kweli Tanzania ni shamba la bibi

JBAM

Member
Feb 16, 2012
22
13
wakuu kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), asilimia 96 (96%) ya uvunaji wa mazao ya misitu unafanyika haramu kinyume cha sheria na taratibu na hivyo kutochangi kwenye pato la taifa. Ni asilimia 4 tu ya mazao ya misitu yanavunwa kihalali. Ikumbukwe kuwa kila mwaka zaidi ya hekta laki 4 za misitu hukatwa hapa Tanzania (kwenye shamba la bibi)
source: TBC habari ya saa mbili usiku huu.

Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele

Du kwa kweli "serikali lege lege haiwezi kukusanya kodi" by JK Nyerere.
 
Sasa kama Twiga na urefu wote ule, alikunjwa hadi akaingizwa kwenye ndege mchana kweupe, unafikiri nini kimebaki mkuu? Yetu macho.
 
halafu hapo hao jamaa wanaochoma mkaa ni kwa ajili ya kutusaidia tu na ukikutwa huko polini lazima umwagiwe maji ya betri kama adhabu we acha tu mikaaa yenyewe ikikamtwa inachukuliwa na wao wenyewe...
 
Back
Top Bottom