
sasa kama nauza matairi ya gari, nitauaje biashara ya mpinzani wangu mwafrica? Au niseme matairi ya duka lile ukinunua unapoteza nguvu za kiume?
 
Ahahahaahaah!!! Watu waoga kweli ktk suala la nguvu za kiume.
 
Unaposema kweli waafrika tumetumwa tukazaliane. Je ni mtu gani yeyote duniani ataambiwa kitu fulani kina madhara na asichukue hatua kabla ya hayo madhara?
 
mfumo legelege wa uongozi wa nchi unachangia kwa kiasi kikubwa. Manake mambo mengi hufanyika kiholela na hata bidhaa nyingi huingia sokoni kwa njia wanazojua wenyewe wafanya biashara. Ukijaribu kuchunguza utaona kuwa suala la imani linachukua nafasi kwenye ufanyaji wa biashara siku hizi.

Ukianzisha biashara yako na wapinzani wakikuzushia kuwa bidhaa zako feki basi huna ujanja, manake watumiaji pia wanathamini maisha yao, serikali na wahusika wako kimya, au wakiongea basi wanaonekana wanatetea maslahi yao, maana wananchi hawana imani nao tena kutokana na mambo yaliyowahi kutokea.

Niende mbali kidogo, kwa mfano hi meli iliyozama Nungwi kama mtu angejitokeza kabla na kusema kuwa haifai kubeba abiria usishangae mtu kutoka serikalini angejitokeza kuitetea na hata makaratasi kuthibitisha hoja zake tungepewa!!
 
TANMO, kuhusu hili la meli- SUMATRA walienda huko zanzibar na wakaikomalia kuwa ilikuwa haina sifa, kesho yake walituliwa na kuambiwa kuwa sumatra niya bara pekee.
mfumo legelege wa uongozi wa nchi unachangia kwa kiasi kikubwa. Manake mambo mengi hufanyika kiholela na hata bidhaa nyingi huingia sokoni kwa njia wanazojua wenyewe wafanya biashara. Ukijaribu kuchunguza utaona kuwa suala la imani linachukua nafasi kwenye ufanyaji wa biashara siku hizi, ukianzisha biashara yako na wapinzani wakikuzushia kuwa bidhaa zako feki basi huna ujanja, manake watumiaji pia wanathamini maisha yao, serikali na wahusika wako kimya, au wakiongea basi wanaonekana wanatetea maslahi yao, maana wananchi hawana imani nao tena kutokana na mambo yaliyowahi kutokea. Niende mbali kidogo, kwa mfano hi meli iliyozama Nungwi kama mtu angejitokeza kabla na kusema kuwa haifai kubeba abiria usishangae mtu kutoka serikalini angejitokeza kuitetea na hata makaratasi kuthibitisha hoja zake tungepewa!!
 
Ngoja nami nijaribu hili, huenda nitaokoa mamaia ya vijana wetu wanaokufa kila siku ama kupata ulemavu wa kudumu-BODABODA ZINAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME na KUONGEZA NGUVU ZA KIKE. Wana JF naomba muniungemkono na muache kununua bodaboda.
Ahahahaahaah!!! Watu waoga kweli ktk suala la nguvu za kiume.
 
Yaani nimeamini kama una ugomvi wa kibiashara na mfanyabiashara mwenzako ,mbinu ambayo itakurahisishia mkakati huo ni kusema kuwa bidhaa hiyo ina punguza nguvu za kiume! na watu wakaamini hivyo utakuwa umemumaliza mshindani wako.

Hili suala kipindi cha nyuma lilishawahi kutokea kwenye ile juice ya super dip kwa wale wanayoikumbuka paketi moja unachanganya na maji ndoo moja. Ilitokea kupendwa sana miaka hiyo, pale waliposema kuwa inapunguza nguvu za kiume tu ndio ikawa mwisho wake!

Mfano mwingine ni hivi vyandarua vinavyogawiwa na serikali, watu wanavichukua na kuviweka ndani tu, na wengine wanatumia kuvulia samaki! kisa vinapunguza nguvu za kiume, na hata watoto wa kiume wameshakatazwa na wazazi wao kuvitumia.

Kuna sehemu moja nimekwenda wameshahamia kwenye hizi AZAM COLA, wanasema nazo zinapunguza nguvu za kiume! eti kutokana na gesi iliyomo, kwani soda gani kila uifunguapo gesi haiishi! Mpaka wiki bado inafuka gesi!

KWELI WA AFRIKA TUNAJARI SANA ILE "KAZAENI MUONGEZEKE".NA KIBAYA ZAIDI WATU WAKISHA JAZWA FIKRA HIYO KUWA BADILISHA TENA UFANYE KAZI TENA YA ZIADA

Hivi wewe ukiambiwa bidhaa fulani unayotumia inapunguza nguvu za kiume na kweli ikathibitika hvyo, utaendelea kuitumia kwa kuwa wewe uko against na huo msemo wa 'nendeni mkazaliane muijaze dunia'? Kuna vitu vingine vinagusa maisha moja kwa moja wewe...!
 
Naskia hata hizi mboga za majani kama chainizi na spinach nazo zinapunguza nguvu za kiume..
 
sasa kama nauza matairi ya gari, nitauaje biashara ya mpinzani wangu mwafrica? Au niseme matairi ya duka lile ukinunua unapoteza nguvu za kiume?

Unadai kwamba Matairi yale ya mpinzani wako yanatumiwa na Sumry na Champion...
 
Back
Top Bottom