Kweli Tanzania ni Nchi ya amani

Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
392
Nasema hivi kwa sababu pamoja na matukio mengi yaliyaandama tangu uchaguzi wa 2010, matukio ambayo huleta hasira kwa karibu kila mtanzania huko maisha yakizidi kuwa magumu kila kukicha, ilhali matukio ya kifisadi yakirindima karibu kila sekta ya umma, na sasa kwa mbinu ya serikali kuwahi mahakamani ili jambo husika lisihojiwe zaidi kwa kisingizio kuwa suala liko mahakamani, hasa matukio ya hivi karibuni: madaktari, Dk. Ulimboka, walimu. Katika yote hayo wananchi tumekaa tu kimyaaa kama vile hakuna kilichotukia. Ndo maana nasema kweli Tanzania ni Nchi ya amani, vinginevyo hawa viongozi wangeshafurumushwa kwa mawe kutoka huko magogoni... maana inaleta hasira hadi kichwa kinauma... viongozi wanaotawaliwa na "sijui" nyingi, labda hata hawajui kwanini wako madarakani.
Kama sio amani, basi tunatawaliwa na uwoga...... sina nia ya kuhamasisha vurugu.. ila viongozi wana haki ya kuepusha vurugu kwa kutoa huduma stahiki kwa jamii.. vinginevyo ipo siku viti vitakuwa vya moto..
 
Hapana si nchi ya amani. JK ametuharibia nchi yetu na dream za kila mtu, ni kazi kuirudisha kazi mstarini
 
Hamna Amani ni nidhamu ya uoga tuu kwani Hakuna Amani pasipo haki kwa wote....kibaki alimuonya Jk kuwa siku watz wako wakitoka usingizini utakuwa hatarini kwani itakuwa Mara dufu ya zaidi ya yaliyotokea Kenya
 
Back
Top Bottom